88940 v1 JAMHURI YA KENYA Mkakati wa Ushirikiano FY2014-2018 M U K H TA S A R I Mkakati wa Ushirikiano wa Jamhuri ya Kenya FY2014-2018 Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi M U K H TA S A R I Juni 2014 F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya Utangulizi Safari ya Kenya ya maendeleo kwa wote K enya ina nafasi ya kuwa mojawapo ya mataifa yaliyostawi barani Afrika. Hii ni kwa sababu taifa hili linajivunia sekta ya kibinafsi iliyoimarika, idadi kubwa ya vijana na kuandaa uchaguzi mkuu uliopita kwa amani; maswala yanayoipatia fursa nzuri ya kupata maendeleo kwa jamii zote katika miaka ijayo. Hata hivyo, viwango vya umaskini vingali juu huku watu wanne kati ya kumi wakiwa maskini licha ya kwamba asilimia 10 ya matajiri nchini wanamiliki asilimia 40 ya jumla ya pato la taifa. Je, ni nini kinaweza kufanywa kumaliza umaskini na kupata maendeleo kwa kila mmoja ifikiapo mwaka 2030? Na je mashirika ya Benki ya Dunia (WBG) yanayojumuisha IFC, MIGA na Chama cha maendeleo ya Kimataifa IDA yanaweza kusaidia vipi katika azma ya Kenya kujiendeleza katika miaka ijayo? Maswali haya ndiyo msingi wa Mkakati wa kitaifa wa Maendeleo kwa ushirikiano na WBG, (CPS). Mkakati huu umetayarishwa kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya Kenya, serikali za county, sekta ya kibinafsi, mashirika ya umma, na mashirika ya kimataifa yanayohusika na maendeleo. Ripoti hii inaangazia haja ya mipangilio ya kudumu itakayopelekea kustawisha uchumi kwa haraka na kutilia maanani sekta zinazowaathiri watu wanaoishi katika umaskini. Sekta ya umma inaweza kuongoza katika kubuni nafasi mpya za ajira huku serikali ikiboresha mazingira ya kufanyia biashara ili mashirika yaweze kuimarisha biashara zao. Hata hivyo, ustawi bora ni lazima ujumuishe maswala yote muhimu ili kila mmoja afurahie maisha bora. Wakenya wengi wanapitia hali ngumu ya maisha kutokana na kwamba walizaliwa katika maeneo fulani au hali za familia zao na wala sio kwa sababu ya juhudi zao au talanta zao; jambo ambalo haliwezi kukubalika.Ustawi wa jumla utaboresha huduma Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi i za afya, kuhakikisha kwamba vijana wanaweza kufanya kazi, kuimarisha kilimo haswa katika jamii zenye mapato ya chini, kulinda jamii maskini dhidi ya majanga na athari za mabadiliko ya anga na kuboresha hali ya maisha katika miji mikuu. Ustawi bora pia ni lazima uweze kuwajibikiwa. Katiba mpya ya mwaka 2010 ni hatua kubwa kwani inaweka masharti ya usawa wa kijinsia na inatoa nguvu zaidi kwa mashirika ya kupambana na ufisadi. Vile vile inatoa mwongozo wa ugatuzi kwa kiwango kikubwa ambacho hakijaonekana kwingineko. Hizi zote ni changamoto kubwa. Azimio letu ni kutoa dola bilioni 4 au zaidi kwa miradi na rasilmali mpya katika miaka ijayo, ili kusaidia taifa hili kuafikia agenda yake ya maendeleo thabiti yanayojumuisha kila sekta na kufikia kila mwananchi na ambayo yanaweza kuwajibikiwa. Benki ya Dunia inajivunia uhusiano mwema kati yake na Kenya na inatazamia ushirikiano mzuri wa washirika wa kitaifa na kimataifa katika sekta za umma na kibinafsi. Kwa ushirikiano, Kenya ina fursa ya kuafikia uwezo wake wa kuinua maisha ya mamilioni ya familia kutoka kwa umaskini na kustawisha uchumi wake kufikia viwango vya kisasa. Diariétou Gaye Cheikh, Oumar Seydi Mkurugenzi anayesimamia Kenya, Mkurugenzi wa IFC, Benki ya dunia, bara la Africa Mashariki na kusini mwa Africa ii F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya MUKHTASARI 1 Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliyo na nafasi bora zaidi ya kustawi barani Afrika. Kenya inajivunia idadi kubwa ya vijana, sekta ya kibinafsi inayoimarika, na msingi wa mabadiliko kutokana na katiba mpya. Aidha inajivunia kuandaa uchaguzi mkuu uliopita kwa amani na inaongoza kiuchumi na kimaendeleo katika Afrika Mashariki. Hata hivyo viwango vya umaskini nchini viko juu huku takwimu zikionyesha kwamba angalau watu wanne kati ya kumi ni maskini hohe hahe huku asilimia 10 ya matarjiri wakimiliki asilimia 40 ya pato la kitaifa. Malalamishi kuhusu uongozi yamekithiri na japo uchumi umeripotiwa kukua, unatatizwa na viwango vya chini vya uwekezaji na mapato duni kutoka kwa viwanda na mashirika. Ukuaji kiuchumi bado haujafikia viwango vinavyohitajika kubadilisha maisha ya mwananchi. Matarajio ya kujiendeleza: Uchunguzi wa kina wa hali ya taifa na agenda ya maendeleo 2 Mpangilio huu unatokana na uchunguzi wa kina wa ushahidi kutambua changamoto na nafasi za Kenya katika kuafikia malengo mawili muhimu. Kulingana na takwimu, viwango vya Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi iii umaskini vilishuka kutoka asilimia 47 mwaka 2005 hadi asilimia 39 mwaka 2012. Viashiria muhimu vya maisha vimeimarika japo bado hakuna usawa kati ya watu wa tabaka tofauti. Nafasi za kujiendeleza kwa wanawake ni duni ikilinganishwa na wanaume haswa wale wanaoishi maeneo ya mashambani yasiyo na maendeleo huku pia swala la ukabila likiathiri maendeleo ya jamii. Kwa mtazamo, kumaliza umaskini hohe hahe ifikiapo mwaka 2030 kutamaanisha kupunguza viwango vya umaskini kwa silimia 2 kila mwaka. Hili litawezekana tu ikiwa uchumi wa taifa unatua mara mbili ya ilivyo sasa na pia ikiwa tofauti ya mapato kati ya matajiri na maskini itapungua kwa asilimia 50. Ili kuanzisha maendeleo ya kudumu, ni sharti Kenya kuangazia changamoto za uwekezaji duni na uzalishaji wa viwango vya chini katika viwanda. Ukuaji wa haraka unahitaji mabadilikoo katika sera za matumizi ya pesa za umma kuimarisha miundo msingi. Aidha mazingira ya kufanya biashara yanastahili kuboreshwa ili kuimarisha sekta ya kibinafsi na kuthibiti ushuru unaotozwa wafanyibiashara. Maono: Kipaumbele cha serikali na mikakati ya kipindi cha 2013-2017 (Medium Term Plan) 3 Kenya inalenga kuwa taifa linalotambulika kote ulimwenguni kwa ukuaji wa kiuchumi na hali nzuri ya maisha kwa wananchi wake. Mpango wa “Vision 2030”, umeundwa kwa misingi ya uchumi, jamii na siasa na unajumuisha maazimio ya serikali iliyopita na iliyoko mamlakani sasa. Msingi wa kiuchumi unaazimia kuimarisha sekta muhimu zikiwemo kilimo na huduma za fedha kupelekea ukuaji wa uchumi kwa silimia 10 kila mwaka. Msingi wa kijamii unalenga kuimarisha hali ya maisha ya wananchi kupitia kwa elimu, huduma za afya na makaazi bora haswa kwa wanawake, vijana na jamii zilizotengwa. Nao msingi wa kisiasa unaangazia hali ya baadaye ya taifa hili kwa kuboresha utekelezaji wa sheria, na kutilia mkazo iv F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya uwazi katika uongozi. Hii inaungwa mkono na mpango wa kipindi cha mwaka 2013-2017 (second Medium-Term Plan (MTP2, 2013- 17), ambao agenda yake inalingana na lengo la Benki ya dunia la kuangamiza umaskini kote duniani. Hali hii pamoja na mchango wa washika dau unaofuatia mazungumzo ya kina inatoa mwanzo mzuri kwa mkakati wa ushirikiano huu. (CPS) Changamoto na nafasi za maendeleo 4 Changamoto kuu na ya msingi ni kuafikia ukuaji ulioimarika na kwa haraka angalau katika muongo mmoja. Nafasi iliyopo ni kutumia rasilmali za umma na za kibinafsi kupitia ushirikianao mathubuti wa sekta za umma na kibinafsi ambao kwa sasa haujakuzwa ipasavyo. Juhudi mpya zinastahili kutiliwa maanani kuthibiti mishahara ya wafanyikazi wa umma ili kuimarisha mfumo wa kifedha kwa ujumla. Pia, kuna haja ya mipangilio mahsusi kuimarisha mazingira ya kufanya biashara sawa na kushughulikia maswala yaliyoangaziwa na ukaguzi uliofanywa na Benki ya Dunia. Mabadiliko haya yatawezekana tu kukiwepo na takwimu halali na zinazotolewa kwa muda unaofaa kusaidia katika uundaji wa sera na ukaguzi wa miradi. 5 Kuna haja kubwa ya kutilia mkazo kuimarishwa kwa hali ya maisha ya wananchi. Ukuaji unafaa kujumuisha watu wote ili kila mmoja ashuhudie, na kufurahia maendeleo. Inasikitisha kwamba, Kenya ni miongoni mwa mataifa ya bara Afrika ambapo vifo vingi zaidi vya watoto wachanga huripotiwa. Kwa kila watoto laki moja wanaozaliwa, 488 huaga dunia. Aidha wananchi wengi hawana chakula cha kutosha, wanakosa maji safi, hawawezi kufikia huduma za afya na hawana makao mazuri. Asilimia 21 ya vijana hawana ajira,mara mbili zaidi ya watu wazima. Kuna umuhimu kuwapa vijana elimu ya kisasa na nafasi za kazi ili kutambua na kukuza talanta zao. Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi v Miji mikuu isiwe tu ya kutengeneza nafasi za ajira bali pia inafaa kutoa huduma muhimu za kimsingi kwa wakaazi wake. Kwa kuwa Kenya ni taifa la watu wa tabaka mbali mbali, ni bora kufanya juhudi kushirikisha kikamilifu watu waliotengwa na wasiojiweza katika jamii katika mipango yote ya maendeleo ya taifa. Ili kuamliza umaskini, ni sharti maendeleo yaanzie mashinani ambako kuna idadi kubwa ya watu maskini wanaolengwa katika miradi ya kuangamiza umaskini. Uwekejazi unafaa kuelekezwa mashinani ili kuboresha kilimo na kuweka mikakati ya kuwazuia wananchi kutumbukia katika umaskini. Aidha mikakati hii inafaa kuvutia wawekezaji wa kibinafsi, kuinua viwango vya elimu na kuboresha huduma za afya mashinani. 6 Mabadiliko katika taasisi za uongozi na usimamizi wa rasilmali yamepelekea ugatuzi ambapo baadhi ya shughuli za serikali sawa na asilimia 30 ya pato la taifa zipelekwa katika uongozi wa serikali za kaunti 47. Mabadiliko haya bila shaka ni ya kihistoria haswa ikizingatiwa kwamba ni mataifa machahe tu ambayo yamejaribu kufuata mfumo huu wa uongozi. Changamoto iliyoko mbele ni kutimiza malengo ya ugatuzi kwa kushirikisha wananchi, kuboresha huduma za serikali, na kuweka miundo msingi bora ya serikali mashinani. Miundo misingi hii itaimarisha uhusiano kati ya serikali kuu na serikali za county na kuwezesha rasilmali kutumika kikamilifu kuunda sera zitakazotumika kuleta mabadiliko ya kudumu mashinani. 7 Nafasi hizi zote zinaweza kutumika kikamilifu ikiwa kutawekwa mikakati ya kuboresha uongozi na kupunguza ufisadi. Ili kuafikia maazimio haya muhimu, benki ya dunia itasisitiza umuhimu wa kumaliza ufisadi na kutii sheria kwa wananchi wa tabaka zote huku ikiweka matarajio yanayoweza kuafikia maendeleo hatua kwa hatua. Kuna nafasi ya kuboresha usimamizi wa fedha za umma, kuimarisha vi F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya uongozi, kuhimiza uwazi katika shughuli za serikali na kudumisha mipango itakayolinda mikakati hii. Mpangilio huu wa kuimarisha taasisi utasaidia kulinda hadhi ya rasilmali za Benki ya dunia na pia rasilmali za Kenya ambazo huchangia asilimia 90 ya matumizi ya pesa za umma. Mikakati muhimu ya utumizi bora wa rasilmali za WBG 8 Ushirikiano huu unalenga Kusaidia Kenya kukabiliana na changamoto hizi. Aidha ushirikiano huu unatokana na uhusiano bora wa miaka mingi na unatoa mpangilio wa jinsi rasilmali za Benki ya Dunia IFC na MIGA zitatumika kikamilifu kusaidia taifa hili kuafikia lengo lake la kustawi na kueneza maendeleo kwa wananchi wake wote. Benki ya dunia itatumia jaribio maalum kuchagua jinsi ya kugawa rasilmali ili kuongezea uwezekano wa kupata matokeo bora zaidi. Mpangilio wa jaribio hili utakuwa katika viwango vinne; a) kufuatilia na kuthibitisha maono ambayo yatapelekea mabadiliko ya kudumu kukabiliana na umaskini na kuanzisha maendeleo. (b) Kukagua kikamilifu uwezo wa Benki ya Dunia na kuzingatia nafasi yake bora katika kuleta mabadiliko muhimu kupitia kwa ushirikiano (c) Kusisitiza umuhimu wa mwananchi kumiliki miradi na d) kuchunguza na kutilia maanani uwezo wa mteja (Mwananchi) kulingana na mpangilio wa miradi yenyewe. Jaribio hili hutumika kwa muundo wa kuwiana kutambua majukumu matatu yanashirikishwa, kutambua maswala muhimu katika kila jukumu na kulinganisha uhusiano kati ya mipangilio, ushauri na ukaguzi. 9 Jukumu la kwanza la ushirikiano nikuimarisha ushindani na maendeleo. Uti wa mgongo wa maendeleo ya kudumu ni kuboresha miundo msingi, kuboresha mazingira ya kufanyia biashara na kukabiliana na shinikizo kutokana na mabadiliko ya kila Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi vii mara. Sera za benki ya dunia zitasaidia viongozi kutoa mpangilio maalum wa utenda kazi na uthibiti wa sekta ya kawi. Ufadhili wa IDA utaelekezwa kwa uwekezaji wa miradi ya umma nazo IFC na MIGA zitasaidia kuvutia rasilmali za sekta ya kibinafsi. Kwa mapana, Benki ya dunia itaongeza mara dufu mchango wake kwa ushirikiano wa sekta ya umma na kibinafsi haswa huduma za maji na uchukuzi zinazoonyesha matumaini ya kukua kwa kipindi kilichoko. Katika uchukuzi, IDA itaelekeza ufadhili wake kwa barabara za vijijini na zile zinazounganisha kaunti tofauti ili kurahisisha usafiri na kuwezesha wananci kufikia nafasi zaidi za uwekezaji. Aidha, ushindani utaimarishwa kwa kuboresha mazingira ya kufanyia biashara, kutoa nafasi zaidi za uwekezaji katika kila sekta kulingana na maeneo na kuendeleza huduma za fedha na soko la hisa. Benki ya Dunia pia itaunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha sekta mpya za mafuta na gesi. Ufadhili wa IFC na Benki ya Dunia utatumika kutengeneza nafasi za ajira katika sekta ya kibinafsi na kuboresha hali ya maisha katika miji mikuu ambako hali ya umaskini limekuwa donda ndugu. 10 Jukumu letu la pili katika ushirikiano huu ni kuwalinda waliotengwa na wanaokabiliwa na hatari katika jamii na kuwasaidia wafikie malengo yao, jambo ambalo ni muhimu katika maendeleo. Uhifadhi wa maadili na hadhi ya jamii pia utaangaziwa huku Benki ya Dunia ikiendelea kushikilia nafasi muhimu katika kuafikia haya. Afya pia ni muhimu sana; katika sekta hii, juhudi za pamoja za IDA NA IFC, pamoja na ufadhili wa kimataifa na washirika wengine, zitaimarishwa. Njia nyingine muhimu ya kuwasaidia wasiojiweza ni kulenga kilimo. Kutokana na kwamba kilimo husaidia moja kwa moja familia za mashambani ambako idadi kubwa ya wakenya wanaishi. Mipango ya IFC ya kuwekeza katika miundo msingi, kuongeza dhamana katika bidhaa za kilimo, pamoja na mashirika ya kifedha, viii F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya pia husadia lengo hili. Kuongezeka kwa idadi ya vijana kunachangia kuleta fursa na pia changa moto katika juhudi za WBG kusaidia katika elimu, kubuni ajira na kutoa mafunzo. Kuwasaidia wasiojiweza ambao pia wanaathirika kutokana na mabadiliko ya kila mara ya hali anga, pia kutakuwa katika mipango yetu ya usaidizi. Pamoja na kwamba shughuli za kijinsia za WBG zitaimarishwa, ikiwemo elimu ya wasichana, biashara, na kusaidia makundi ya wanawake wa mashambani. 11 Jukumu la tatu katika kazi hii, litakuwa kuangazia usawa na kuona kwamba mradi huu unakuwa thabiti na wa kutegemewa. Hili ni jukumu la muda mrefu ambalo litahusisha sana ugatuzi. Mpango wa benki ya dunia wa kuwapa watu wengi uwezo na mpango wa AAA, itachangia shughuli kadhaa za IDA kusaidia kaunti na mashirika ya kitaifa katika juhudi zake za kuona kwamba ugatuzi unafaulu. Ikiwa WBG itaulizwa isaidie, basi itaanzisha na kusimamia hazina ambayo itatumiwa na wafadhili kuweka pesa za msaada ambazo wanaolengwa watazifikia kwa urahisi. Mpango wa uwekezaji wa IDA utasaidia mbinu za kubuni sera ambazo zinategemea hali ilivyo, kutumia fedha za umma na mageuzi katika kusimamia fedha za umma. Ustawi wa maendeleo ya Kenya utategemea uthabiti wa ushirikiano wakanda hii na mataifa jirani; na mpango wa uwekezaji wa WBG utafanywa wa mataifa, ikiwemo sekta za kawi na uchukuzi. 12 Kibinafsi na kijumla, kufaulu kwa maendeleo ya kudumu kunaweza tu kupatikana ikiwa kuna ushirikiano kupitia mfumo utakaohakikisha utawala bora, swala ambalo limekuwa vigumu kuafikiwa hapo mbeleni. Mpango wa usaidizi wa WBG, pia hutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha taasisi simamizi, ikiwa ni pamoja na mafunzo kuhusu usimamizi bora wa fedha za umma na zaidi Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi ix uwazi katika taasisi na hasa uwazi kwa upande wa wanaotafuta huduma, na hivyo ni muhimu pia kutumia mikutano iliyo wazi ya kijamii kwa manufaa ya pande zote. Benki itaendelea kuchunguza manufaa ya mikakati inayowekwa kusimamia miradi ambayo tayari ipo, na kuimarisha zaidi mikakati iliyofaulu, ikiwa ni pamoja na kupata usaidizi kutoka kwa kitengo cha WBG cha INT kuhusu namna ya kulinda miradi na usaidizi kwa mashirika ya kutegemewa kama vile tume ya maadili na kupambana na ufisadi, EACC. WBG itatumia mbinu za kuchunguza ufisadi katika mradi wake wa kukopesha pesa kwa kubadilisha sehemu zinazolengwa na kupunguza pesa ikiwa kutazuka maswala ya kutiliwa shaka ambayo yanatishia mipango ya IDA na IFC katika matumizi yake ya fedha. Kutekeleza kwa ajili ya matokeo 13 Mkakati huu unahusisha kulenga matokeo katika ushirikiano huu, hasa shughuli maalum, na mkakati wenyewe unafaa kuwa tayari kuangazia hali mpya na habari kama vile kuhusu takwimu zinazoongezwa kuhusu umaskini. Matokeo yanayolengwa yamedhihirika katika mtindo wa sekta mbali mbali, kuashiria kutegemeana kwa huduma kote katika mkakati huo. Juhudi za pamoja na benki kusimamia matokeo katika mpango huo kote nchini, zinategemea mifumo ya taifa na uwezo wa kupima na kuchunguza hatua zinazopigwa. Ushirikiano katika benki na pia na washirika wengine utalenga maswala Fulani kama vile hali ya biashara, sekta ya fedha, ushirikiano wa sekta za umma na kibinafsi, kawi, na kilimo. Majaribio ya kuchagua tayari yanailazimu WBG kupanua baadhi ya shughuli zake—kama vile kusaidia miji midogo, kusaidia maendeleo mashambani, pamoja na ugatuzi—na kuhakikisha benki inashiriki katika mambo mengine kama vile barabara kuu, usimamizi wa mali asili, na mabadiliko ya kisheria. Utaratibu huu hubadilika, na uchunguzi pia utaendelea kubadikila. x F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya 14 WBG inaweza kuwa ikitoa zaidi ya dola billion 1 kila mwaka kwa Kenya kwa muda wote wa ushirikiano huu. Usimamizi bora wa mradi huu utaendelea kuwa muhimu katika kuhakikisha matokeo mazuri—pamoja na mbinu bora za kushughulikia hali mbali mbali za benki, mipango ya uwekezaji ya IFC, na MIGA. IFC inalenga kupanuliwa kwa mradi huu pengine hata kufikia dola million 785 kufikia kati ya mradi huu (FY14), ikiwa hali itaruhusu. Kwa sasa MIGA inatumia jumla ya dola million 255 hapa Kenya, na haja ya wawekezaji wa kimataifa kuwekeza katika sekta za miundo msingi, kawi, na kilimo biashara, inatoa fursa ya upanuzi zaidi wa mradi wa MIGA. Mipango ya kila mwaka ya benki hii itategemea mpango wa IDA 17 ambao hutumia dola million 600 kila mwaka. Hali hii itaimarisha mpango wa IDA nchini Kenya wa dola billion 4.3 kufikia kati ya mradi ( FY14), kufadhili miradi 23 ya kitaifa kwa gharama ya dola bilioni 3.5) na miradi 7 ya maeneo ambayo Kenya ni mwanachana (kwa gharama ya dola 0.8B). Ni muhimu kuendelea kupiga hatua hasa katika uwekezaji wa IDA, na pia katika juhudi za IFC, kwa kuangazia miradi mikubwa na matumizi mazuri ya fedha za ziada. Kudhibiti uwezekano wa hatari 15 Hali yoyote ya ukosefu wa uthabiti katika mradi wowote ambao sio wa fedha nyingi, inaweza kuwa hatari sana kwa juhudi za kupigana na umaskini. Mkakati wa kusaidia, bila shaka unahusisha mipango ya muda mrefu ya kuimarisha ushindani na mauzo ya nje, pamoja na mikakati ya kuweka akiba, na kuweza kufikia fedha za kimataifa ili kuweka kukabiliana na hatari hiyo. Majanga na hatari nyingine yoyote; inayotokana na mabadiliko ya ulimwengu na kusababishwa na binadamu, vinaweza kutokea japo wakati wake ama ukubwa wake haviwezi kujulikan; benki na washirika wakewatatafuta mbinu za kusaidia kukabiliana na hatari hiyo katika siku za baadaye. Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja na Ustawi xi Hatari nyingine inaweza kuhusisha mabadiliko ya ghafla ya kisiasa, mwelekeo wa kisera na mwelekeo wa wizara katika sekta muhimu, mabadiliko ya haja ya kufadhili kwa upande wa wafadhili ama kukosa kuona maana ya mpango unaofadhiliwa kwa upande wa wafadhili wa IFC na MIGA. Haya yote, yatahitaji kujipanga tena ili kuzuia mabadiliko hayo kuathiri mipango inayofadhiliwa na WBG. Hatimaye, hatari zinazoambata na kuendesha mpango wenyewe ni pamoja na usimamizi mbaya na ufisadi, hata katika kaunti ambako utawala mpya unapanua shughuli zale. Hatua ambazo zinaweza kuokoa hali ni (a) kufanya mabadiliko ambayo yatahakikisha usimamizi bora wa ushirikiano huu na pia kushiriki ugatuzi, (b) ushirikiano mwema kati ya INT, benki na mamlaka husika ili kuwekwe mikakati ya kuzuia na madai yanapozuka, yanashughulikiwa haraka na hatua zinachukuliwa; na (c) mawasiliano mazuri na washirika dau, ikiwa ni pamoja na bodi. xii F Y 2 0 1 4 - 2 0 1 8 • M kakati w a U shirikia n o w a J amhuri ya K e n ya “Raha tupate na ustawi” ~ Wimbo wa Taifa Picha: Benki ya Dunia VIDOKEZO The World Bank Design/Layout: Robert Waiharo Delta Center Cover image: Original Images Menengai Road, Upperhill PO Box 30577-0100 Nairobi, Kenya JOIN THE CONVERSATION! Tel: +254 20 2936000 Fax: +254 20 2936382 www.facebook.com/worldbankkenya Website: www.worldbank.org/kenya www.twitter.com/worldbankkenya