JAMHURI YA KENYA WIZARA YA KILIMO, MIFUGO, UVUVI NA UNYUNYIZAJI (MoALFI) IDARA YA KITAIFA YA UVUVI, KILIMO CHA MAJINI NA UCHUMI WA BAHARINI (SDFA-BE) RASIMU YA MWISHO MFUMO WA MAKUNDI YALIYOTENGWA NA KUTELEKEZWA (VMGF) MRADI WA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI WA UVUVI WA BAHARINI KENYA (KEMFSED) WARSHA YA KUHALALISHA MOMBASA JUNI 19 - 20, 2019 Utangulizi 1. Mfumo huu wa Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMGF) umeandaliwa kwa ajili ya Maendeleo ya Uchumi wa Jamii katika Uvuvi wa Baharini nchini Kenya (KEMFSED) na utafadhiliwa na Benki ya Dunia. Umebuniwa kutokana na matokeo na mapendekezo ya utafiti wa Kuchunguza Jamii ambao ulifanywa kwa ajili ya mradi huu katika Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na kingo za maji katika Pwani ya Kenya. Kwa sababu mikakati ya mradi unaopendekeza itatekelezwa katika maeneo ambapo kuna Wenyeji (IP) ambao wanarejelewa kuwa Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMG)1 nchini Kenya, sera ya ulinzi ya Benki ya Dunia (WB) ya OP/BP 4.10 imerejelewa na mfumo wa VMGF umetayarishwa ili kuongoza utekelezaji wa mradi huu. 2. Mradi wa KEMFSED unalenga kuimarisha uchumi na maisha ya wapwani kutokana na uvuvi wa baharini na kilimo cha maji huku ikidumisha ubora wa mfumo husika wa ekolojia kupitia utaratibu unaoshirikisha jamii. Imebuniwa kutokana mafunzo tuliyopata kupitia utekelezaji wa Mradi wa Maendeleo ya Pwani ya Kenya (KCDP) ambao pia ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na mikakati mbalimbali iliyotekelezwa na jamii ambayo ililenga kuboresha maisha ya makundi ya VMG katika kaunti za pwani ya Kenya. Malengo ya Mfumo wa Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMGF) 3. Lengo la mfumo wa VMGF ni kuongoza muundo, mpangilio na utekelezaji wa mikakati ya KEMFSED ambayo huenda ikaathiri makundi ya VMG katika maeneo yaliyopendekezwa kwenye mradi. Mfumo wa VMGF unatokana na kifungu cha OP 4.10 cha Benki ya Dunia pamoja na kanuni na sheria husika za Serikali ya Kenya. Kifungu cha OP 4.10 hurejelewa wakati ambapo kuna uwezekano wa makundi ambayo yanatimiza vigezo vya kifungu cha Benki ya Dunia cha OP 4.10 “yanayoishi au yana uhusiano wa pamoja na eneo ambako mradi utafanyika.” Mfumo wa VMGF inajumuisha aina za shughuli na mikakati iliyopendekezwa; athari nzuri na mbaya kwenye makundi ya VMG; mbinu za kuhakikisha mashauriano yanayoeleweka, ya wazi na yanayopangwa mapema; mipango ya taasisi ya kukagua shughuli zinazoendelezwa katika mradi na kukagua na kubaini uwepo wa makundi yaVMG katika eneo la mradi; mbinu za kufuatilia na kuripoti, na kufahamisha makundi yaVMG kuhusu mbinu hizo. 4. Mfumo wa VMGF utatumiwa na Idara ya Kitaifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini, mashirika ya kutekeleza mradi wa KEMFSED na Benki ya Dunia ili kuhakikisha kuwa vifungu vya Sera ya Utendaji wa Benki ya Dunia (OP) 4.10 vinazingatiwa katika utekelezaji na usimamizi wa mradi huu. Hatua hii itahakikisha kuwa athari mbaya zinatambuliwa kikamilifu na kushughulikiwa, ilhali athari nzuri zinaendelezwa kwenye makundi ya VMG. Vipengee vya Mradi 1 VMG ni jamii ambazo zinalengwa na mradi wa KEMFSED na zinatimiza masharti na vigezo vya Benki ya Dunia kwa mujibu wa kifungu cha OP 4.10 na vigezo vya Serikali ya Kenya (GoK) vya “jamii zilizotengwa” na za “wachache” kwa mujibu wa Katiba ya Kenya. 5. Vipengee vya Mradi vimebuniwa ili kuafikiana na Mfumo mpana wa Uchumi wa Baharini nchini Kenya na mchakato unaoendelea wa ugatuzi. Vipengee vikuu na vidogo vilibainishwa na kupangwa ili kuboresha malengo, utaratibu, ujumuishaji na usawazishaji wa dhana za miundombinu pamoja na usaidizi wa kiufundi/programu, mafunzo na kukuza uwezo wafanyakazi. Mchoro 1: Nadharia ya Mabadiliko ya Mradi wa KEMFSED Kipengee cha 1 – Kuboresha Uongozi na Usimamizi wa Uvuvi wa Baharini. 6. Hatua hi italenga kuboresha usimamizi wa uvuvi wa baharini katika maeneo yanayokaribia kingo za maji nchini Kenya. a) Kipengee kidogo cha 1.1: Kuboresha uongozi wa uvuvi na uchumi wa baharini. Kipengee hiki kidogo kitalenga kuboresha uongozi na usimamizi wa uvuvi, kukagua sera za uvuvi na sheria husika na kuimarisha mbinu za ufuatiliaji na uchunguzi wa mradi. Kipengee hiki kidogo pia kitalenga utafiti unaotakikana ili kuimarisha usimamizi wa uvuvi baharini, ikiwa ni pamoja na kutengenezwa kwa Mfumo wa Ufuatiliaji na Habari za Uvuvi (FIMS) ambao ni thabiti na utarahisisha hatua ya kufikia habari ili kuboresha usimamizi wa shughuli za uvuvi. Katika maeneo yakayobainishwa, uvuvi maalum utalengwa kupitia mikakati mahususi kulingana na Mipango ya Kuboresha Uvuvi (FIP), ikiwa na nia ya kubadilisha uvuvi huu ili uweze kusimamiwa vizuri kwa nia ya kuhakikisha manufaa ya kudumu katika jamii husika. Mradi huu pia utasaidia kuendeleza Hatua ya Mipango za Kitaifa za kukabili uvuvi wa papa, ndege na Uvuvi Haramu, Usioripotiwa na Usiodhibitiwa (IUU). b) Kipengee kidogo cha 1.2: Kuboresha usimamizi wa uvuvi unaokaribia ufuko. Kipengee hiki kitaimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi zinazofanyika karibu na ufuko na utekeleza wa Mipango ya Usimamizi wa Uvuvi (FMP). Kwa kushirikiana na FMP za kitaifa kwa ajili ya uvuvi maalum, maeneo mapya Yaliyounganishwa na Kusimamiwa kwa Pamoja (JCMA) yatabuniwa. Usimamizi wa maeneo yaliyopo utaimarishwa. Mradi huu pia utaendeleza utekelezaji wa Maeneo Yanayosimamiwa kwa Pamoja (CMA) ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mikakati ya Ufuatiliaji, Udhibiti na Uchunguzi (MCS) na utoaji wa vifaa vinavyotakikana na usaidizi wa kiufundi kwa ajili ya MCS. c) Kipengee kidogo cha 1.3: Uendelezaji wa miundombinu kwa ajili ya usimamizi wa uvuvi. Kipengee hiki kidogo kinajumuisha uendelezaji wa miundombinu ambayo inalenga kusaidia usimamizi wa uvuvi katika viwango vya kitaifa na kaunti. Hususan, inajumuisha jengo la ofisi ya Huduma za Uvuvi Kenya (KeFS) mjini Nairobi na Kituo cha Kitaifa cha Mafunzo na Rasilimali za Baharini katika Kaunti ya Kwale. Mifano ya miundombinu ya uvuvi inajumuisha kuboresha viwango vya ofisi za uvuvi za kaunti na kupanua chuo cha Mombasa Bandari Maritime Training College. Kipengee cha 2 – Kuwezesha Uwekezaji wa Kudumu katika sekta ya Uvuvi wa Baharini na Kilimo cha Majini 7. Hatua hii itabuni Huduma ya Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Wastani (SME/SME-DS), zinazotoa huduma za kitaalamu kwa wajasiriamali, SME na makundi ya serikali katika kaunti za pwani,. Pia itawezesha kuongezeka kwa faida inayotokana na uvuvi na kilimo cha baharini kwa kuwekeza katika miundombinu ya umma kama vile barabara, umeme na maji, inayohusiana na utaratibu wa kuboresha bidhaa na uwekezaji wa binafsi. a) Kipengee Kidogo cha 2.1: SME-DS Katika Jamii za Pwani. Tutahusisha SME-DS itakayojumuisha timu ya wataalamu wa SME wanaoshughulikia maendeleo, watakaopatikana katika jamii za wavuvi zinazoishi katika pwani ya Kenya. Wataalamu hawa wataendeleza huduma zao kwa Vitengo vya Usimamizi wa Fuo (BMU) na wenyeji wa pwani wanaotaka kuanzisha au kukuza biashara inayohusiana na uvuvi. Pia, watatoa usaidizi wa kiufundi unapotakikana, huduma za uchanganuzi, mafunzo kwa wafanyakazi na kutoa ushauri mbalimbali. SME-DS itabaini pia matatizo au hatari za kimfumo ambazo zinazuia kutelelezwa kwa miradi inayotarajiwa na itapendekeza hatua za kusuluhisha zinazotakikana ili kuondoa au kupunguza athari za hatari hizo. Itajumuisha pia mafunzo na maelekezo ya kufikia njia mpya na zilizopo za kupata mikopo. Kipengee hiki kidogo pia kitasaidia SME ambazo zinataka kuanzisha huduma ili kuboresha na kufanya utaratibu wa kutengeneza vyakula vya baharini uwe wazi zaidi. Zaidi ya hayo, mradi utatoa usaidizi wa kiufundi ili kuongoza mchakato wa kuanzisha na kuendeshwa kwa Mamlaka ya Kenya ya Soko la Samaki. b) Kipengee Kidogo cha 2.2: Kuboresha Miundombinu Inayohusiana na Uvuvi na Kilimo cha Majini kwa ajili ya kuendeleza Utaratibu wa Kutayarisha Bidhaa. Kipengee hiki kidogo kitalenga mapengo yanayobainishwa na kaunti katika miundombinu ya umma (maji, umeme, usafiri) ambayo inazuia nafasi za uwekezaji wa binafsi katika uvuvi wa mabahari na Kilimo cha Baharini. Ili kuhakikisha kuwa uwekezaji wote utathibitishwa vizuri, kuendeleza uwekezaji wa binafsi na kupunguza uwezo wa kuvua samaki kupita kiasi, miundombinu yote ya umma inayohusiana na utaratibu wa kutayarisha bidhaa inayopendekezwa na kaunti itatokana na mpangilio na ramani ya maendeleo ya miundombinu ya Kilimo cha Baharini na uvuvi katika kaunti. Mabadiliko ya anga yanayohusiana na hatari yatazingatiwa wakati wa kuanzisha uwekezaji wote wa miundombinu. Kipengee cha 3 – Riziki na Uimarishaji wa Jamii za Pwani. (Dola za Marekani milioni 30) 8. Kipengele hiki kitalenga kuimarisha maisha ya familia maskini katika jamii za pwani, kama njia ya kijitegemea na pia kuwasaidia wavuvi kutii masharti ya usimamizi wa uvuvi. Mbinu ya jumla inayolenga njia za ziada za kuendeleza maisha itafuatwa, kwa kiasi fulani kupitia kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na biashara za kifedha zilizopo au biashara mpya zinazotumia mifumo ya kilimo ya kandarasi katika kilimo cha majini au kilimo cha kawaida ili kuwasaidia watu wanaokuza bidhaa ndogo ndogo. Kwa njia ya jumla zaidi, miradi midogo ya kujipatia riziki, inayotekelezwa na watu mahususi au makundi ya biashara ndogo ndogo, itafadhiliwa kupitia utoaji wa ruzuku, usaidizi wa kiufundi na mafunzo ya ujuzi na ya biashara. a) Kipengee Kidogo cha 3.1: Kuimarisha Hali ya Maisha ya Jamii za Pwani. Kipengee hiki kidogo kinajumuisha ufadhili wa ruzuku unaosaidia watu wanaotimiza masharti kupitia njia tatu zilizobainishwa: i) Ruzuku za kujipatia riziki kwa wakulima wa kiwango cha chini wanaofanya miradi midogo, ambao wametimiza masharti; ii) Ruzuku kwa ajili ya miradi midogo ya jamii na mazingira (mtaji asili); na iii) Ruzuku za kuongeza mtaji kwa makundi ya akiba na mikopo vijijini (VSL). b) Kipengee Kidogo cha 3.2: Huduma za Usaidizi katika Kuendeleza Uwezo wa Wafanyakazi na Kuboresha Riziki. Vipengee hivi vidogo ambavyo vitatekelezwa na kaunti mahususi, vitatoa aina mbalimbali za huduma za usaidizi na kukuza uwezo wa wafanyakazi katika makundi yanayolengwa ambayo yanatarajiwa kuanzisha shughuli zinazotekelezwa chini ya kipengee kidogo cha 3.1 ikiwa ni pamoja na: i) Kutoa Huduma na Usaidizi wa Kiufundi (TA) ili kutambua na huduma ili kubaini watakaopokea ruzuku na kusaidia katika maandalizi, usimamizi na uchunguzi wa miradi midogo; ii) Kutoa mafunzo ya ujuzi na biashara kwa watakaopokea ruzuku na wafanyabiashara wengine wadogo wadogo; iii) Mpango wa Akiba na Mikopo Vijijini (VSL); na iv) Ufadhili wa masomo rasmi, mafunzo ya kiufundi na elimu ya shule. Kipengee cha 4 – Usimamizi wa Mradi. 9. Kipengee hiki cha 4 kitatoa usaidizi waziada wa kifedha katika usimamizi wa miradi katika viwango vya kitaifa na kaunti ili kuhakikisha usimamizi na utekelezaji unaofaa wa shughuli za miradi. Hususan, itasaidia kuchunguza na kusimamia mradi ikiwa ni pamoja na kuwezesha Kamati ya Kitaifa ya Kuendeleza Miradi (NPSC) na Kamati ya Kutoa Ushauri wa Kiufundi kwenye Mradi (PTAC); kuanzisha na kuendeleza Kitengo cha Usimamizi wa Mradi (PCU) katika kiwango cha kitaifa na Vitengo vya Kutekeleza Mradi (PIU) katika kiwango cha kaunti, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa, usimamizi udhamini, ikijumuisha uhasibu na ukaguzi wa hesabu za ndani/nje; mifumo ya kuhakikisha na kudhibiti ubora, usimamizi wa ulinzi wa jamii na mazingira; na ukaguzi wa kiufundi kadri inavyotakikana. Kipengee hiki pia kitatoa ufadhili wa kutayarisha na kutekeleza mikakati ya mawasiliano na utekelezaji wa mfumo wa Kutathmini na Kufuatilia. Mfumo wa Kutathmini na Kufuatilia (M&E), ambao unahitaji kutekelezwa ili kurekodi data kuhusu hatua za kifedha na hali halisi, utendaji wa shirika la utekelezaji na mashirika mengine ya kutoa huduma, na matokeo yatakayopatikana kwa njia za matumizi na mafanikio. Vile vile, itasaidia ubunifu wa Mbinu za Kushughulikia Malamiko na kuhakikisha kuwa wananchi wanashirikishwa. Eneo la Mradi 10. Mradi huu utatekelezwa katika sehemu tano zinazokaribia kingo za maji katika kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi, Lamu na Tana River; kwenye kaunti ndogo za Matuga, Kinango, Msambweni, Lunga Lunga, Kilifi Kusini, Kilifi Kaskazini, Malindi, Magarini, Lamu Magharibi, Lamu Mashariki, Tana Delta/Garsen, Changamwe, Nyali, Kisauni, Jomvu, Likoni, Mvita. 11. Mahali kwenye mradi ambapo jamii ya VMG inaishi na ambapo kifungu cha sera ya Benki ya Dunia cha OP.4.10 kitarejelewa wakati wa mradi ikijumuisha; Wadi ya Pongwe/Kikokeni (Visiwa vya mukwiro na wasini na kijiji cha Tswaka) katika kaunti ndogo ya Lunga Lunga, wadi ya Ramisi katika kaunti ndogo ya Msambweni na Samburu/Chengoni, Kasemeni, wadi za Mackinon Road katika kaunti ndogo ya Kinango zote zinapatikana katika kaunti ya Kwale; Dabaso na wadi ya Watamu katika kaunti ya ndogo ya Kilifi Kaskazini, Maarafa, wadi za Gongoni na Adu katika kaunti ndogo ya Magarini zote zinapatikana katika kaunti ya Kilifi; wadi za Kiunga na Basuba katika kaunti ndogo ya Lamu Mashariki na wadi za Hindi, Mkunumbi, Witu na Mkomani katika kaunti ndogo ya Lamu Magharibi katika kaunti la Lamu na Kipini katika kaunri ndogo ya Garsen/Tana Delta, kaunti ya Tana River. Vikundi vya VMG ambavyo vilijumuishwa katika uchunguzi huu vilikuwa; Wakifundi, Wavumba, Watshwaka, Washiratzi, Watha katika Kwale (kaunti ndogo ya Kinango) na kaunti ya Kilifi; Aweer/Boni na Saanye katika kaunti ya Lamu na Wasaanye wanaoishi katika wadi ya Kipini katika kaunti ndogo ya Tana Delta, kaunti ya Tana River. Miradi Midogo ambayo inaweza kufadhiliwa chini ya mradi wa KEMFSED kulingana na vipengele vya Mradi 12. Kipengee cha 1 – Usimamizi na udhibiti wa uvuvi wa baharini na rasilimali za majini ambao unalenga kuimarisha udhibiti wa kilimo cha majini na uvuvi wa baharini ili kuzuia matukio ya kuvua samaki kupitia kiasi na kudumisha au kuboresha ongezeko la bidhaa na kukuza hadhi ya mfumo wa ekolojia husika. Kipengee kidogo cha 1 kitalenga kusimamia na kuimarisha taasisi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za kilimo cha majini na uvuvi zinalindwa katika muktadha wa kutekeleza mfumo wa uchumi wa baharini. kipengee kidogo cha 2 kitalenga uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano ya Uvuvi (FIS) ili kuhakikisha upatikanaji wa habari za sekta zote kwa ajili ya kuwasiliana kuhusu umuhimu wa sekta ya kilimo cha majini na uvuvi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yote ya pwani. Kipengee kidogo cha 3 kitalenga kuboresha usimamizi wa uvuvi wa kiwango kidogo kidogo unaofanyika ufuoni. Kipengee kidogo cha 4 kitalenga kuboresha usimamizi wa uvuvi unaofanyika maeneo yaliyo mbali na ufuo. Utekelezaji wa Mipango ya Kuboresha Uvuvi (FIP) na usaidizi wa kubadilisha sekta ya uvuvi ili kuboresha usimamizi, utazingatia jinsi makundi ya VMG yatakavyoathiriwa na mabadiliko katika usimamizi ambayo yanaweza kujumuisha uanzishaji wa kanuni, masharti na miundo mipya ambayo znaweza kuathiri kabisa kushiriki kwa makundi ya VMG katika shughuli za uvuvi kutokana na kiwango cha chini cha elimu, matatizo ya hesabu na kiwango kidogo cha kujishirikisha katika shughuli za uchumi wa uvuvi, ingawa kuna uwezo wa kuboresha jinsi wanavyoweza kushirikishwa katika uvuvi karibu na ufuo unaofanywa na wanaume wa VMG na shughuli za kuboresha hatua za wanawake kutayarisha samaki, kama vile biashara za mama karanga, kung'oa mwani na shughuli za burudani kwenye ufuo. Mojawapo ya miundo hii ya usimamizi ni Kuanzisha Maeneo Yaliyounganishwa na Kusimamiwa kwa Pamoja (JCMA) ambayo yanajumuisha wenyeji kupitia mpango wa kupendelea wenyeji. Mashauriano yatafanyika ili kutathmini uwezekano wa athari ya miundo mipya iliyotekelezwa ya udhibiti wa uvuvi kwenye jamii za VMG. Mbinu za kujumuisha makundi ya VMG pamoja na wenyeji katika miundo ya udhibiti zitajadiliwa kupitia mikutano ya mashauriano na kukubaliwa na pande zote kabla ya kutekeleza miundo mipya au kuimarisha miundo iliyopo ya udhibiti ambayo inafaa ili kutimiza malengo ya mradi wa KEMFSED. Zaidi ya hayo, tutaangazia zaidi miundo iliyopendekezwa ambayo inalenga kuboresha usimamizi wa uvuvi wa kiwango kidogo au unaofanyika karibu na ufuo kwa sababu hii ndiyo shughuli ya uvuvi inayofanywa na makundi ya VMG katika pwani ya Kenya. 13. Kipengee cha 2 – Kuendeleza uwekezaji katika uvuvi wa baharini na kilimo cha majini ili kuwezesha utumiaji bora na kuongeza thamani kwa rasilimali kwa kuongeza kiasi cha uwekezaji katika sekta ya kilimo cha majini na uvuvi wa baharini. Kipengee kidogo cha 1 kitalenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa sekta ya binafsi katika uvuvi na kilimo cha majini kupitia Huduma za Maendeleo ya Biashara za Wastani na Ndogo Ndogo (SME/SME-DS). SME-DS zitatoa huduma za kitaalamu kwa wajasiriamali, SME na makundi ya serikali katika kaunti za pwani. Kutakuwepo na wataalam wa kuendeleza huduma za Vitengo vya Usimamizi wa Ufuo (BMU) na wenyeji wa pwani wanaotaka kuendeleza au kukuza biashara zinazohusiana na uvuvi. Pia, watatoa usaidizi wa kiufundi unapotakikana kupitia juhudi za kuboresha ujuzi wa wafanyakazi, ambazo zitajumuisha huduma za mafunzo. Utekelezaji wa shughuli katika kipengee hiki kidogo utaanza kwa kutathmini kiwango cha uwakilishaji wa makundi ya VMG, kwa wanaume au wanawake katika BMU. Uendelezaji wa uwekezaji katika uvuvi wa baharini utahitaji pia juhudi za kuboresha ujuzi wa wafanyakazi kwa lengo la kubadilisha mitazamo ya jamii za VMG ili kuchukulia shughuli za uvuvi kama uwekezaji huku wakitarajia kupata faida ikilinganishwa na mtazamo wa sasa wa jamii ambapo shughuli za uvuvi katika fuo za pwani zinafanywa na jamii za VMG kama njia ya kupata riziki tu. SME-DS itabaini pia matatizo au hatari za kimfumo ambazo zinazuia kutelelezwa kwa miradi inayotarajiwa na itapendekeza hatua za kusuluhisha zinazotakikana ili kuondoa au kupunguza athari za hatari hizo. Tutachukua tahadhari ili kuhakikisha kuwa tathmini za matatizo au hatari za kimfumo za kuzuia utekelezaji wa mradi inafanyika katika njia inayofaa tamaduni ya wanajamii wa VMG bila kupoteza utambulisho wao wa kitamaduni. Itajumuisha pia mafunzo na maelekezo ya kufikia njia mpya na zilizopo za kupata mikopo. Kipengee hiki kidogo pia kitasaidia SME ambazo zinataka kuanzisha huduma ili kuboresha na kufanya utaratibu wa kutengeneza vyakula vya baharini uwe wazi zaidi. Zaidi ya hayo, mradi utatoa usaidizi wa kiufundi ili kuongoza mchakato wa kuanzisha na kuendeshwa kwa Mamlaka ya Kenya ya Soko la Samaki. Ufikiaji wa soko la samaki chini ya Mamlaka ya Soko la Samaki nchini Kenya na masharti ya utaratubu wa utayarishaji katika ufikiaji kama huo yatakuwa sehemu ya kanuni chini ya hatua ya kupendelea wenyeji ili kuwezesha jamii za VMG kufikia huduma. Shughuli za SME-DS zitategemea SME zilizobainishwa, ambazo jamii za VMG zinafanya jinsi itakavyobainishwa katika utafiti wa Kuchunguza Jamii za VMG kama vile kujihusisha katika biashara za kiwango kidogo katika maeneo kuweka samaki na maeneo yenye samaki wengi, shughuli za watalii kutokana na vijana, biashara ya korosho na nazi na shughuli za kilimo cha mwani. 14. Kipengee kidogo cha 2 kitaboresha miundombinu inayohusiana na uvuvi na Kilimo cha Baharini ili kuwezesha uongezaji wa thamani ya bidhaa. Kaunti hii ndogo italenga mapengo yaliyobainishwa na kaunti katika miundombinu ya msingi ya umma kama vile maji, umeme na usafirishaji, ambayo inazuia nafasi za uwekezaji wa binafsi katika uvuvi na Kilimo cha Baharini. Miundombinu yote ya umma inayohusiana na michakato ya kuongeza thamani ya bidhaa, itakayopendekezwa na kaunti itatokana na mpango na ramani ya maendeleo ya miundombinu ya uvuvi na Kilimo cha Baharini katika kaunti. Hii itaunganishwa na Mipango ya Maendeleo Iliyojumuishwa katika Kaunti (CIDP) maeneo ya kaunti zinazolengwa yanayokaribia kingo za maji. Juhudi zitatekelezwa ili kuhakikisha mipango na mipangilio ya maendeleo ya uvuvi na Kilimo cha Baharini inajumuisha kwa njia ya wazi maeneo/wadi ambazo VMG wanaishi. La muhimu pia ni kuendeleza miundombinu ya maji ili iwafae kwa njia ya wazi wanajamii wa VMG, katika mpango uliojumuishwa kupitia hatua za kupendelea wenyeji. Jamii za VMG zililalamika wakati wa utafiti wa kuchunguza jamii, kwamba kulikuwa na miradi ya maji ambayo ilipitia maeneo yao lakini hawakufaidika kutokana na miradi hiyo kwa kufungua maeneo ya kuuza maji ili kuhudumia jamii za VMG jinsi ilivyofanyika katika jamii jirani za Mijikenda. 15. Kipengee cha 3 – Kuboresha Riziki inayotokana na Kilimo cha Majini na Uvuvi wa Baharini kwa jamii zinazoishi pwani, ambayo inalenga kupitia mbinu ya jumla, kuleta manufaa ya kiuchumi na kijamii ambayo jamii za pwani zitapata kupitia utumiaji wa kudumu wa rasilimali za baharini. Uendelezaji wa njia za ziada za kupata riziki kupitia mchakato wa kubuni ushirika wa kimkakati na biashara mpya za kifedha au au zilizopo, kwa kutumia mifumo ya kilimo cha kandarasi cha majini au kilimo cha kawaida ambacho kinawafaidi wakulima wadogo wadogo, itakuwa sehemu ya shughuli za kipengee hiki. Juhudi za wazi zitafanyika ili kuwezesha jamii za VMG zishiriki na zipate manufaa kutokana na miradi midogo ya kupata riziki inayofanywa na makundi mahususi ya VMG au makundi madogo ya biashara kupitia uanachama kwenye VMG. Katika hali ambapo usaidizi kama huo unatolewa kwa vikundi vya biashara kupitia uanachama kwenye VMG pamoja na wanachama wa kikundi kikubwa cha wenyeji, mbinu za ndani zitabainishwa katika uanachama wa kikundi uliojumuishwa ili kuhakikisha kuwa VMG zilizo ndani ya vikundi zinanufaika kupitia utoaji wa ruzuku, usaidizi wa kiufundi na mafunzo ya ujuzi na biashara, pamoja na wanachama wengine wa kundi. Hatua muhimu ya utekelezaji katika kipengee hiki itakuwa kurekodi kwa njia ya wazi kuwepo kwa mpango wa Akiba na Mikopo Vijijini (VSL) miongoni mwa VMG na ufaafu wa kupata manufaa kutokana na shughuli za kipengee cha tatu cha mradi wa KEMFSED. Ili kufanikisha mbinu inayojumuisha jamii kupata maendeleo yanayotarajiwa chini ya mradi wa KEMFSED, tutabuni kigezo ambapo VSL au makundi ya Jamii yanayotuma ombi, yanapaswa kuonyesha kuwepo kwa wanachama wa VMG miongoni mwa wanachama wengine wa jamii. Tunastahili kuwa makini kuzuia ujumuishaji wa wanachama wa jamii jirani wanaojifanya kuwa wawakilishi wa VMG na kutenga wawakilishi halisi wa VMG kwenye vikundi vinavyozingatiwa kupata ruzuku na kuboresha uwezo wa wafanyakazi. Kigezo cha kuchagua VMG katika mashirika makubwa ya jamii kitabuniwa kupitia mchakato wa mashauriano wakati wa kubuni VMGP na kujumuisha VMGP katika mpango wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya KEMFSED. 16. Kipengele cha 4 –Kipengee hiki kinalenga usimamizi wa mradi ambao unajumuisha uzinduzi na utekelezaji wa kamati ya mradi, wadhamini na ulinzi wa jamii na mazingira na ufuatiliaji na kutathmini mradi. Utekelezaji unaofaa wa ulinzi wa kijamii na kimazingira unaobuniwa na KEMFSED utahakikisha kushirikishwa na kujumuishwa kwa jamii ya VMG katika shughuli za mradi. 17. Kutokana na matokeo ya utafiti wa kuchunguza jamii na ukaguzi wa mpango wa utekelezaji wa mradi wa KEMFSED, kuna uwezekano wa kupendekeza miradi kadhaa midogo. Kuna uwezekano kuwa miradi hii midogo inaweza kupendekezwa ili kufathiliwa chini ya vipengee vitatu vya mradi wa KEMFSED ambavyo vinajumuisha; Udhibiti Bora wa Uvuvi na Uchumi wa Baharini, Kuboresha Usimamizi wa Uvuvi Karibu na Fuo, Kuendeleza Miundombinu ya Usimamizi wa Uvuvi chini ya kipengee cha kwanza. Miradi midogo inayoweza kubuniwa chini ya kipengee hiki italenga kuzuia matendo ya kuvua samaki kupita kiasi, uvuvi haramu na shughuli za uvuvi ambazo haziripotiwi katika Fuo za Bahari ya Hindi. 18. Baadhi ya shughuli za miradi midogo ambazo zitapendekezwa chini ya kipengee hiki kidogo zinaweza kujumuisha; kuzuia matendo ya kuvua samaki kupita kiasi, kudumisha uzalishaji wa samaki na kuboresha mfumo husika wa ekolojia. VMG zinaweza kunufaika kutokana shughuli za kuvua samaki kupita kiasi kupita shughuli za ‘mama karanga’. Kuna jamii za VMG ambazo zinahusika na uhifadhi wa msitu wa mikoko ambayo inatambulika kuwa maeneo muhimu ya kudumisha ukuzaji wa samaki na mfumo wa ekolojia ya bahari. Juhudi za kuboresha uwezo wa wafanyakazi zinazolenga kuimarisha shughuli za miradi midogo chini ya kipengee hiki kidogo zinaweza kufanywa katika lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka na jamii zote za VMG. Zaidi ya hayo, shughuli nyingine za miradi iliyo chini ya kipengee hiki zinaweza kujumuisha kuimarisha usimamizi wa uvuvi unaodumu na utumiaji wa rasilimali za baharini na inaweza kuhusisha uimarishaji wa taasisi za usimamizi na kubuni masharti mapya au kuendeleza masharti yaliyopo yanayohusu shughuli za uvuvi ambayo hayawezi kuathiri riziki ya watu mahususi wanaotumia boti za kuvuta nyavu, neti au mikuki na pia jamii nzima ambayo inategemea uvuvi kwa jumla. Hii itajumuisha shughuli za jamii za VMG ambao ni mama karanga wanaofanya biashara ya samaki katika maeneo ya kuweka samaki, zinazotegemea kiwango cha samaki waliovuliwa. Kuna uwezekano kuwa shughuli za mradi mdogo zitajumuisha kuboresha/kupanua miundombinu ili kuboresha usimamizi wa uvuvi kando na maeneo ya kuweka samaki, maeneo yenye samaki wengi kama vile Shimoni, kupanua na kuwezesha BMU ili kuboresha shughuli za usimamizi wa uvuvi. Kuna BMU ambazo zinajumuisha VMG wengi ambako watu wa VMG hizo ndio wengi katika jamii. Hii ni hali halisi katika BMU walio katika Visiwa vya Mukwiro na Wasini pia BMU wa Bodo na Munje katika kaunti ya Kwale ambazo zina Washiratzi wengi. Hata hivyo, kuna ubaguzi na utengaji wa jamii za VMG katika maeneo mengine kama vile BMU ya Kilifi ambapo jamii za VMG zinaishi pamoja na jamii za Mijikenda, Wabajuni na Wapemba. 19. Utafiti wa kuchunguza jamii ya VMG ulionyesha kuwa kutokana na hali ya utengaji, jamii za VMG hazifikii taasisi za mikopo, hazina makundi ya kujitegemea yaliyosajiliwa au Mashirika ya Jamii (CBO) na kuwa baadhi ya mashirika ya jamii ambayo yalianzishwa hapo awali yalianguka kutokana na usimamizi mbaya na ukosefu wa soko kwa bidhaa zao kama vile mwani. Vijana katika jamii za VMG ambao wanajihusisha katika shughuli za utalii wamesajili makundi ya vijana ambayo yanajumuisha wahudumu wa mashua (aghalabu ni wanaume) na wanawake kufanya shughuli za burudani kwenye ufuo. Utafiti wa kuchunguza jamii ulionyesha kuwa wanapata changamoto za kufikia huduma za mikopo na kuna umuhimu wa kuboresha uwezo wa wafanyakazi ili waweze kushindana na watu wengine wanaojihusisha na shughuli za kuendeleza utalii, zinazowapa riziki. 20. Baadhi ya miradi midogo katika kipengee cha 2 inaweza kujumuisha kuendeleza shughuli za kilimo cha majini na Kilimo cha Baharini kupitia miundombinu bora, kuendeleza biashara Ndogo Ndogo na za Wastani (SME) kwa kutoa mikopo, ushauri au kuboresha uwezo wa wafanyakazi watakaopata mikopo. Jamii za VMG zitalengwa na shughuli hizi katika mradi. 21. Kipengee cha 3 cha KEMFSED kinalenga kuwezesha jamii za pwani na kuwapa njia za kudumu za kupata riziki kupitia huduma za usaidizi na riziki kwa Jamii za Pwani zinazolenga kuimarisha riziki na kuboresha uwezo wa wafanyakazi. Baadhi ya shughuli za miradi zitakazofanyika chini ya kipengele hiki ni pamoja na; kutoa ufadhili wa elimu, kutoa zawadi za kifedha na za kiufundi kama njia za ziada za kupata riziki na kupanua nyenzo za mapato na kuendeleza utalii wa Baharini na Pwani. Hizi zinaweza kujumuisha kuendeleza shughuli za kilimo, kuwapa vijana mafunzo ili kupata riziki kupitia shughuli za kitalii na kufufua baadhi ya viwanda vilivyokuwa vimeanguka kama vile kiwanda cha korosho na kuboresha njia za mapato yanayotokana na ukulima wa nazi. Pia itasaidia makundi ya jamii ili yapande miti kama njia mbadala ya kukuza mikoko. Kwa mfano, miongoni mwa Washiratzi, kuna Shirika la Jamii la Misitu (CFA) ambalo linahifadhi misitu na juhudi hizi zinastahili kuigwa katika jamii nyingine za VMG ili zihifadhi mikoko. Wakifundi na Wavumba tayari wanajihusisha katika shughuli za kitalii licha ya kupata changamoto kadhaa ambazo zinawazuia kutekeleza uwezo wao kikamilifu. Kutakuwepo na juhudi za kusaidia njia hizi mbadala za kupata riziki kupitia ubunifu wa mipango ya hatua kujumuishwa kwa jamii za VMG ambazo zinategemea mipango ya jumla ya utekelezaji wa mradi wa KEMFSED. Mipango ya Utekelezaji 22. Mradi wa KEMFSED utatekelezwa na Idara ya Taifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini kama shirika kuu, kwa ushirikiano na idara mbalimbali za serikali kama vile za mimea, Mifugo, usimamizi wa uvuvi, Hazina ya Kitaifa, Idara ya Kitaifa ya Mazingira na Misitu, mwenyekiti wa kamati ya idara za serikali katika Sekta ya Kilimo, Kitengo cha Mfumo wa Usimamizi wa Fuo za Bahari ya Pwani, Shirika la Pwani la Wakulima wa Samaki na Shirika la Kenya la Watayarishaji na Wauzaji wa Samaki katika Nchi za Kigeni (AFIPEK) katika ngazi ya kitaifa; Serikali za kaunti husika katika fuo za pwani zitakuwa mashirika ya utekelezaji wa mradi katika kiwango cha serikali za kaunti. Zitatoa mbinu za ufuatiliaji na utekelezaji katika kiwango cha kaunti. Chini ya viwango vya kaunti vya utekelezaji na viwango vya usimamizi, kutakuwa na viwango vya jamii vya miundo ya utekelezaji ambavyo vitajumuisha hasa Mashirika ya Maendeleo Yanayosimamiwa na Jamii. Miundo ya utekelezaji katika kiwango cha jamii itakuwa na kamati ndogo. Kutakuwepo na mashauriano mengine baada ya Mashauriano yanayoeleweka, ya wazi na yanayopangwa mapema (FPIC) yanayofanywa katika jamii za VMG kuhusu mipango ya utekelezaji WA mradi wa KEMFSED na kutambua mikakati ya kutekeleza mradi jumuishi ambao unazingatia sifa za kipekee za uchumi na jamii za VMG kabla ya kufanya mikutano ya mashauriano ya utekelezaji wa jamii yote. Methodolojia 23. Data ilikusanywa kwa wakati mmoja ili kufahamisha SA na VMGF kwa kutumia njia za msingi na za upili. Data ya upili ilipatikana kupitia kusoma vitabu, ilhali data ya msingi ilikusanywa kupitia mashauriano na wadau, kuhoji wataalamu (KII), majadiliano yanayoangazia makundi (FGD) na kutembea nyanjani. Mifumo ya Sheria, Sera na Taasisi 24. Katiba ya Kenya (CoK) 2010 inatambua haki za tamaduni uchumi na uchumi wa jamii za wananchi wote jinsi ilivyoashiriwa katika Kifungu cha 56 kinachohusu Makundi ya waliotengwa na ya wachache. Kifungu hiki kinabainisha kuwa “taifa litaanzisha mipango ya kupendelea wenyeji ambayo itahakikisha kuwa makundi ya waliotengwa na ya wachache yanashiriki na kuwakilishwa katika uongozi na sehemu nyingine za maisha, b) yanapewa nafasi maalum katika nyanja za uchumi na elimu, c) yanapewa nafasi maalum za kazi, d) yanaendeleza matendo, lugha na shughuli za kitamaduni, na e) yanapata huduma nzuri za maji, matibabu na miundombinu. Kifungu cha 260 kinatambua makundi yaliyotengwa na yaliyotelekezwa. Kinatambua jamii za VMG kuwa jamii za wachache ambao wametengwa kupitia matendo ya kihistoria. Inakataza ubaguzi wa makundi yaliyotengwa kupitia dhana kuwa jamii hizo zina watu wachache au sababu nyinginezo, haijaweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi na jamii nchini Kenya kwa jumla. Pia, inatambua jamii ambazo zimedumisha utambulisho na tamaduni zao za kipekee, hatua inayozizuia kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi katika nchi ikiwa ni pamoja na usasi na utafutaji wa vyakula mwituni, miongoni mwa nyingine. Utambuaji wa makundi haya ya VMG unapaswa kuchangia katika uhifadhi wa utambulisho wao na kuwawezesha washirikishwe katika maendeleo na makundi mengine, ikiwa ni pamoja na shughuli za kisiasa. Hali za Uchumi wa Jamii za Kaunti za KEMFSED 25. VMG ilibaini ukosefu wa zana za uvuvi unaofanyika katikati mwa bahari, ukosefu wa ujuzi wa uvuvi, kukosa kuwakilishwa katika miradi ya jamii ikiwa ni pamoja na uanachama katika Vitengo vya Usimamizi wa Fuo kwa sababu zinashindwa katika kura na makundi yenye watu wengi. Makundi ya Waliotengwa na Waliotelekezwa (VMG) yana matatizo ya mashamba na wanaishi kama maskwota. 26. Vijana katika makundi ya VMG wameanzisha njia za kutengeneza mapato kupitia miradi ambayo inajumuisha uhifadhi wa mazingira (upanzi wa miti na kuhifadhi mikoko), kuosha magari, huduma za burudani kwenye ufuo na shughuli za mashua zinazolenga watalii. 27. Wanawake miongoni mwa makundi ya VMG wamejikita katika shughuli za ukulima wa mwani, ushonaji na ‘mama karanga’ (kukaanga samaki) kuwa njia ya kutengeneza mapato pamoja na ukulima wa vyakula ambao unategemea mvua. 28. SA ilitambua kuwa makundi mengi ya VMG yanapungua katika idadi au yanaacha tamaduni zao ili kufuata tamaduni za wengi; kwa mfano, lugha ya Kisaanye inapotea na inajumuishwa katika tamaduni na lugha ya Kibajuni. Watha wamejipanga ili kulinda utamaduni wao, kutetea haki zao na kuhamasisha jamii zao ili kuendeleza mipango ya maendeleo. 29. Kuna kiwango cha chini cha elimu miongoni mwa jamii za VMG katika Pwani ya Kenya. Kiwango cha chini cha elimu kinatokana na ukosefu wa pesa za kulipa karo ya watoto kwa sababu ya viwango vikubwa vya umaskini. Ukosefu wa elimu rasmi unaoendeleza hali ya kutengwa na jamii jirani. Athari Zinazoweza Kutokea Kulingana na Vipengee Kipengee cha 1: Kuboresha Udhibiti na Usimamizi wa Uvuvi wa Baharini. 30. Makundi ya VMG yatafaidika haswa kutokana na uimarishaji wa taasisi kama vile BMU kupitia kuboresha uwakilishaji wake katika miundo ya usimamizi wa uvuvi kwenye maeneo ya pwani. Kuzuia shughuli za kuvua samaki kupita kiasi na kudumisha uzalishaji wa samaki pamoja na mfumo wa ekolojia ulioimairishwa utachangia kuongezeka kwa idadi ya samaki wanaovuliwa na kuongezeka kwa mapato ya makundi ya VMG. 31. Nafasi za kazi zitaongezeka kupitia watu kujiari au kuajiriwa iwapo shughuli za uvuvi zitasimamiwa vizuri. Kipengee cha 2: Kuwezesha Uwekezaji wa Kudumu katika sekata ya Uvuvi wa Baharini na Kilimo cha Majini 32. VMG zitanufaika kutokana na mipango ya kuendeleza kilimo cha majini kama njia mbadala za kutengeneza pesa kupitia mpango wa mradi wa KEMFSED wa kujadili vikwazo vinavyozuia uwekezaji katika shughuli za kudumu za uvuvi. 33. Baadhi ya VMG katika utafiti wa kuchunguza jamii walisema kuwa waliacha kujihusisha katika kilimo cha mwani kwa sababu walikosa soko la bidhaa zao. Uboreshaji wa mazingira ya biashara kupitia shughuli za mradi wa KEMFSED utaimarisha ufikiaji wa soko kwa wakulima wa mwani na kuendeleza shughuli za kilimo cha majini katika jamii za VMG. Kipengee cha 3: Riziki na Uimarishaji wa Jamii za Pwani 34. Utafiti wa kuchunguza jamii uliofanywa na KEMFSED umeonyesha kuwa jamii za VMG zilizo katika eneo la mradi zinakosa uwezo wa kiufundi (ujuzi unaotakikana katika shughuli za uvuvi bora) na uwezo wa kifedha (vifaa vya uvuvi) ambazo zinaweza kuwasaidia wapate riziki ya kudumu kutokana na rasilimali za baharini. Zaidi ya hayo, utafiti wa kuchunguza jamii umeonyesha umuhimu wa kuwa na mabadiliko ya mitazamo ya jamii za VMG kuwa uvuvi unaweza kutumika kama shughuli za kibiashara lakini si kwa matumizi ya nyumbani pekee. Pia VMG walielezea kuwa watoto wao hawawezi kupata ufadhili wa kielimu au pesa zilizotengewa jamii ambako wanaishi kutokana na ubaguzi. Watanufaika kutokana na shughuli za mradi wa KEMFSED zinazolenga kuimarisha uwezo wa jamii kupata ujuzi wa biashara na kupata usaidizi wa ruzuku na kifedha. Mipango kama hiyo ya kuboresha uwezo wa wafanyakazi itakuza ujuzi wao katika uvuvi na biashara ikiwa ni pamoja na kubadilisha mitazamo kuhusu shughuli za uvuvi. 35. Utoaji wa huduma za mikopo na ufadhili wa elimu utaboresha viwango vya elimu kwa watoto katika jamii za VMG kwa kuwafanya kuendelea na masomo. 36. Utafiti wa kuchunguza jamii ulionyesha kuwa kuna mashirika yaliyopo ya Jamii ambayo yamesajiliwa ama hayajasajiliwa ambayo yanatoa mikopo kwa jamii za VMG. Pia kuna ushahidi wa mashirika ya jamii ambayo yalianguka katika maeneo ya jamii za VMG. Makundi ya VMG yatapata fursa ya kufufua mashirika yaliyoanguka au kuimarisha mashirika ya jamii yaliyopo kupitia njia za kupata fedha na mikopo. 37. Kuboresha shughuli za uchumi na utumiaji wa kudumu wa rasilimali za bahari kupitia mpango jumuishi utaendeleza utangamano katika jamii miongoni mwa makundi ya VMG na jamii kubwa jirani ili yaishi kwa amani. Athari Mbaya Zinazoweza Kutokea 38. Utafiti wa kuchunguza jamii ulionyesha kuwa kuna wanawake – ‘mama karanga’ ambao wanapata samaki kutoka kwa wavuvi wa kiume wanaotoka baharini ili wazikarange na wawauzie wenyeji katika maeneo ambayo samaki zinaletwa kutoka Bahari ya Hindi ya pwani mwa Kenya. Hiki ni kitega uchumi kikuu ambacho ni maarufu kwa wanawake maskini na wanaoweza kutelekezwa ambao pia wanatafuta riziki kwa familia zao katika Pwani mwa Kenya. Usasishaji na uboreshaji wa maeneo ya kuwekwa samaki, unaweza kuanzisha kodi na masharti mapya ya usafi. Hali hii inaweza kuwafurusha mama karanga kwenye biashara zao na kuathiri riziki ya jamii za VMG ambazo tayari ni maskini. Kama njia ya kuzuia hili, kupitia mpango wa makazi mapya, njia za ziada za kupata riziki zitaanzishwa katika mradi huu kuwa njia za kufidia hasara yoyote inayotokana na uchumi. 39. Utafiti huu ulionyesha zaidi kuwa kuna vijana ambao wanabeba wasafiri kwa mashua kati ya visiwa kama vile jamii za Wakifundi na Wavumba katika Visiwa vya Mukwiro na Wasini katika bandari ya kuweka samaki ya Shimoni. Vijana hawa wanaoendesha mashua wanasafirisha watu kutoka na kuenda barani na kituo cha afya ambacho wenyeji wanategemea kiko Msambweni –Msambweni Sub-District Hospital. Vijana walihofia kuwa uboreshaji wa bandari ya Shimoni, uwezekano wa kuzuia usafiri na uanzishaji wa vyombo vikubwa vya majini, zinaweza kufanya wakose kazi. Pia kulikuwa na hofu kuwa njia ya kufikia kituo cha afya cha Msambweni itakuwa vigumu iwapo bandari itaboreshwa na mashua ndogo kuzuiliwa kufanya kazi kwenye visiwa. Pia, usasishaji wa bandari ya Shimoni unaweza kusababisha uhamiaji wa wahudumu wengi walioelimika wanaoendesha mashua, ambao wanajimudu katika lugha za kigeni kama vile Kihispani, Kifansa na Kijerumani, walio na vyeti vya Mawasiliano ya Kompyuta ambao unatakikana ili kuhudumu katika sekta ya utalii, hali ambayo itawaathiri wenyeji Wavumba na Wakifundi wanaoendesha mashua na hawajui lugha hizi za kigeni. 40. Shughuli za mradi wa KEMFSED zitaathiri vibaya Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMG) iwapo shughuli za mradi zitasababisha uharibifu wa miti au maeneo ya kidini kama vile makaburi au maeneo ya kuabudu. Jamii za VMG ziliteta kwamba hakutakuwa na mashauriano iwapo shughuli za mradi zitaharibu misitu na maeneo ya kidini. Mipango ya Kufuatilia na Kuripoti 41. Ripoti za maendeleo ya kila robo ya mwaka zitaandaliwa na mashirika yanayotekeleza mradi kuanzia mifumo ya kiwango cha jamii, kaunti na mifumo ya kiwango cha kitaifa, kama masharti ya ripoti ya jumla ya Ufuatiliaji na Tathmini ili kufafanua maandalizi na utekelezaji wa VMGP na malalamiko yaliyopatikana na kusuluhishwa. Ripoti hii itawasilishwa kwa Benki ya Dunia kupitia shirika linaloongoza utekelezaji – idara ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini. Mifumo ya Kufuatilia na Kutathmini Mradi 42. Hatua zifuatazo zimependekezwa kuwa mbinu za kubuni mfumo bora wa kutathmini na kufuatilia mradi: • Kuhamasisha na kufunza jamii kuhusu usanifu, uandalizi na utekelezaji wa mradi. Mafunzo haya yanayolenga jamii yanapaswa kushirikisha wadau wote katika viwango vya jamii na vinajumuisha; viongozi wa jamii, viongozi wa madini na utamaduni, vijana (wakibainishwa kulingana na jinsia), wanawake na makundi mengine husika katika jamii • Kubuni mbinu ya kuhakikisha kuwa kuna mfumo wa kutoa maoni kwa wakati unaofaa, ambao unaweza kudumisha kuangaziwa kwa shughuli za mradi. Mbinu hii itakayobuniwa wakati wa mashauriano ya jamii inapaswa kuwa na mbinu ya kindani ya kuwawezesha wawakilishi wa jamii kutoa ripoti maendeleo kwa jamii pana. Aidha, njia zinazofaa na zilizokubaliwa za mawasiliano katika jamii zinatakiwa kubuniwa ili kuimarisha shughuli za kutathmini na kufuatilia mradi. • Timu inayofaa ya kufuatilia na kutathmini mradi inapaswa kuwepo na itajumuisha wawakilishi waliochaguliwa wa jamii ya VMG kuwa miongoni mwa wawakilisha kutoka kwa jamii jirani, wawakilishi wa serikali ya kaunti na wawakilishi wa kamati ya utekelezaji wa mradi wa KEMFSED. • Mbinu inapaswa kubuniwa ili kujumuisha wawakilishi waliochaguliwa wa vijana, walemavu na wanawake katika timu ya kutathmini na kufuatilia mradi. Viashiria vya Kutathmini na Kufuatilia Mradi wa KEMFSED/VMGF 43. Jedwali lililo hapa chini linaonyesha viashiria vya kufuatilia na kutathmini jinsi KEMFSED itakavyoathiri jamii ya VMG. Ufuatiliaji na Tathmini Kiashiria Wajibu Vyanzo vya Data Viashiria vya KEMFSED Mradi Juhudi za kuboresha Idadi ya wanachama wa Usimamizi wa Warsha za mafunzo uwezo wa wafanyakazi VMG waliopata mafunzo Uvuvi na Idara katika SME, ujuzi wa ya biashara, kuvua, ya Kitaifa ya uvuvi, kuendesha mashua Uvuvi na Kuendesha mashua, Na ujuzi wa usalama wa Uchumi wa usalama baharini na baharini, Kilimo cha Baharini shughuli za utalii Baharini na kilimo cha zinazohusika, Kilimo cha majini. Baharini Na kilimo cha majini Kuipa jamii mapema Idadi ya wanachama wa Usimamizi wa Fomu za maombi ya Vifaa vya uvuvi vya kisasa VMG ambao wamepata Uvuvi na Idara bidhaa (neti, boti n.k) boti na neti bora za uvuvi, ya Kitaifa ya zinazonunuliwa nk Uvuvi na Uchumi wa Baharini Kuimarisha ufikiaji wa Idadi ya wanachama wa Usimamizi wa Rekodi ya huduma za ufadhili wa VMG ambao wamenufaika Uvuvi na Idara walionufaika kupata kifedha na usaidizi wa kutokana na usaidizi wa ya Kitaifa ya usaidizi wa kifedha ruzuku ruzuku/kifedha Uvuvi na na ruzuku Uchumi wa Baharini Ushauri kwa walionufaika Idadi ya VMG Usimamizi wa Orodha za kutokana na usaidizi wa walionufaika kutokana na Uvuvi na Idara mahudhurio na ripoti ruzuku na fedha usaidizi wa ruzuku na ya Kitaifa ya za mafunzo Usaidizi fedha ambao wamefunzwa Uvuvi na kuhusu SME Uchumi wa Baharini Ufadhili wa elimu Idadi ya wanajamii wa Usimamizi wa Rekodi za VMG ambao wamenufaika Uvuvi na Idara walionufaika kutokana na ufadhili wa ya Kitaifa ya kutokana na ufadhili elimu katika viwango Uvuvi na wa elimu katika mbalimbali Uchumi wa vikundi mbalimbali Baharini Ufuatiliaji wa utendaji wa Wawakilishi wa wanajamii Usimamizi wa Ripoti za Kufuatilia BMU wa VMG katika BMU Uvuvi na Idara na Kutathmini Mradi ambapo BMU hiyo ya Kitaifa ya inapatikana katika Uvuvi na jamii/mfumo wa Uchumi wa wanajamii wa VMG Baharini Kuboresha uwezo wa Idadi ya wawakilishi wa Usimamizi wa Orodha za Wafanyakazi katika BMU VMG ambao Uvuvi na Idara mahudhurio na ripoti wameshiriki/kuhudhuria ya Kitaifa ya za mafunzo vipindi vya kuboresha Uvuvi na uwezo wa wafanyakazi Uchumi wa katika BMU Baharini Usajili na utoaji leseni wa Idadi ya mashua za uvuvi Usimamizi wa Ripoti za Kufuatilia mashua za uvuvi zinazomilikiwa na VMG Uvuvi na Idara na Kutathmini Mradi ambazo zimesajiliwa na ya Kitaifa ya kupewa leseni ili Uvuvi na zihudumu katika BMU Uchumi wa Baharini Uwezeshaji wa jinsia ili Ulinganishaji wa idadi ya Usimamizi wa Ripoti za Kufuatilia kupata riziki ya ziada wanawake na wanaume Uvuvi na Idara na Kutathmini Mradi Shughuli katika VMG ambao ya Kitaifa ya wamewezeshwa kuendesha Uvuvi na SME, wamesaidiwa Uchumi wa kufanya kilimo, Baharini Uendelezaji wa shughuli za Idadi ya shughuli za Usimamizi wa Ripoti za Kufuatilia kudumu za mfumo wa kuhifadhi mazingira katika Uvuvi na Idara na Kutathmini Mradi ekolojia jamii (mikoko, njia ya Kitaifa ya mbadala ya kupanda miti Uvuvi na nk) ambazo zimeanzishwa Uchumi wa na kujumuisha uongozi wa Baharini VMG miongoni mwa wanachama wengine katika jamii pana Mikutano ya uhamasishaji Idadi ya mikutanao ya Usimamizi wa Rekodi za mikutano wa jamii ya kusaidia jamii uhamasishaji ya kusaidia Uvuvi na Idara za jamii pana ya VMG jamii pana iliyofanywa ya Kitaifa ya miongoni Uvuvi na mwa/kuhudhuriwa na Uchumi wa jamii za VMG Baharini Mbinu ya Kushughulikia Malalamiko 44. Kila mwanachama wa VMG katika eneo la mradi alikuwa na mbinu thabiti za zinazoongozwa na tamaduni/mila kulingana na mfumo wa Baraza la Wazee ambao waliashiria kuwa njia waliyopendelea kusuluhisha mizozo wakati wa kutekeleza VMGP. Kulingana na jamii nyingi, mwanajamii yeyote ambaye anakataa kukubali unamuzi wa “mahakama” za kimataduni amelaaniwa na wazee na jamii na yuko tayari kusuluhisha mzozo kupitia njia za mahakama na kisheria. Kanuni hii itatumika kama njia ya kusuluhisha mizozo katika mradi huu. 45. Wakati wa mashauriano, wanachama mbalimbali wa VMG walielezea kuwa wangependa kusuluhisha mizozo na malalamiko kupitia miundo ambayo wamewakilishwa kikamilifu na isiyoathiriwa zaidi na jamii kuu. Walipendekeza kiwango cha chini zaidi, yaani kiwango cha jamii, kwa kutumia mifumo ya kiusimamizi na ya kitamaduni ya wazee wa vijiji kadri iwezekanavyo. Walitilia shaka viwango vya juu vya Kusuluhisha Mizozo kwa kuwa hawajawakilishwa na hawakuamini mifumo ambayo inasimamiwa na watu waliosoma sana. Mipango ya Kuidhinisha na Kuvumbua Kuidhinisha 46. Rasimu hii ya VMGF itapitia hatua mbalimbali za uidhinishaji katika Idara ya Kitaifa ya Uvuvi, Kilimo cha Majini na Kilimo cha Baharini, timu ya utekelezaji wa mradi wa KEMFSED na timu ya Ulinzi wa Benki ya Dunia katika nchi na kanda. Uvumbuzi 47. Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya CoK, 2010 na sera ya Benki ya Dunia ya Kuvumbua kwa Umma, 2011, uwazi na uwajibikaji ni mambo muhimu katika mchakato wa maendeleo yanayolenga kupunguza umaskini. Kwa hivyo, uvumbuzi katika umma wa VMGF utachukua mtindo wa: (i) shughuli ambazo mradi unafadhili; (ii) jinsi rasilimali zimegawanywa na kutumiwa; (iii) maendeleo katika utekelezaji wa mradi; na mwisho, (iv) mafunzo ambayo yametokana na mradi ili yashirikiwe miongoni mwa wadau na wahusika wa mradi. 48. Njia inayofaa ya kuvumbua maelezo haya itabainishwa mara kwa mara, japo kupitia mashauriano tulifahamu kuwa mabaraza ya umma (mikutano ya jumla ya jamii), wadi, utawala wa eneo, miundo inayofaa ya kiwango cha kaunti na kaunti ndogo na ofisi za chifu ingependelewa kwa VMG. Uvumbuzi hasa katika kiwango cha jamii, hasa kupitia mabaraza ya jumla utafanyika katika Kiswahili, lugha ambayo inatumiwa zaidi na jamii ya VMG. Muhtasari utafaa katika hali hii. Ripoti kamili inapaswa kuvumbuliwa kwenye makao makuu ya Kaunti na Kaunti ndogo. Mwisho, VMGF imechapishwa kwenye tovuti za washirika wanaotekeleza mradi, haswa zile za idara ya Kitaifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini na pia Tovuti za Nje za Kimataifa. Muhtasari wa Mapendekezo, Majukumu na Wajibu wa KEMFSED Mapendekezo 49. Ili kushirikisha VMG zaidi, kuna umuhimu wa kujumuisha jamii katika hatua zote za mradi. Wakati wa utekelezaji, ujumuishaji wa VMG na uhusiano wao na jamii nyingine, pamoja na athari za mradi katika masilahi yao yanapaswa kufuatiliwa kikamilifu. a) Shughuli zinazofaa za uhamasishaji na uwasilishaji zinapaswa kuratibiwa kupitia hatua mbalimbali zinazotumika za mawasiliano, kuwa sehemu ya mbinu za utoaji huduma (yaani ulengaji, malipo, G&CM nk.). Inatarajiwa kuwa hali hii itaendelea katika awamu zote za huduma ya KEMFSED, na kutekelezwa zaidi wakati wa KEMFSED. b) Mikakati na zana za mawasiliano itajumuisha mabaraza ya jumla ya jamii, redio, SMS, vipeperushi, matangazo kupitia megafoni nk. Hususan, Mikakati ya Uhamasishaji kwa Wanaonufaika kupitia ujumbe maalum wa VMG itatumika ili kuhakikisha ujumuishaji wa VMG na itatoa mbinu zinazofaa za kuhakikisha kuwa VMG wamefikiwa na kuwa habari inatolewa kwa njia ambazo zinaeleweka kwa urahisi. Huenda hatua hii itahitaji kulenga makundi mbalimbali ya VMG, kulingana na mahali waliko, lugha, kiwango cha elimu, kujumuishwa katika jamii pana na elimu ya uraia. c) Kuandika idadi na aina ya malalamiko ambayo yamewasilishwa kuhusu mradi na hatua ambazo zimechukuliwa na kuhakikisha kuwa njia zinazofaa zimebuniwa na kutekelezwa. d) Kukusanya data ya malalamiko na maoni ya wanaonufaika mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa maeneo yanayolengwa ambayo jamii ya wachache ipo yanafikiwa na malalamiko yanayojirudia yanapelelezwa ili kupata njia za kuyasuluhisha. e) Kuhakikisha kuwa vizuizi vya ujumuishaji (kama vile ugumu wa kupata Vitambulisho na Huduma Namba) vinashughulikiwa kwa wanajamii husika, ikiwa ni pamoja na VMG. f) Ufahamu na rekodi bora za lugha, tamaduni na kizazi cha Wasaanye itatakikana ili kuchunguza Wasaanye ambao watanufaika kutokana na mradi wa KEMFSED na miradi ya baadaye ya Benki ya Dunia inayolenga jamii Zilizotengwa na Zinazotelekezwa g) Kuna umuhimu wa mawasiliano ya ziada katika jamii ili kubainisha maeneo mengine ambako inatarajiwa kuwa shughuli za mradi wa KEMFSED zinaweza kuathiri misitu ya kidini na sehemu za VMG. 50. Kuna umuhimu wa kuhamasisha na kuwapa mafunzo wadau wote kuhusu utambulisho na ujumuishaji unaofaa wa aina mbalimbali za VMG. Kwa hivyo, mashirika yanayotekeleza KEMFSED yanapaswa kukagua hifadhidata iliyopo ya VMG kwa kila kaunti ya KEMFSED. Zaidi ya hayo, maafisa wa mpango wanapaswa kuhamasishwa kuhusu hali za ukasumba, na jinsi ya kujumuisha makundi kama hayo katika KEMFSED. Hatua hii itasaidia kuelewa sifa na maeneo ya VMG na kuwahamasisha maafisa kuhusu VMG ili waweze kuwasiliana nao na kuwalenga vizuri. Ili kuongeza uhusiano na VMG, kuna haja ya kuhimiza ushirikiano kati ya idara za serikali za uvuvi na uchumi wa baharini na washirika wa utekelezaji na mashirika mengine ya jamii na ya serikali ambayo yanafanya kazi na VMG. 51. Elimu ya uraia na mafunzo kwa jamii yanapaswa kufanywa ili kuimarisha weledi na haki za kila mtu, ikiwa ni pamoja na VMG. Mafunzo kuhusu haki yanaweza kufanywa kama sehemu ya mpango wa kuhamasiaha wanaonufaika katika jamii na wote wanaonufaishwa na KEMFSED. 52. Wakati wa kuwasiliana na VMG, hakikisha kuwa njia na mbinu zinazofaa za mawasiliano zinatumiwa na kutambuliwa na wanajamii wa VMG wenyewe. Huenda vituo vya redio vya FM visifikiwe au kueleweka na kila mtu. Kwa hivyo, unaweza kupiga simu, kutuma ujumbe kwa wawakilishi na viongozi na kufanya mikutano ya mabaraza ya moja kwa moja. 53. Wakati unalenga makundi ya wachache, jumuisha makundi ya wachache wakati wa kupanga ili wakuunge mkono na uendeleze utangamano unaofaa. Hakikisha kuwa makundi ya wanawake na vijana yanashauriwa vizuri kuhusu njia bora ya kuyahusisha na mapendekezo yao ili mradi utimize malengo yake. 54. Mashirika ya utekelezaji yanapaswa kuandaa VMGP kwa kila shughuli ya KEMFSED iwapo VMG watatambuliwa kuwepo katika eneo la shughuli na kuchukuliwa kuwa wameathiriwa na shughuli na itaongozwa na sheria ya Benki ya Dunia ya OP4.10, Annex B. Hususan, VMGP itatayarishwa kwa ajili ya jaribio la mikakati ya kiuchumi, kwa kuwa athari kwenye VMG inatarajiwa iwe kubwa zaidi katika shughuli hizi. Hata hivyo, VMGP pia itaandaliwa katika shughuli hizo nyingine mbili (utoaji wa pesa na upanuaji wa neti za usalama), panapofaa, kutokana na utambuaji wa VMG katika maeneo ya mradi. Idhini ya Benki ya Dunia kwa VMGP itatakikana kabla ya utekelezaji. Majukumu na Wajibu Mashirika ya Utekelezaji wa KEMFSED 55. Mashirika ya utekelezaji wa KEMFSED katika Kaunti yatakuwa na wajibu wa: i. Kubaini makundi ya VMG katika kaunti zao, ikiwa ni pamoja na mahali waliko na jinsi ya kuwafikia; ii. Kuendeleza VMGP ili kutambua athari kubwa, kubuni njia za kusuluhisha na kutoa mwelekeo kuhusu jinsi njia hizo za kusuluhisha zitafadhiliwa na kufuatiliwa. iii. Kuchunguza athari za mradi na ufanisi wa njia zilizopendekezwa za kusuluhisha matatizo yanayotokana na VMG husika. Wakati wa kutekeleza shughuli za mradi, athari na hatari za jamii, hali za makundi ya VMG yaliyoathiriwa na uwezo wa mashirika ya utekelezaji kutoka kiwango cha kitaifa na kaunti, unapaswa kuchunguzwa. iv. Kuchunguza utoshelezaji wa utaratibu wa mashauriano na usaidizi mpana wa VMG zilizoathiriwa katika mradi. Hii itajumuisha utekelezaji wa VMGP, kushughulikia matatizo ya utekelezaji na kurekodi mambo waliyojifunza yanayohusu VMG na utumiaji wa VMGF/VMGP. Benki ya Dunia i. Kuidhinisha VMGF kwa KEMFSED. ii. Kupokea VMGP zote zilizoandaliwa, kuzikagua na Kuziidhinisha au vinginevyo, kabla ya kutekeleza shughuli za KEMFSED. iii. Wakati wa kutekeleza, itathmini na kufuatilia nyanjani, inavyohitajika. iv. Kusaidia katika kuboresha uwezo wa wafanyakazi kadri inavyotakikana.