f 52074 Ushirikiano baina ya nchi za kusini mwa Ulimwengu Mabadilishano ya Ujuzi na Uvumbuzi Baina ya India, Uganda na Tanzania Katika Sekta ya Maziwa The World Bank Yaliyomo f Vifupisho 1 Utangulizi 2 Muhtasari 3 Kwanini India? 5 Umuhimu wa maziwa 6 Jinsi gani mzalishaji mkubwa ametayarishwa India? 7 Uganda 9 Tanzania 11 Vifupisho f AI Artificial insemination AMUL Anand Milk Union Limited DC Dairy Corporation DCS Dairy co-operative societies DDA Dairy Development Authority EAC East African Community EPRC Economic Policy Research Centre FMD Foot and mouth disease GDP Gross domestic product GoT Government of Tanzania HPI Heifer Project International IFPRI International Food Policy Research Institute ILRI International Livestock Research Institute MAAIF Ministry of Agriculture, Animal Industry & Fisheries MUM Molasses-urea-mineral (blocks) NDDB National Dairy Development Board SALL SAMEER Agriculture and Livestock Ltd. UNDATA Uganda National Dairy Traders' Association UNDFA Uganda National Dairy Farmers Association UDISA Uganda Dairy Stakeholders Association (UDISA) UDPA Uganda Dairy Processors' Association (UDPA) UHT Ultra-high temperature Ushirikiano huu uliongozwa na: Michael Wong (South Asia Poverty Reduction, Economic Management, Finance and Private (SASPF)) na Moses Kibirige (Africa Finance and Private Sector Development). Wajumbe wengine ni: Sakm Abdul Hye, Suhail Kassim, Aza Rashid (all SASFP), Justina Kajange (WB-TZ), Peace Lwanga (WB-UG), Dr Kasim Mchau (mtaalamu elekezi) na Martin Fowler (mtaalamu elekezi). Mradi huu umefadhiliwa na: the South South Exchange Trust fund. Helena Nkole (TF Coordinator), Simon Bell, John Speakman na Ernesto May (management SASFP), John McIntire (Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Uganda na Tanzania) na Kundhavi Kadiresan (Country Manager Uganda) walitoa ushauri. 1 UTANGULIZI f Ushirikiano wa nchi za kusini (South-South cooperation) kuhusu mabadilishano ya ujuzi baina ya India, Tanzania na Uganda ulizinduliwa mwaka wa 2008, na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Robert Zoellick pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bi. Okonio Iweala Ngozi. Mabadilishano ya uzoefu yaliungwa sana mkono na Bi. Amrita Patel, Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini India (NDDB) na Bw. Shri B. M. Vyas, Mkurugeni Mwandamizi wa Muungano wa Ushirika wa Soko la Maziwa Gujarat Ujumbe wa Uganda, Tanzania na Ethiopia pamoja na Dr. Verghese Kurien, Baba wa (GCMMF Ltd) wa kule Anand, India. mapinduzi "meupe" ya maziwa. Lengo kuu la mradi huu wa kubadilishana ujuzi ( kwa kifupi, `South/South' ) ni kuboresha mikakati ya maendeleo, uzalishaji na ushirikishwaji katika sekta ya maziwa nchini Tanzania na Uganda. Zoezi hili lililenga kuongeza uzalishaji na unywaji wa maziwa. Malengo/matokeo ya muda mfupi zaidi ni: ushirikiano bora zaidi baina ya wafugaji wadogo wa ng'ombe wa maziwa; upatikanaji wa teknolojia bora na endelevu katika vituo vya kukusanya maziwa na viwanda vya kusindika maziwa; ushirikiano bora kati ya wafugaji na wasindikaji; kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara; na kuimarisha bodi za maziwa katika nchi husika. Serikali na wadau nchini Uganda na Tanzania wanatambua fursa zilizopo katika sekta ya maziwa. Sekta hii inaweza kuchangia kwa kiwango kikubwa kufikiwa kwa Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenea ( Millennium Development Goals) ya kupunguza vifo vya watoto na mama wazazi pamoja na kuongeza pato la kaya zilizopo mashambani. Sehemu muhimu ya ushirikiano huu ni kuongeza uelewa wa walengwa kuhusu mbinu za soko na jinsi ya kupanga bei ya maziwa ili kuweza kushindana na vinywaji vingine vilivyoko sokoni. Mradi huu umepitia awamu kadhaa. Katika awamu ya kwanza, walengwa walitembelea India mwezi Juni 2008, ili kubadilishana uzoefu, kuzungumzia mambo muhimu ya sekta, kupitia muundo wa uendeshaji, n.k.. Awamu ya pili wataalamu kutoka India walitembelea Uganda na Tanzania kwa siku tatu kila nchi na kushiriki katika warsha ya wadau. Hatimaye jopo za wataalamu zitaunganisha utekelezaji wa mradi huu pamoja na ule wa miradi mingine inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, kwa mfano: marekebisho ya sheria kuunganishwa na miradi inayolenga sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara; kuunganisha vyama vya wafugaji wadogo na huduma ya ushauri wa kilimo. 2 Muhtasari Mradi wa kubadilishana ujuzi baina ya India na nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ulizinduliwa mwaka wa 2008 ili kuwezesha mafanikio ya India katika sekta ya maziwa yaongeze kasi ya maendeleo kwenye sekta hiyo nchini Tanzania na Uganda. Washiriki walijionea wenyewe mbinu mpya za kuongeza uzalishaji, uuzaji na unywaji wa maziwa na bidhaa zake. Ujuzi huu pamoja na Ujumbe wa Uganda, Tanzania na Ethiopia utekelezaji wa mikakati hii utaongeza uhakika wa huko Gujarat India chakula / lishe pamoja na kipato cha tabaka la chini la jamii kwenye nchi hizi mbili. Ongezeko la uzalishaji wa maziwa nchini India linashangaza - takriban maradufu katika kipindi cha miaka 15 kuishia 2007. India inaongoza kwa uzalishaji wa maziwa duniani, ikichangia asilimia 15 ya thamani yote ambayo ni sawa na Dola za Marekani bilioni 20 kwa mwaka. Sekta hiyo ya maziwa ina wafugaji milioni 12 na wengine milioni 78 wana ajira katika mtiririko wa kuyaongezea maziwa thamani kabla hayajamfikia mlaji. Kitovu cha sekta ya maziwa ni vyama vya msingi vya ushirika wa wafugaji wenye vituo vya kukusanya maziwa vijijini. Hivi vimeungana kwenye ngazi ya wilaya kuunda vyama vikuu vyenye dhamana ya kuendesha viwanda vya usindikaji. Uganda na Tanzania ni nchi zenye nafasi nzuri ya kuzalisha maziwa kwa wingi lakini bado hazijaweza kutumia nafasi hiyo kikamilifu. Hata hivyo wakati Uganda inakisiwa kujitosheleza kwa maziwa, kiasi kikubwa cha maziwa yaliyo katika soko rasmi nchini Tanzania huagizwa kutoka nje. Uzalishaji unaongezeka kwa kasi nchini Uganda na sehemu kubwa ya maziwa yanayotoka kwa wafugaji, huingia kwenye sekta kubwa isiyo rasmi ambako husindikwa na kuuzwa sokoni kuziba pengo lililoachwa wazi na sekta iliyo rasmi. Sekta hii inaipiku iliyo rasmi kutokana na uwezo wake wa kuwalipa wafugaji bei kubwa zaidi na kumfikishia mlaji maziwa kwa uhakika na kwa bei nafuu zaidi. Matokeo yake ni kwamba viwanda katika sekta iliyo rasmi havipati maziwa ya kutosha na hivyo kuendeshwa chini ya uwezo wake kwa kiasi kikubwa. Nchini Tanzania napo uzalishaji wa maziwa unaongezeka, na sekta isiyo rasmi ni kubwa zaidi. Eneo la Afrika ya Mashariki na Kati lina soko la maziwa linaloshamiri. Kuna changamoto au mapungufu kadhaa muhimu yanayozuia maendeleo katika mtiririko wa ongezeko la thamani kwenye sekta ya maziwa nchini Uganda na Tanzania. Baadhi ya changamoto hizi zinafanana katika nchi zote mbili. Kwa mfano, kushindwa kwa sekta kukabiliana na tatizo la kuyumba kwa kiwango. 3 1 Muhtasari f cha uzalishaji kutoka msimu mmoja hadi mwingine, uhaba wa takwimu ambazo ni muhimu katika kuweka mipango na kuendesha sehemu mbalimbali za mtiririko wa thamani, uwezo mdogo na uchache wa vikundi vya wafugaji/wasindikaji/wafanya biashara viwe vya ushirika au umoja, na mtandao mbovu wa barabara vijijini. Changamoto nyingine zenye kusisitizwa zaidi Uganda ni pamoja na ufinyu wa huduma mbalimbali (zikiwemo mikopo, pembejeo, ushauri na mafunzo ya biashara) ambazo ni muhimu kwa ufanisi wa sekta, na matumizi haba ya teknolojia na mbinu bora za uzalishaji. Athari za mapungufu yote haya zinaongezewa na uhaba wa madaktari wa mifugo. Ukuaji wa sekta ya maziwa Tanzania unakwamishwa na wingi wa sheria na kanuni ambazo huongeza gharama za kuendesha biashara na pia mfumo wa kodi ambao unamwongezea mlaji mzigo wa bei ya bidhaa za maziwa yaliyosindikwa na sekta rasmi. Yote haya yanapunguza motisha kwa mwekezaji wa sekta binafsi. Uzoefu wa India unabainisha "chachu" kadhaa zilizochochea kasi ya maendeleo ya sekta ya maziwa nchini humo. Itakuwa muhimu kuzikumbuka hizi wakati wa kuandaa mipango ya maendeleo ya sekta za maziwa katika nchi hizi mbili za Afrika ya Mashariki. Muhimu zaidi kuzingatia ni: kupunguza kabisa kwa serikali kuingilia uanzishwaji na uongozi wa vyama vya ushirika (pamoja na kuhimiza ukweli na uwazi katika uendeshaji); kuweka sera, sheria na kanuni zinazolenga kupunguza gharama za kufanya biashara na kutoa motisha kwa wawekezaji; kuongeza ufanisi katika kuratibu sehemu mbalimbali za mtiririko wa thamani katika sekta ya maziwa; pamoja na kufanya utafiti wa kudumu wa masoko ili kuboresha soko la maziwa. Matumizi madogo ya teknolojia bora za uzalishaji 4 KWANINI f India? India imejitokeza kuwa nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa maziwa duniani. Mwaka wa 2007 dunia ilizalisha tani milioni 676 ambazo India ilichangia asilimia 15. Ilikuwa ni nchi isiyojitosheleza kwa maziwa miaka ya 1960 lakini ikawa imefikia tani milioni 100 mwaka wa 2007, na kuifanya sekta ya maziwa ndiyo inayoongoza katika kilimo kwa mapato. Uzalishaji kwa mwaka umekuwa Baada ya shule wanafamilia wakipeleka maziwa kwenye kituo ukiongezeka kwa kasi zaidi cha kijiji cha kukusanya maziwa. katika miongo miwili iliyopita. Kutoka tani milioni 56 mwaka wa 1991/92 hadi tani milioni 100.9 mwaka 2006/07 zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 20. Katika kipindi hicho upatikanaji wa maziwa kwa mtu mmoja kwa siku uliongezeka kutoka gramu 178 hadi gramu 246. India imeweza kupata mafanikio haya kwa kuwafanya watu wa kipato cha chini kuwa wazalishaji, wasambazaji na walaji wa maziwa. Wafugaji milioni 12 (wengi wao wakiwa wadogo, wa pembezoni au wasio na ardhi) wanazalisha maziwa. Hawa ni wanachama wa vyama vya msingi vya ushirika 122,500 vinavyo kusanya kilo milioni 23 kwa siku. Takwimu za NDDB zinaonyesha kwamba vyama hivi vinajishughulisha katika zaidi ya wilaya 346. Wanachama milioni 3.4 ni wanawake. Sekta ya mifugo inachangia asilimia 27 ya pato la taifa linalotokana na kilimo (agricultural GDP), ambapo asilimia 70 yake ni kutoka sekta ya maziwa. Inakisiwa kwamba sekta ya maziwa huchangia asilimia 4 ya pato la taifa na kuajiri takriban watu milioni 90, asilimia 83 yao wakiwa ni wanawake. 1 Hali ya chakula - Tathmini ya mwenendo wa soko duniani, May 2008 5 1 Umuhimu wa Maziwa Maziwa yanatambuliwa kama chanzo muhimu sana cha lishe bora katika vyakula vya watoto na watu wazima. Maziwa yana viini lishe tisa muhimu hivyo kuyafanya yawe moja ya vinywaji vinavyoongoza kwa virutubisho. Protini ya maziwa ina viini vyote muhimu vinavyohitajika na mwili wa binadamu. Maziwa pia yana kiwango kikubwa cha madini ya chokaa ambayo ni muhimu kwa mifupa imara, mishipa ya fahamu, misuli na kuganda kwa damu kwenye jeraha. Madini mengine ni pamoja na fosforasi ( muhimu kwa mi- fupa), potassium (kwa ajili ya misuli na damu) na sodium ( mishipa ya fahamu). Maziwa pia ni chanzo kizuri cha vitamini A (muhimu kwa ukuaji wa chem- bechembe za mwili na kinga ya mwili), vitamini B1, B2, B3 (muhimu kwa uzalishaji wa nishati mwilini), vitamini B12 (muhimu kwa mishipa ya fahamu) na vitamini D (muhimu kwa kufyonzwa kwa madini ya chokaa na fosforasi tumboni kutoka kwenye chakula na kuingia mwilini kwa ajili ya mifupa). Kutokana na kiwango-lishe kikubwa cha maziwa, inazidi kudhihirika kwamba vyakula vitokanavyo na maziwa vinachangia kuukinga mwili dhidi ya maradhi mengi. Kwa mfano, maziwa ya kutosha kwa watoto wa umri kati ya miaka mitatu hadi 13 huimarisha mifupa na kupunguza maradhi ya kuvunjika mifupa (oste- oporosis). Madini ya chokaa (kwenye maziwa) hupun- guza uwezekano wa kupata shinikizo la damu. Ulaji wa vyakula vya maziwa pia ni kinga dhidi ya kisukari (type 2). 6 India f Jisi gani mzalishaji anayeongoza nchini India alivyo shirikishwa? Sekta ya maziwa nchini India ni mfano mzuri wa muundo wa soko unaopendelea wanyonge. Wafugaji wameungana kwenye vyama vya msingi vya ushirika vijijini. Vyama hivi huendesha vituo vya kukusanya maziwa. Chama kikuu cha ushirika kwenye ngazi ya wilaya humiliki na kuendesha kiwanda cha kusindika maziwa. Chama cha Msingi cha Ushirika kwenye Kijiji: Chama cha msingi kina wastani wa wanachama wafugaji 300 hadi 400 kwa kijiji. Kila mwanachama ana hisa kwenye ushirika na hulipa ada kidogo kulingana na idadi ya ng'ombe alionao. Wanachama wamekubaliana kuuzia ushirika asilimia fulani ya maziwa wanayozalisha. Ushirika hununua maziwa ya kila mwanachama asubuhi na jioni. Bei ya maziwa hutegemea kiwango cha mafuta ya siagi baada ya vipimo vya papo kwa hapo kwa kila chombo. Malipo ya maziwa ya jioni hupatikana kesho yake asubuhi, na ya asubuhi hupatikana jioni. Watumishi wa Ushirika: Chama cha msingi hufanya uchaguzi wa mara kwa mara wa kamati ya usimamizi na mwenyekiti. Kamati huajiri wafanyakazi wa nusu siku kadhaa: katibu, mpokea maziwa, mpimaji, karani, mhamilishaji na mhasibu. Kamati ya usimamizi hukutana mara kwa mara na wanachama kupitisha mahesabu yote ya fedha. Vyama vingi hupata faida na kuwalipa wanachama gawio juu ya hisa. Chama Kikuu cha Ushirika kwenye Wilaya: Vyama vya msingi huunda Vyama Vikuu vya Ushirika kwenye ngazi ya wilaya. Hivi viko 170 kwa sasa na huuza maziwa kwenye miji mikubwa yote pamoja na zaidi ya miji 800. Jukumu lingine ni kulea chama kipya cha msingi hadi kiimarike kiuchumi - kwa kawaida ndani ya miezi mitatu hivi. Vyama vipya vya msingi hupewa mashine za kupima mafuta kwenye maziwa na Chama Kikuu bila malipo. Lakini zinapozeeka vyama vya msingi vinawajibika kujinunulia mashine mpya. Pindi chama cha msingi kinapoweza kujitegemea, Chama Kikuu kinapendekeza kisajiliwe na Idara ya Ushirika ya Jimbo ( kutokana mwelekeo wa kijamaa wa India, kila jimbo lilikuwa na shirika la kueneza ushirika). Lakini hata baada ya chama cha msingi kuweza kujitegemea, Chama Kikuu huendelea kukisimamia na kukipatia huduma mbalimbali pamoja na pembejeo. Idara ya Ushirika ya Jimbo hukagua mahesabu ya vyama vyote vya msingi vilivyosajiliwa, mara nne kwa mwaka. 7 1 India f Chama Kikuu cha Ushirika hukusanya maziwa kutoka kwenye kila kituo cha maziwa mara mbili kwa siku Market kwa malori. Vyama vyote vya msingi vimewakilishwa Markets milk and kwenye Chama Kikuu ambacho huendeshwa na milk products bodi ya wakurugenzi yenye wajumbe 19, ambao State Milk Federation 12 wanatoka vyama vya msingi na saba waliobaki ni pamoja na mwakilishi wa Idara ya Ushirika Milk ya Jimbo, mtaalamu wa maziwa, mwakilishi wa products taasisi za fedha, n.k. Bodi hufanya maamuzi yote Procures milk of member ya sera na kuajiri Meneja Mkuu anayesimamia societies, processes and shughuli za siku hadi siku. Mapato ya Chama markets within state Kikuu hutumika kwenye miradi mbalimbali kwa District milk union mfano uzalishaji wa mifugo bora. Milk Vyama vikuu vya AMUL hutoa huduma tiba ya mifugo kwa wanachama, uhamilishaji kwa ajili ya kuboresha mifugo, vyakula bora vya mifugo. Collects milk from Kulingana na imani ya AMUL kwamba mkulima producer members huthamini zaidi kitu alicholipia, wanachama at village wanalipia huduma na pembejeo zote Village cooperative society wanazopata. Producer members Kwa mfano, kila mwanachama analipa takriban Dola za Marekani mbili kila anapotembelewa na daktari wa mifugo. Asiye mwanachama hulipa Dola za Marekani 3.50. Huduma ya dharura inapatikana masaa 24. Aidha mwanachama mmoja kutoka kila kijiji hufundishwa huduma ya kwanza ya mifugo na kazi yake hukaguliwa kila wiki na madaktari wa mifugo wa AMUL. Madaktari hao wanamrejeshea bila malipo dawa zote alizotumia. Kwa kumalizia, Chama Kikuu hulipa asilimia 75 za gharama ya kuanzisha kituo cha kwanza cha huduma ya kwanza ya mifugo kwenye kila kijiji. AMUL inamiliki viwanda vya kusindika maziwa kupata bidhaa zisizoharibika upesi ikiwa ni pamoja na maziwa ya unga. Kwa hiyo mkulima anaweza kuongeza uzalishaji wa maziwa na akawa na uhakika wa soko na bei mwaka mzima. Zaidi ya maziwa, viwanda vya AMUL huzalisha bidhaa nyingine kama samli, vyakula vya watoto wachanga, jibini, n.k. Bidhaa hizi zinauzwa na AMUL nchi nzima. 8 Uganda f Changamoto za sekta ya maziwa nchini Uganda Changamoto au mapungufu makuu yanayo kwamisha maendeleo ya sekta ya maziwa kwenye nyanja za uzalishaji, usindikaji na masoko ni: Ufinyu wa motisha za kuingia kwenye soko rasmi la maziwa: Bado kuna motisha kidogo kwa wafugaji wadogo kuuza maziwa yao kwenye soko rasmi ukilinganisha na lisilo rasmi. Inabidi kuweka mkazo zaidi kuwashawishi wafugaji kuuza maziwa mengi zaidi kwenye soko rasmi na pia kusajili wale walio kwenye soko lisilo rasmi pamoja na shughuli zao. Juhudi za DDA za siku za karibuni zimeelekezwa kwenye maeneo hayo, kwa mfano kutoa mafunzo na usajili wa wadau wa sekta isiyo rasmi ili kuongeza ubora na usalama wa maziwa - badala ya kuwanyanyasa au kuwafungia shughuli zao. Matumizi kidogo ya teknolojia na mbinu mpya za uzalishaji: Sababu kubwa ya ongezeko kidogo la uzalishaji kitaifa ni kasi ndogo ya wafugaji kupokea na kutumia mbinu na teknolojia mpya za uzalishaji. Kwa mfano, ni asilimia 2 hadi 15 tu ya wafugaji wanaotumia uhamilishaji kutokana sio tu na gharama kubwa na ufinyu wa huduma yenyewe, bali pia na wasiwasi kuhusu tija. Sera ya serikali nayo imesababisha upungufu wa kiasi cha mbegu zinazoagizwa kutoka nje (inakisiwa kwa theluthi moja ya mahitaji halisi). Wakati huo huo, kuna mahitaji makubwa ya ng'ombe bora wa maziwa. Ni wazi kwamba kuna nafasi kubwa ya kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maziwa nchini kwa kuboresha mifugo hasa ikizingatiwa kwamba sehemu nyingi nchini zina mazingira mazuri kwa ajili ya kilimo na ufugaji. Kukosekana kwa huduma za kuweka na kukopa: Kuna haja ya kuwepo kwa huduma ya kuweka na kukopa kwa ajili ya wafugaji (kununulia pembejeona mifugo bora), wafanya biashara (kupata mtaji) na wasindikaji (kununulia vifaa na mashine za usindikaji). Huduma ya mikopo ni finyu na gharama (riba) yake ni kubwa. Uhaba wa huduma nyingine muhimu: Uhaba uliopo wa pembejeo, huduma za mafunzo, biashara pamoja na matumizi kidogo ya teknolojia na mbinu mpya za uzalishaji, athari zake zinaongezewa na upungufu wa madaktari wa mifugo. Ufinyu wa usindikaji: Sehemu kubwa ya kiasi cha maziwa yanayozalishwa kwa mwaka huharibika kutokana na kushindwa kuyasindika ili kupata bidhaa za thamani kubwa na zisizoharibika upesi (Keyser, 2009). Hii husababisha hasara kwa wafugaji na kupunguza pato la taifa kutokana na bidhaa zinazouzwa nje. Mfugaji pia anashindwa kutabiri pato lake la mwaka. 9 1 Uganda f Kukosekana kwa huduma za kuweka na kukopa: Kuna haja ya kuwepo kwa huduma ya kuweka na kukopa kwa ajili ya wafugaji (kununulia pembejeona mifugo bora), wafanya biashara (kupata mtaji) na wasindikaji (kununulia vifaa na mashine za usindikaji). Huduma ya mikopo ni finyu na gharama (riba) yake ni kubwa. Uhaba wa huduma nyingine muhimu: Uhaba uliopo wa pembejeo, huduma za mafunzo, biashara pamoja na matumizi kidogo ya teknolojia na mbinu mpya za uzalishaji, athari zake zinaongezewa na upungufu wa madaktari wa mifugo. Ufinyu wa usindikaji: Sehemu kubwa ya kiasi cha maziwa yanayozalishwa kwa mwaka huharibika kutokana na kushindwa kuyasindika ili kupata bidhaa za thamani kubwa na zisizoharibika upesi (Keyser, 2009). Hii husababisha hasara kwa wafugaji na kupunguza pato la taifa kutokana na bidhaa zinazouzwa nje. Mfugaji pia anashindwa kutabiri pato lake la mwaka. Ufinyu wa miundombinu: Miundombinu inayotumika katika kukusanya, kusindika na kusambaza bidhaa sokoni - kwamfano barabara za vijijini, vituo vya kupozeshea maziwa, mtandao wa umeme - ni finyu, hususan maeneo ya kaskazini na mashariki kunapopatikana maziwa. Mfumo hafifu wa ushirika: Pamoja na historia ndefu ya ushirika kwenye sekta ya maziwa, vyama/vikundi vingi vya wafugaji wimeshindwa kupanua uwigo wa usindikaji na soko la maziwa. Vimeshindwa pia kuwa na sauti moja ya kutetea maslahi yao na ya sekta. 10 Changamoto muhimu za sekta f ya maziwa Tanzania Mazingira duni ya uwekezaji na biashara: Mazingira ya uwekezaji na biashara katika sekta ya maziwa ni duni kutokana wingi wa mashirika yanayosimamia sekta kisheria. Yako 17 na baadhi yana she- ria na taratibu zinazofanana. Hii imeongezea gharama za kufanya biashara katakana na muda mwingi unaotumika kupata leseni na vibali, pamoja na malipo ya leseni hizo. Matokeo yake ni kwamba zaidi ya nusu ya viwanda binafsi vya kusindika maziwa vilivyofunguliwa miaka ya 1990 vimefungwa. Bei kubwa ya bidhaa zilizosindikwa: Ushuru juu ya mashine na vifungashio vinavyoagizwa kutoka nje pamoja na kodi ya ongezeko la tha- mani (VAT) ya bidhaa za maziwa vinasababisha bei ya maziwa na bidhaa kwenye soko rasmi kuwa kubwa kuliko ya bidhaa za soko lisilo rasmi ambazo hazitozwi kodi. Ushindani huu usio sawa unafanya wawekezaji kukwepa sekta ya maziwa. Pengo kati ya uzalishaji na mahitaji ya maziwa kuongezeka: Pengo kati ya uzalishaji na mahitaji ya maziwa linaongezeka. Aidha kutokana na uzalishaji usio sawa kati ya misimu, kiasi kikubwa cha maziwa (hususan ya masika) hakimfikii mlaji. Pamoja na kwamba kuna maeneo ambayo walaji hawana desturi ya kunywa maziwa, kuna dalili kwamba mabadiliko ya ulaji pamoja na ongezeko la idadi ya watu pamoja na kipato vinaongeza mahitaji ya maziwa. Kwa vile idadi ya ng'ombe wa kisasa kwenye nyanda za juu haiongezeki kwa kasi, ongezeko la uzalishaji wa maziwa litatokana na kuboresha idadi kubwa ya ng'ombe wa kienyeji walioko kanda ya kati ya nchi. Hata hivyo miundombinu katika ukanda huu ni finyu na kwa vile maziwa huzalishwa wakati wa masika, kiasi kikubwa (asilimia 20 hadi 50) huharibika kutokana na kukosa soko. Wakati wa kiangazi kiwango cha uzalishaji hushuka na kushindwa kukidhi mahitaji ya soko. Hata hivyo, kwa kutumia teknolojia ya UHT au kutengeneza maziwa ya unga pamoja na kuboresha lishe ya ng'ombe wakati wa kiangazi (kwamfano kulisha jiwe la molasi-urea-madini) tatizo hili linaweza kupunguzwa. Ufinyu wa miundombinu: Miundombinu ya kunakopatikana maziwa (barabara, umeme, maji) bado ni hafifu, hasa kwenye eneo la kati la nchi lenye mifugo mingi. Hii, pamoja na gharama kubwa za umeme na maji vinapunguza kasi ya uwekezaji kwenye sekta ya maziwa. 11 Tanzania Vyama hafifu vya wafugaji: Katika miaka ya nyuma, vyama vya ushirika na vikundi vya wafugaji havikupata msukumo na usi- mamizi wa kutosha na vingi vilidhoofika au kufa kabisa. Kutokana na historia hii, wafugaji wengi bado hawana imani na vikundi au ushirika. Lakini vikundi au ushirika ndio njia pekee ya kuwapatia huduma za pamoja kama ushauri, pembejeo, soko la maziwa na tiba ya mifugo yao. Mafunzo kutoka India Jedwali 1, hapa chini, linaonyesha jinsi teknolojia na mbinu za uzalishaji kutoka India zinavyoweza kutatua mapungufu yanayokwamisha maendeleo ya sekta ya maziwa nchini Tanzania. Mapungufu Tanzania Teknolojia/Mbinu kutoka India 1. Uhaba wa takwimu kuhusu uzalishaji, ukusanyaji Teknolojia ya habari na mawasiliano iliyobuniwa na na usindikaji wa maziwa katika sekta rasmi ya NDDB na kutumika katika sekta rasmi ya mtiririko maziwa. wa thamani India. Ikitumika hapa nchini itaboresha mipango na uendeshaji wa sekta ya maziwa kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Maziwa ya Tanzania, Chama cha Wasindikaji Maziwa Tanzania na Chama cha Wazalishaji Maziwa Tanzania. 2. Kiwango duni cha ubora wa maziwa kwenye Mfugaji: Makeni ya maziwa ya lita 15; ndoo za ngazi ya mfugaji, mlanguzi na vituo vya kukamulia za lita 10; faneli, vichujio na vikombe vya kukusanya maziwa. kuchunguza maziwa. Mlanguzi: Makeni ya maziwa ya lita 20 - 40. Msindikaji: Tenka za kusafirisha maziwa. 3. Matumizi finyu ya raslimali ya masalio ya mazao Teknolojia ya matofali ya Molasi-Urea-Madini inayo- kwa ajili ya kulishia mifugo hususan wakati wa faa wafugaji. kiangazi. 4. Uhaba wa vifaa wanavyotumia wahamilishaji pamoja Vifaa vya wahamilishaji. na mbegu bora za ng'ombe wa maziwa. Matangi ya kuhifadhia mbegu (lita 5-20) Vifaa vya kupima ubora wa mbegu. Mbegu bora 12 1 f Tunayoweza kujifunza kutoka India Serikali kutoingilia uanzishwaji na uongozi wa vyama vya ushirika ni kigezo muhimu cha mafanikio ya ushirika. Kuingiliwa kwa ushirika na wanasiasa kwa maslahi ya kisiasa au "kutekwa nyara" kwa ushirika na serikali kwa kuwateua watumishi wa serikali kuwa wajumbe kwenye bodi za ushirika kunadhoofisha au kuua ushirika. Amul ni mfano unaoongoza kwa ubora wa ushirika wenye umiliki na udhibiti imara wa wanachama. Bodi na menejimenti zinawajibika kwa wafugaji (wamiliki) na sio kwingineko. Serikali ya India imepitisha sheria mpya ya makampuni inayoruhusu kuundwa kwa kampuni zinazomilikiwa na wazalishaji (wakulima/wafugaji). Sera, sheria na kanuni zilenge kupunguza gharama ya kufanya biashara na pia kutoa motisha kwa wawekezaji wazalendo. Mfano wa kuigwa ni ondoleo la kodi "zero taxation" kwenye pembejeo za usindikaji wa maziwa. Hii inawezesha bidhaa za maziwa kumfikia mlaji kwa bei zenye unafuu wa ushindani wa soko. Aidha, kanuni na taratibu za kupata leseni na vibali zimerahisishwa. Hali hii ni tofauti sana na ile ya sekta ya maziwa Tanzania ambako shughuli zote za mtiririko wa thamani zinakwamishwa na utitiri wa kanuni zisizo za lazima na zinazoongeza gharama ya kufanya biashara. Ufanisi kwenye kuratibu shughuli za uzalishaji wa maziwa umeongeza ushindani. Kuna ushirikiano mkubwa baina ya wafugaji, madaktari wa mifugo, vituo vya maziwa, wasindikaji, n.k. Ushirikiano huu unawezesha kila hatua kwenye mtiririko wa thamani kupata faida itokanayo na ongezeko halisi la thamani. Aidha ushirikiano huu, umeimarisha mawasiliano ya habari kwenye ngazi zote na imewawezesha watoahuduma kutoa huduma zinazotakiwa na kwa wakati unaostahili. Kwa mfano, mshindonyuma kwa wafugaji kuhusu idadi ya vimelea kwenye maziwa, huwafikia masaa sita tu baada ya kufikisha maziwa kituoni. Hii inawawezesha madaktari wa mifugo kushughulikia mara moja matatizo ya uzalishaji shambani kwa wafugaji Huduma zote ni sehemu ya mtiririko wa thamani, hulipiwa kikamilifu na hazitegemei serikali. Wanachama wote wanapata huduma ya tiba ya mifugo, uhamilishaji, vyakula bora vya mifugo, n.k., zote zikilenga 13 Tanzania f kuiboresha mifugo. Aidha, swala la kulipia huduma linatokana na imani kwamba wafugaji wanathamini na kutunza vizuri zaidi vitu walivyolipia. Kwa vile washiriki wote katika mtiririko wa thamani wana lengo moja - unafuu wa bei kwa mlaji - na wameungana kupitia mfumo wa ushirika unaomilikiwa na wafugaji, malipo yote yanatokana na gharama halisi za huduma na hakuna kulanguliwa. Kulimudu soko kikamilifu kutokanako na utafiti wa kudumu wa soko ni muhimu katika kuhakikisha kwamba mahitaji ya maziwa ni zaidi ya uzalishaji. Amul imefaulu kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye soko la mlaji. Ushindi huu umepelekea bidhaa zake kupendwa zaidi kuliko za makampuni makubwa ya nje na hatimaye kuhakikisha kwamba maziwa ya mfugaji wa India yanaendelea kupata soko. Mafanikio kwenye soko, yanayotegemea ubora na unafuu wa bei za bidhaa, ndio msingi wa mkataba wa muda mrefu kati ya wafugaji na wasindikaji. Makubaliano ya muda mrefu juu ya bei yanawaondolea wafugaji athari za kuyumba kwa bei na wasindikaji athari za kukosa maziwa. Kwa hiyo mipango ya uwekezaji na upanuzi kwenye maeneo hayo mawili inakuwa ya uhakika zaidi. Kuyumba na kushuka kwa kiwango cha uzalishaji wa maziwa mwezi hadi mwezi, kutegemeana na msimu, kunaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa kulisha ng'ombe wanaokamuliwa, tofali za molasi-urea-madini (MUM). Nchini India, teknolojia hii ya kulisha ng'ombe wa maziwa, ilienezwa kwa wafugaji na bodi ya maziwa, NDDB, miaka ya 1980. Matokeo yake ni kwamba maziwa, kukua kimwili na uzaaji vyote viliongezeka kwa kiasi kikubwa. Uwiano kati ya gharama na mapato, kwa maziwa peke yake, ulikuwa kuanzia 1:2 hadi 1:4. Kadiri hali ya hewa inavyozidi kubadilika na mvua kupungua hapa Afrika Mashariki, umuhimu wa teknolojia hii kwa wafugaji utazidi kuongezeka. Pamoja na kwamba uzalishaji na matumizi ya matofali ya MUM umeshaanza kwa kiwango kidogo nchini Tanzania, ujuzi na uzoefu wa India unahitajika ili teknolojia hii iwafikie wafugaji wote. Uwazi na ukweli. Uwazi na ukweli ni msingi wa mafanikio katika ushirika na tija katika kampuni za wafugaji. Lengo linaloeleweka la "maziwa mengi na yanayouzwa na wafugaji kwa bei kubwa" kunapelekea kwa watumishi wakereketwa katika ngazi zote. 14 1 Mfano wa kioski cha maziwa jijini Dar es Salaam Kioski cha maziwa cha "Bahati" ni duka dogo la maziwa kwenye mtaa wa watu wengi jijini Dar es Salaam. Ni cha mama wa watoto wawili wadogo. Alianzisha biashara ya maziwa miaka miwili iliyopita kujiongezea kipato. Kila siku hununua lita 20 za maziwa kutoka kwa mlanguzi ambaye naye anayanunua kutoka kwa wafugaji walio nje kidogo ya jiji (kilometa 10 hadi 40 hivi) na kuyasafirisha kwa baiskeli au mabasi. Mtaji wa kuanzia biashara aliupata kutoka kwenye vikundi vya akina mama vya kukopeshana, akanunua jiko la mkaa, sufuria, chupa za chai, vikombe vya plastiki, meza ndogo na fomu mbili za kukalia wateja (vyote kwa gharama ya shilingi 48,000 hivi). Ndani ya mwaka mmoja duka lake likawa mahali wateja, hususan vijana, wanapenda sana kuja kunywa maziwa ya moto, chai au kahawa na mauzo yakaongezeka. Sasa akawa ananunua lita 70 kwa siku kutoka kwa walanguzi kadhaa. Ghafla, siku moja akapewa notisi kutoka wilayani ya kumtaka akate leseni ya biashara la sivyo afungiwe duka lake la maziwa. Utaratibu wa kupata leseni na kibali cha bwana afya cha kuuza maziwa kikawa kirefu na cha gharama kutokana na urasimu mwingi. Ulichukua yafuatayo: 1. Ukaguzi wa bwana afya (siku 3 za kufuatilia na gharama ya teksi shilingi 20,000). 2. Kuweka marumaru, beseni la kunawa mikono, maji moto (mwezi mmoja wa usimamizi na shilingi 400,000 za vifaa na ufundi). 3. Tangi dogo la kuchemshia maziwa (shilingi 300,000). 4. Kabati la vyombo lenye mlango wa kioo (shilingi 35,000). 5. Jokofu (shilingi 600,000). 6. Meza mbili na viti nane vya plastiki (shilingi 100,000). 7. Gharama za kufanyiwa mchanganuo wa faida na hasara wa cuplike (shilingi 50,000). 8. Kupata namba ya mlipa kodi na kodi ya awali ya makisio (shilingi 300,000) 9. Leseni ya serikali za mitaa (shilingi 30,000). 15 Tangi la kuchemshia maziwa pamoja na jokofu lilikuwa mkopo kutoka shirika la kuweka na kukopa la akina mama, na mkopo wenyewe ulikuwa na riba ya asilimia 30 kwa mwaka. Dhamana ulikuwa asilimia 15 ya mkopo, fedha taslimu, pamoja na vifaa vyenyewe. Malipo ya mkopo ilikuwa ni kwa mwezi. Ilichukua karibu miezi sita kupata vibali vyote pamoja na kukamilisha marekebisho ya duka. Katika kipindi hiki, biashara likuta inaendeshwa bila kibali na hivyo kinyume na sheria. Ili kuwatuliza wakaguzi, ilibidi kutoa rushwa ya shilingi 180,000. Hata hivyo, alipofungua duka hilo "jipya", mauzo yaliongezeka hadi lita 200 kwa siku baada ya mwaka hivi. Kufikia hapo, mwenye duka alianza kusindika kiasi kidogo cha maziwa (freshi na mtindi) na kuyafunga kwenye pakiti. Pia ilibidi kuajiri wasaidizi sita (baadhi yao kwa mkataba wa nusu siku). Pamoja na kwamba mtaji ulikuwa kiwi, lakini mauzo na faida iliongezeka. Kutokana na mradi kuwa mdogo, aliweza kutumia vifaa na eneo la biashara kwa tija, akaweza kupata faida mwaka wa 2007. 16 Tanzania Kituo cha kukusanya maziwa Kwenye ukanda wa kati wa Tanzania, kituo cha kawaida kina tangi la kupozeshea maziwa la ujazo wa lita 1,000. Hii ina maana kwamba msimu wa maziwa mengi (masika) litapokea lita 1,300 kwa siku, na lita 700 tu wakati wa kiangazi. Maziwa yaliyozidi ujazo wa tangi, inabidi yashughulikiwe kwa kuongeza tripu za tenka la kusafirishia maziwa. Tangi la kupozeshea maziwa kutoka India linagharimu takriban shilingi milioni 12 hadi kulifikisha Dar es Salaam. Mahali ambapo hakuna umeme wa gridi, tangi la maziwa linaweza kuendeshwa na mtambo wa umeme wa kilowati 10, unaogharimu shilingi milioni 50. Vifaa vingine vinavyohitajika kituoni ni vile vya kupima ubora wa maziwa. Ukichukulia kwamba nyumba ya kituo ni ya kupanga (na sio ya kujenga wenyewe), kituo kimoja kinagharimu shilingi milioni 65 kukikamilisha. Kimsingi, kituo cha kupozesha maziwa kazi yake kubwa ni kuhifadhi maziwa yasiharibike yakisubiri kusafirishwa hadi kiwandani kusindikwa. Hakiwezi kufanya biashara kubwa ya maziwa baridi kwa sababu bei itakuwa kubwa kuliko ile ya Matumizi kwa mwaka mfugaji au mlanguzi. Mkopo (malipo ya miaka 5 kwa riba ya 20%): 21,735,000 Tsh Ndio sababu vituo vilivyo Pango: 650,000 Tsh jirani na miji mikubwa Uchakavu: 6,500,000 Tsh vinakosa maziwa wakati Maji: 60,000 Tsh wa kiangazi kwa vile Mishahara: 2,288,000 Tsh mengi yanauzwa na Sabuni n.k.: 120,000 Tsh wafugaji/walanguzi moja kwa moja kwa Jumla ya matumizi: 31,353,000 Tsh mlaji. Mfano huu ni wa kituo kinachomilikiwa na mwenye kiwanda cha kusindika maziwa. Pamoja na kwamba kituo kinatumia umeme wa gridi, inabidi genereta litumike kutokana na umeme kukatika mara kwa mara. Hii inaongeza gharama ya umeme ambayo tayari iko juu. Kwa hiyo mwenye kituo amedhamiria kununua mtambo wa kuzalisha umeme kutokana na upepo. Mchanganuo ufuatao umechukulia kupatikana kwa umeme huo. Jumla ya maziwa yaliyokusanywa kwa mwaka ni lita 345,500. Kwa hiyo thamani iliyo ongezwa kwa lita moja ni shilingi 90. 17 Mlanguzi wa maziwa Walanguzi hununua maziwa na kuyauza kituoni, kiwandani, kioski au kwa mlaji. Wakati wa maziwa mengi (masika), walanguzi huuza maziwa mengi zaidi kituoni au kiwandani, lakini yanapo adimika (kiangazi) mengi huuzwa kwa walaji kwa bei ya juu zaidi. Walanguzi wa ukanda wa kati hutumia baiskeli kusafirisha maziwa hadi umbali wa kilomita 20. Kiangazi, ng'ombe huhamishiwa mbali kwenye malisho, kwa hiyo walanguzi wameanza kutumia pikipiki ambazo pia zinabebaba maziwa mengi zaidi. Haya yote yanagusa faida anayo pata mlanguzi. Maziwa husafirishwa ndani ya ndoo za plastiki za lita 20 ambazo haziosheki vizuri, jambo ambalo huchangia kushusha ubora wa maziwa. Makeni ya chuma ndio yaliyopendekezwa lakini ni ya gharama zaidi na huenda yasibebeke vizuri kwenye baiskeli. India ni mtengenezaji mkubwa (na wa bei nafuu) wa makeni duniani. Keni moja la lita 20 linauzwa shilingi 50,000, bei ya rejareja. Baiskeli moja ina uwezo wa kubeba makeni matatu (lita 60). Kwa hiyo mtaji wote pamoja na baiskeli ni shilingi 300,000 hivi. Hii ni sawa na mapato ya shilingi 50,000 kwa Annual Income mwezi, ambayo ni chini Milk sales; 13,500 liters ya mshahara wa kima (9,000 x 280 + 4,500 x 350 ) 4,095,000 Tsh cha chini. Hiki sio kipato kidogo ikizingatiwa Annual Expenditure kwamba hii ni kazi ya Milk purchases (9,000 x 230 + 4,500 x 300) 3,420,000 Tsh nusu siku hivi na kwamba Losses (1%) 34,200 Tsh ajira ya mshahara vijijini Bicycle repairs 50,000 Tsh ni adimu. Total Expenditure 3,504,200 Tsh Annual Gross Margin: 590,800 Tsh 18 1 f Photography: Claudia Fichtner, Great Lakes Film Production, DDA Design: