Kuongeza kasi ya Maendeleo 1 48332 Kuongeza kasi ya Maendeleo: Elimu ya Juu kwa Maendeleo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Muhtasari Kuongeza kasi ya Maendeleo: Elimu ya Juu kwa Maendeleo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara Muhtasari AFTHD (Benki ya Dunia) DECRG (Benki ya Dunia) Oktoba 2008 4 Kuongeza kasi ya Maendeleo Kuhusu hakimiliki, nk. Ripoti ya jumla ya utafiti huu imeandikwa na Shahidi Yusufu, William Saint na Kaoru Nabeshima kwa kutumia tafiti za awali kuhusu elimu ya juu katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tafiti hizo zilihusu: uchunguzi kuhusu namna ya kuongeza aina za bidhaa zinazouzwa nje ya nchi uliofanywa na Vandana Chandra na utafiti kuhusu mahusiano kati ya vyuo vikuu na viwanda uliofanywa na watafiti mbalimbali wa Afrika. Yaw Ansu alitambua haja ya ripoti hii na akatoa msaada kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Jee-Peng Tan ndiye aliyeianzisha kazi na akaisimamia timu iliyoiandaa ripoti. Peter Maselu aliisimamia kazi na kuongoza mashauriano na Jopo la Washauri wa Nje. Petra Righeti alitoa msaada katika kuandaa utafiti na shughuli za kiutawala. Marinella Yadao alisaidia katika kuuchapisha mswada. Matokeo, ufafanuzi na mahitimisho yaliyomo ndani ya ripoti hii ni ya waandishi na, kwa namna yoyote ile, yasihusishwe na Benki ya Dunia, Jumuiya zake wala Bodi yake ya Wakurugenzi au nchi wanazoziwakilisha. Kuongeza kasi ya Maendeleo 5 Dibaji Kuanza tena kwa ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara ni hatua ya kutia moyo. Jambo la muhimu na ambalo ni changamoto kubwa kabisa ni kuyafanya mafanikio haya yawe stahimilivu kwa siku za mbeleni. Ni muhimu kwa kuwa hii ndiyo njia pekee ya kupunguza umaskini na kupiga hatua ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Ni changamoto kwa sababu nchi za Kiafrika bado ziko nyuma sana katika kuyatimiza masharti ya maendeleo stahimilivu na zinakumbwa na vipingamizi vikubwa katika kuleta maendeleo kutokana na kupanda kwa bei ya nishati na chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na vizuizi vya kuliingia soko la kimataifa kwa bidhaa zinazotengenezwa Afrika. Changamoto hii ni lazima ikabiliwe kwani itakuwa ni janga kubwa kwa uchumi kudidimia na kufikia viwango vya miaka ya 1990. Hata hivyo, kuendeleza na hata kuiongeza kasi ya ukuaji wa uchumi ya sasa kunahitaji hatua thabiti za kukuza ushindani wa kiuchumi na kupanua shughuli za kibiashara. Ili kuyafikia malengo haya, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara hazina budi kutumia mtaji na ujuzi zaidi. Na haya mambo mawili yanakamilishana. Eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara linahitaji kuwekeza zaidi katika miundombinu na katika kujenga uwezo wa uzalishaji. Hata hivyo, kuongeza uzalishaji na kufikia viwango vya kiushindani kutategemea ongezeko na ubora wa mtaji watu. Katika ulimwengu wa utandawazi, ufunguo wa mafanikio ya kiuchumi unategemea sana uwezo wa nchi kupata na kutumia ujuzi kwa ufanisi na kwa faida katika sekta za kipaumbele na ambazo zinaweza kukua. Mafanikio hayo yatategemea pia namna nchi inavyoweza kuongeza faida kwa kuiboresha teknolojia. Katika ulimwengu wa sasa, rasilimali ni suala lenye umuhimu wa kwanza lakini kinachoweza kuendeleza mafanikio ya kiuchumi ni uwezo wa kupata na kuutumia ujuzi kikamilifu. Nchi za Afrika zimepiga hatua kubwa katika kuyafikia malengo ya kufuta ujinga na kuongeza udahili katika shule za msingi lakini pia zinajitahidi kuongeza ubora wa elimu inayotolewa. Hatua hizi zinaweka msingi kwa maendeleo ya baadaye. Kwa sasa ni muhimu kuchukua hatua za haraka ili kupata ujuzi na utaalamu wa hali ya juu ambao utaziwezesha nchi za Afrika kuongeza nafasi yake katika shughuli za kiuchumi na hatimaye kuweza kujenga viwanda vipya na kutoa huduma mpya. 6 Kuongeza kasi ya Maendeleo Toleo hili linaonyesha kwa wazi haja ya kukuza ujuzi zaidi kwa kutilia mkazo elimu ya sekondari lakini pia kuipa umuhimu mkubwa zaidi elimu ya juu kwani pamoja na kuongeza udahili katika elimu ya juu, bado idadi ya wahitimu ni ndogo mno. Vile vile ubora wa elimu bado ni duni sana pamoja na jitihada zilizofanywa kuiboresha. Hata hivyo ungalipo uwezekano wa kuiboresha elimu zaidi; na hii itaharakishwa zaidi kwa kuwepo kwa rasilimali na fursa zinazotokana na maendeleo ya kiuchumi. Kitabu hiki ambacho kimekuja kwa wakati muafaka kimejikita katika kusisitiza haja ya kuchukua hatua za haraka katika kujenga msingi wa maendeleo yanayotegemea elimu na sera ambazo nchi za Afrika zinaweza kuzifuata katika kukuza ujuzi katika elimu ya juu. Ni matumaini yangu kuwa chapisho hili litawaleta pamoja wadau wote husika katika ngazi za kitaifa na kikanda katika Afrika na kati ya nchi za Kiafrika na wadau wengine wa maendeleo ili kuibua mjadala mahususi kuhusu umuhimu wa maboresho, kukabiliana changamoto na uwekezaji katika elimu. Hii itaziwezesha nchi husika kupata ujuzi na utaalamu wa juu ili kuwa na ushindani kiuchumi katika dunia hii ya utandawazi. Ni dhahiri kuwa mageuzi yoyote yale yatategemea mazingira ya kila nchi katika kuamua muundo na mfumo wake. Na katika mchakato mzima wa mageuzi hayo, kutakuwa na ugumu katika kufanya baadhi ya mabadiliko na kutahitajika ustahimilivu katika kuyafikia malengo. Ni muhimu kwa jamii ya wadau wa maendeleo kuisaidia Afrika katika mchakato kama huu. Msaada huu utahusisha ushirikiano kupitia wakala mbambali na kuunganisha jitihada kwa kujifunza kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwingineko duniani. Hii itategemea pia uongozi katika nchi husika. Ni kupitia jitihada ya pamoja tu ndipo Afrika itaweza kuyafikia malengo yake kijamii na kiuchumi. Yawu Ansu Mkurugenzi, Maendeleo ya Jamii, Kanda ya Afrika. Kuongeza kasi ya Maendeleo 7 1. Utangulizi Katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Pato la ndani (GDP) limekuwa kwa kasi na kufikia zaidi ya wastani wa asilimia 6.0 kwa kipindi cha 2002-2007. Hatua hii kubwa ya maendeleo ya kiuchumi imekuwa ni faraja kubwa baada ya zaidi ya miongo miwili ya kudorora kwa uchumi. Haya ni matokeo ya kutengemaa kwa sera za kiuchumi, kuboreka kwa soko na kupungua kwa vizuizi vya kibiashara lakini kubwa zaidi ni kutokana na ongezeko la mahitaji ya mazao yanayotokana na maliasili zilizopo katika eneo hili. Ili ukuaji huu wa uchumi uendelee na kufikia viwango vya juu zaidi na vilivyo stahimilivu katika nchi nyingi zaidi za Afrika, uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu utahitajika katika mtaji vitu na mtaji watu. Ripoti hii inaonyesha haja kubwa kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kujijengea uwezo ili kuwe na viwanda vitakavyozalisha ajira zaidi, viwanda vinavyotegemeana na hatimaye uzalishaji wa aina nyingi zaidi za bidhaa za kuuza nje ya nchi. Uwezo huu unaweza kujengwa kutokana na uwekezaji katika mali vitu kama vile miundombinu na vifaa vya uzalishaji mali na pia katika taasisi na mtaji watu. Katika ripoti hii, tunasisitiza mtaji watu kwani ndio msingi mkuu wa kuwepo kwa mfumo wa viwanda unaochochea ukuaji wa uchumi. Uwekezaji katika mtaji vitu na katika taasisi ni vikamilisho muhimu vya rasilimali watu; kwani rasilimali hii haitatumiwa vizuri iwapo itakosa ujuzi wa kiufundi na kiuongozi. Hata hivyo uwekezaji katika mtaji vitu na taasisi hautatekelezeka iwapo rasilimali watu ni pungufu au haina ubora unaotakiwa. Umuhimu mkubwa wa mtaji watu unatokana na haja ya kukua kiteknolojia ili kuwa na shughuli mbalimbali zinazohusu ujuzi na utafiti na ambazo zinalenga kuyafikia matarajio ya muda mrefu. Shughuli za aina hii zinaweza kuleta faida zaidi na haziathiriwi na shinikizo la ushindani. Zipo sababu nyingine zinazoonyesha umuhimu wa rasilimali watu katika mkakati wa kukuza uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara. Iwapo mtaji watu ingetumiwa vizuri, ingewezesha uchumi wa Afrika kuongeza tija na faida kwa kutumia kiasi kidogo cha mtaji vitu. Zaidi ya hayo, nchi za Afrika zitaweza kukabiliana na changamoto kubwa za magonjwa, ukuaji wa miji na idadi ya vijana, na mabadiliko ya hali ya hewa iwapo zitatumia maarifa na kufanya maamuzi sahihi. Katika Afrika, idadi ya mtaji watu yenye elimu ya sekondari na vyuo bado ni ndogo na yenye 8 Kuongeza kasi ya Maendeleo ubora unaotofautiana sawa. Katika baadhi ya nchi za Afrika, ukuzaji wa ujuzi unaathiriwa na vifo vinavyotokana na magonjwa ya kuambukiza na vilele kwa watu wenye vipaji zaidi kuzihama nchi. Ni kwa kuongeza uwekezaji katika mtaji watu ndipo eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara litaweza kuyafikia maendeleo ya kiuchumi yaliyo stahimilivu ambayo yanahitajika kuongeza ajira kwa idadi ya watu inayoongezeka, kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia na kupunguza pengo la kiuchumi kati yake na maeneo mengine. Kwa muda mrefu, Benki ya Dunia imekuwa mstari wa mbele katika kuikuza elimu na inaendelea kulipa umuhimu Lengo la Maendeleo la Milenia la elimu ya msingi kwa wote ambalo ni la muhimu sana kwa nchi zinazoendelea. Hata hivyo kutokana na sababu zilizotajwa hapo juu na kutokana na mwenendo wa sasa wa kiteknolojia, iwapo elimu ya juu itapuuzwa, malengo ya muda mrefu ya ukuaji wa uchumi hayatafikiwa na pia kasi ya kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia hayatafikiwa; kwani mengi ya malengo hayo yanahitaji mafunzo ya elimu ya juu ili kuyafikia. Katika ripoti hii, tunakubaliana na umuhimu wa elimu ya msingi na sekondari katika kuijenga nguvukazi ya uzalishaji na kama msingi wa ubora katika elimu ya juu. Sambamba na hilo, ripoti hii inalenga kuwaelimisha wana mijadala na watungaji wa sera wakati huu ambapo nchi za Afrika zinaangalia namna ya kufanya maboresho yanayohitajika ili kujenga mifumo ya elimu ya juu inayoendana na changamoto zinazokabiliana nazo katika uchumi wa utandawazi. Mtazamo wa maendeleo unajikita katika kuongeza ujuzi unaonekana kuzivutia nchi nyingi za Afrika. Inawezekana kuwa ndiyo njia pekee kuelekea kwenye maendeleo stahimilivu na yenye uwazi zaidi. Ingawa kuna haja kubwa ya kuongeza udahili katika elimu ya juu, ni lazima kuwe na uwiano na haja ya kuwa na elimu na utafiti vinavyoendana na hali halisi. Ni muhimu vile vile kuhamasisha ukuzaji wa stadi za kiufundi na tafiti zinazoweza kutumika moja kwa moja ili kujenga viwanda vyenye ushindani. Hata hivyo, ongezeko kubwa na la haraka la udahili ambalo limejitokeza miaka ya karibuni limeshusha ubora wa elimu na linaharibu mchango wa elimu ya juu katika maendeleo. Mfumo wa zamani wa elimu ya juu katika taasisi za umma haujaweza kuzisaidia taasisi hizo kumudu ongezeko la udahili kwa namna ambayo inaweza kudumisha ubora wa elimu na kuwa na mfumo stahimilivu wa Kuongeza kasi ya Maendeleo 9 kuzimudu gharama zake. Hiki ndicho kizingiti kikubwa kwa mataifa ambayo yanataka kujiunga na uchumi unaotegemea ujuzi. Kimsingi, vyuo vikuu binafsi, taasisi za ufundi, vyuo vya kijamii vya kutwa, na programu za elimu kwa masafa vingeweza kutoa fursa zenye gharama nafuu zaidi ili kuendelea kuongeza udahili. Hii ni kwa sababu taasisi za umma huchukua muda mrefu zaidi kujiimarisha ili hatimaye vijikite kwenye kuboresha viwango vya elimu, uwezo wa kiutafiti, elimu kwenye ngazi za uzamili na uzamivu. Ili ongezeko la udahili katika elimu ya juu liwe stahimilivu, mifumo ya zamani ya utoaji elimu ambapo wanafunzi wanaishi chuoni na kukutana na walimu wao madarasani itabidi ubadilishwe au usaidiwe na mifumo mingine mbadala. II. Ni kwa nini Elimu ya Juu yenye Tija ni Muhimu kwa Maendeleo? Tafiti nyingi za hivi karibuni zimekuwa na ushawishi katika kuonyesha uhusiano kati ya kuwepo kwa mtaji vitu na vigezo vya jumla vya uzalishaji (vigezo ambavyo kwa kawaida hutumika kupima uwezo wa kiteknolojia) na maendeleo. Mambo haya mawili yanahusiana. Rasilimali huchangia moja kwa moja kwenye maendeleo kupitia mabadiliko ya kiteknolojia ambayo huongeza uzalishaji. Na kwa sababu mabadiliko ya kiteknolojia yanahusiana sana na ujuzi, mtaji watu ni kikamilisho cha ujenzi wa uwezo wa uzalishaji. Rasilimali - watu huathiri maendeleo kwa njia mbalimbali zikiwemo kuongeza ufanisi katika kugawa rasilimali nyingine, usimamizi, utumiaji na utunzaji wa rasilimali hizo. Haya huweza kufanyika kwa njia ya ujasiriamali na ubunifu ambavyo huongeza uzalishaji, hufungua fursa mpya za uwekezaji na kuongeza ushindani kwa bidhaa zinazouzwa nje. Kuenea kwa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kunaongeza zaidi mahitaji ya ujuzi na hasa ule wa viwango vya juu. Kwa kuongeza viwango na ubora wa elimu, nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zinaweza kuhimiza ubunifu, kuongeza aina za bidhaa na huduma, kuongeza faida itakanayo na rasilimali na kuwa na tija zaidi katika ugawaji na usimamizi wa rasilimali. Mwelekeo wa maendeleo unaojikita kwenye ujuzi unaweza kutoa fursa ya kuongeza thamani ya pato la ndani kwa nchi zenye rasilimali na zisizo na rasilimali ili kukabiliana na ushindani toka nchi za Asia ya Kusini na Mashariki. 10 Kuongeza kasi ya Maendeleo Kuna sababu mbalimbali za kutoa kipaumbele kwenye ubora kuliko kiasi katika elimu ya juu: • Ubora unahusiana kwa karibu zaidi na maendeleo. Wafanyakazi wenye ufahamu mkubwa kiakili, kiufundi, kimawasiliano na kimahusiano, wanakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuielewa teknolojia, kujipanua zaidi kiufahamu, kufanya kazi katika makundi, na kufanya maamuzi yenye ufanisi yanayojenga uwezo wa kiteknolojia kwa ajili ya kuwa na ushindani na ambayo ni msingi wa ubunifu katika fani kama vile uhandisi na sayansi za viumbe hai. Uwezo kama huo utalifanya eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikia kiwango cha juu cha maendeleo ambacho kitarahisisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika maeneo ya kupunguza umasikini, usalama wa chakula, elimu na afya. • Iwapo vyuo vya elimu ya juu vitajengewa uwezo wa kutoa elimu bora na kuendesha tafiti zinazoweza kutumika moja kwa moja vinaweza kujenga mahusiano ya pande mbalimbali na viwanda na kuhamasisha maendeleo yanayojikita kwenye ujuzi kupitia njia mbalimbali na za uhakika. • Elimu bora inaweza kupunguza ukosefu wa ajira kwa wahitimu na kuwawezesha kuendelea kujisomea maisha yao yote. III. Uongezekanaji wa Vibadala, Changamoto, na Majibu yaliojitokeza. Mazingira ya kibiashara yenye ushindani zaidi, mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia, uzalishaji na uwezo wa kutoa huduma wa nchi za kusini na mashariki mwa Asia vinachangia nchi za Kiafrika kuchagua au kuchanganya vibadala vifuatavyo: • Kufanikisha modeli asilia za maendeleo kwa kukuza soko lao dogo la kimataifa la hisa katika viwanda vilivyosanifiwa na mazao ya kilimo na viwandani, ambapo ongozeko la thamani kwa mzalishaji linaweza kuwa dogo, ushindani mkali, kuendelea kuishi kunategemea sana matumizi ya (maeneo ya) nyanda za chini, na gharama zenye kuridhisha, na kwa nyongeza, sheria madhubuti za mazingira pamoja na ushiriki katika mkufu thamani wa kiulimwengu. Kuongeza kasi ya Maendeleo 11 • Kupanua biashara kuelekea kusiko na hamaki ya kugombea masoko yafaayo kwa bidhaa za wazalishaji wadogo na wakati au mazao ya kilimo, kutafuta uwezekano wa kiteknolojia ambao haujawahi kutumiwa, na uvumbuzi wenye lengo kuingia katika soko jipya kama vile biofueli. • Kupata mahali pa salama katika soko la huduma zenye kuuzika- hususani huduma zilizowezeshwa za IT. • Kuendeleza mkufu thamani wa mali-asili, kwa kuchakata zaidi mambo haya kiasili na kutumia mahusiano ya nyuma kwa kujenga uhandisi au viwanda vinavyotoa malighafi kwa sekta ya madini. • Kuanza kupata uwezo mpya au ulioboreshwa wa kiteknolojia kwa gharama nafuu-kwa juhudi zaidi ili kuyafanya maarifa yalipo kuendana kabisa na eneo hili. • Udhibiti makini wa maliasili ili kuongeza faida, kuwa hadhiri kwamba maswala ya mazingira yatakuwa muhimu sana na magumu zaidi kuyaelezea kama maswala ya ongezeko la watu na hali ya hewa havitapewa kipaumbele. Kwa maeneo ya nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, umuhimu wa kuhamia kwenye njia anuai za ukuaji umetiwa nguvu na: • Mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kubwa katika upatikanaji wa maji, kilimo, na sekta ya utalii. • Misukumo inayosababishwa na UKIMWI na magonjwa mengine ambayo huathiri uwiano wa wanofanya kazi na wale wasiofanya kazi, kuzaliwa watoto, tija ya nguvukazi, undikishaji watoto elimu ya msingi, mahudhurio shuleni, idadi ya watoto ya yatima, lishe ya watoto wachanga, na sababu nyinginezo. • Wasiwasi unaotokana na ongezeko la watu na jumla ya nguvukazi, uhamiaji kwenda mijini, na �ongezeko kubwa la vijana� • Uchumi usioimara uliosababishwa na mgawanyo wa mapato usiosawa • Kuachwa nyuma katika kutumia teknolojia mpya za kilimo ambazo zingesaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza ulegelege wa kushughulikia wadudu waharibifu na ukame. • Matatizo katika kupanga na kuanzisha miradi, pamoja na kurekebisha na kutunza miundo-mbinu. 12 Kuongeza kasi ya Maendeleo • Kuhama kwa wasomi kwenda ng’ambo na idadi kubwa ya vifo vya wasomi kutokana na UKIMWI, ambao umezisha upungufu wa stadi. • Asasi miundo-mbinu zilizoduni, ambazo zinacchangia mazingira mabovu ya kibiashara, kutoendelea kitaaluma, kuporomoka kwa asasi za elimu ya juu, na matatizo ya kudumu ya kijamii. Viwango vikubwa vya ukuuaji vitahitaji ongozeko la utumiaji bora wa maliasili na vichocheo zalishi vinavyotokana na maendeleo ya teknolojia. Kuharakisha ukuaji wa uchumi kunakotazamwa kwa mtazamo wa ugavi, kunahitaji yafuatayo: • Ongezeko la haraka katika ufanisi wa ugawanyaji unaochangiwa na wakala wa umma, mfumo wa kifedha na sekta ya biashara. • Ufanisi bora zaidi katika matumizi ya mali mtaji ( miundo-mbinu na viwanda), na juhudi endelevu za kuutunza. • Maendeleo imara katika uwezo wa kutambua na kupata teknolojia husika, kuongeza mapato, na kuilekeza teknolojia kwenye malengo kama vile: kuzalisha bidhaa zenye soko, kuboresha huduma za jamii, na kuhifadhi nishati na maji. • Kuwa na stadi nyingi na za kina za uongozi na usimamizi na uzoefu ili kusaidia uanzishaji wa viwanda na uhusiano wa kiuchumi wa kimataifa na ili kuendana na mwelekeo wa ugatuzi wa madaraka na kukuwa kwa miji. Haya yote yanahitaji ongezeko la uiwiano wa wafanya-kazi wenye stadi na ufundi na mtaji, katika hatua za mwanzo za maendeleo. Wafanya-kazi wajuzi na waliobebea sio tu wanatoa elimu ya ufundi na kusaidia uvumbuzi, pia wanadhima kama wagawanyaji wa maliasili, waunganishi na warekebishaji ambao wanawezakutambua na kutumia uwezekano wa kiteknoloji. Pale ambapo maliasili imewekezwa, uchaguzi unaofanywa na watoa maamuzi wa umma na binaafsi ni muhimu: ukadadiriaji wa hatari, teknolojia zilizotumika, usimamizi wa uzalishaji, uongezaji na utunzaji mali, kitega uchumi cha T&D, motisha kwenye kuvumbua, na kuifanya teknolojia mpya iwe ya kibiashara. Ubora wa idadi hii kubwa ya mawazo kwa kiasi kikubwa huamuliwa na jinsi walivyoelimishwa vizuri hao watoa Kuongeza kasi ya Maendeleo 13 mawazo. Hii ni muhimu kwa matokeo mazuri kama malighafi rahisi ya mtaji-watu katika mchakato wa uzalishaji. Hizi kazi ugawanyaji na kuzuia hatari, pamoja na mambo mbalimbali na mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa taasisi nyingi mbalimbali katika kuinua ubora mawazo, ni vijazilizi muhimu katika shughuli ya uvumbuzi. Kwa pamoja husaidia kuongeza mchango wa taaluma katika utendaji wa kiuchumi. Bila kujali kibadala kipi hapo juu kimechaguliwa katika kuinua uchumi au ni kwa jinsi gani vizuizi vya ugavi vimezungumzwa, Mataifa ya Kiafrika yatahitaji kuzalisha kundi la wasomi wenye ubora zaidi kuanzia shahada ya kwanza na kuendelea, na kuwazalisha hususani katika fani ambazo zitaendana na mbinu zilizochaguliwa na nchi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi. IV. Kwa nini elimu ya juu haitoi mchango kamilifu katika kukuza uchumi? Pamoja na kuongezeka kukubwa kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu, vyuo vyingi vikuu vya Kiafrika havitoi wahitimu wengi, na wengi wao hawana stadi zinazohitajiwa kuinua maendeleo ya kiuchumi ya taifa katika karne ya 21. Kwa hiyo kizuizi kimoja kikubwa katika kukuza uchumi ni maamuzi yanayofanywa na vyombo vinavyotunga sera na taasisi zenye kujenga uwezo ambazo zinajukumu la maendeleo ya juu ya maliasili watu. Kwa namna gani juhudi za vyuo hivyo zimekosa mwelekeo? Sababu zifuatazo zinaweza kuchangia. Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, uingiaji wa wanafunzi katika vyuo vikuu uliongezeka kwa haraka zaidi kuliko bajeti iliyotengwa kwa elimu ya juu. Kwa kweli uingiaji ulikuwa mara tatu katika miaka ya 1991 na 2005, imeongezeka katika miongoni mwa viwango vikubwa kabisa duniani (asilimia 8.7). lakini wakati huo huo fedha zilizotengwa ambazo ni wastani wa dola za Kimarekani 6,800 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka zimeshuka hadi dola za Kimarekani 981 katika mwaka 2005 kwa nchi 33 za Kiafrika zenye kipato kidogo. Kadri idadi ya wanafunzi inavyoongezeka, fedha zinazopatikana kwa kila mwanafunzi zinapungua. Ubora na uhalisia wa elimu vyote huathiriwa na hali hiyo. Kukosekana kwa umakini wa jumla wa kuhakiki ubora, mwitikio wa soko la ajira, ukichanganya maswala ya 14 Kuongeza kasi ya Maendeleo kiuongozi na ukosefu wa uwajibikaji, inamaanisha kuwa haya maendeleo hasi yalikuwa hayajawahi kuzungumzwa. Ongezeko la haraka katika uandikishaji wa wanafunzi umesababisha ukosefu wa uwiano katika masomo ya gharama nafuu na kumega (kutumia) fedha zinazotolewa kwa ajili ya utafiti ili kuwasomesha wanafunzi wengi zaidi. Mwaka wa 2004, ni asilimia 28 tu ya wanafunzi waliosajiliwa katika fani ya sayansi na teknolojia. Aidha, shughuli za tafiti zilipungua kwa kuwa Afrika ilitenga asilimia 0.3 ya pato la taifa kama bajeti ya utafiti na maendeleo, jambo ambalo lilisababisha wataalamu wa tafiti kushindwa. Idadi ya wahitimu ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wote wanaosajiliwa na hivyo kupunguza idadi ya wahadhiri na watafiti wa baadaye wakati ambapo idadi yao ingetakiwa kuongezeka maradufu. Mwelekeo huu unazidisha ugumu katika utoaji wa maarifa husika na ujuzi unaotakiwa kwa ajili ya mataifa ya Kiafrika katika kuinua ushindani na kuendeleza ukuaji. Taasisi za elimu ya juu zinakosa mamlaka ya kutoa maamuzi na kukubali kuendana na mabadiliko katika soko la ajira. Mara kwa mara taasisi hizi zimekuwa zikiandaa upya mitaala na kuanzisha kozi mpya za kusoma bila uwekezaji wa rasilimali toshelevu kutoka kwa mwajiri katika ufanisi wa wahitimu katika soko la ajira, hali inayosababisha pengo baina ya ugavi na mahitaji katika viwango vya juu vya ujuzi. Tofauti baina ya elimu inayotolewa na kiwango kinachotakiwa katika soko la ajira huchangia kwa kiasi kikubwa katika ukosefu wa ajira kwa wahitimu, inayozidi asilimia 20 katika nchi 9 kati ya 23 zenye data za soko la ajira lililopo. Ufadhili duni wa tafiti na kupuuza maendeleo ya kitaalamu kumeibua mgogoro katika kupata watumishi wanataaluma pale walimu wanapohitajika sana kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi. Pamoja na mishahara duni, mzigo mkubwa wa kufundisha unaosababishwa na ukosefu wa uwiano sahihi wa mwalimu kwa mwanafunzi, ukosefu wa ujuzi wa utawala wa rasilimali watu, na ukosefu wa nafasi za utafiti husababisha watumishi kudumu kazini na hivyo zoezi la kuajili kuendelea kuwa gumu. Mara kwa mara, viwango vya nafasi wazi za kazi kwa watumishi vyuoni ni kati ya asilimia 25 na 50 na mara nyingi ni za sehemu za fani za uhandisi, sayansi, na biashara zimekuwa zikihusishwa na uvumbuzi na ukuaji wa uchumi. Taasisi za elimu ya juu za Afrika zimekuwa zikizembea katika kusaini msaada wa “misheni ya tatu� kwa ajili ya uchumi ambao umewaimarisha wengine katika sehemu nyingine. Uchumi wa kiushindani wa utandawazi Kuongeza kasi ya Maendeleo 15 na maarifa umebadilisha mitazamo ya awali juu ya jukumu la taasisi za elimu ya juu na kufasili “ufundishaji� na “utafiti� kupanuka kwa haraka kwa maarifa na teknolojia kumepunguza muda wa matumizi ya maarifa na kupelekea uhitaji wa kuendeleza watumishi na elimu isokikomo –kupanua fasili ya “mwanafunzi�ili kujumuisha idadi kubwa ya watu wazima. Kadiri upatikanaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano unavyoongezeka Kunaufanya upatikanaji wa maarifa kuzagaa, mafunzo ya ana kwa ana yanazidi kukosa umuhimu mkubwa. Hivi sasa utafiti unafanywa katika mifumo ya kiuvumbuzi ya kitaifa iliyounganishwa ambapo dola inakuwa ni muwezeshaji wa kifedha zaidi na sio mtoaji wa fedha moja kwa moja. Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoingia katika vyuo vya elimu ya juu kumetoa msukumo wa mfumo wa utoaji elimu wenye gharama ndogo, uanzishaji wa vyanzo vya mapato vya taasisi, na uwajibikaji wa kitaasisi, ikizingatiwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Msukumo wa mwisho kabisa umeibuka na kuwa kama “dhamiri ya tatu� ambapo mafunzo, utatuzi wa matatizo, na uhamishaji maarifa katika kusaidia uchumi unakuwa ni tafsiri mpya ya huduma kwa jamii. Sekta binafsi ya elimu ya juu inakuwa kwa kasi sana kama suluhisho la kushuka kwa ubora katika sekta ya umma, na njia muafaka ya kukidhi haja ya soko la ajira zenye kuhitaji ujuzi. Tangu 1990 vyuo vikuu, na taasisi za kitaalamu za viwango vya elimu ya juu zinazoendeshwa na watu au taasisi binafsi vimeanzishwa kwa kasi sana kuliko vile vya umma. Wakati vyuo vya umma vimeongezeka takribani toka 100 hadi 200 kati ya miaka ya 1990 na 2007, idadi ya taasisi za elimu ya juu za binafsi zimeongezeka katika kipindi hichohicho toka dazani mbili hadi kufikia takribani 468. Hata hivyo, mifumo ya uwekezaji isiyokuwa na sheria zenye ufanisi, utambulisho rasmi, na uhakika wa ubora, na uhaba wa nyenzo kutokana na mfuko wa fedha za utafiti na uvumbuzi wenye ushindani, vimekwamisha uwezo wa sekta binafsi kushindana na taasisi za umma na kupanua wajibu wao katika kukuza ukuaji na ushindani. Elimu ya juu inatofautiana pia. Mwaka 2004 ilikadiriwa kuwa kulikuwa na vyuo ambavyo sio vyuo vikuu 1,000 katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikilinganishwa na vyuo vikuu 300. utofauti huu umepunguzwa kwa kupandisha hadhi vyuo vya kawaida na vyuo vya ufundi na kuwa vyuo vikuu bila kujaza mapengo yaliyoachwa na vyuo vilivyopandishwa hadhi. Kwa hali hiyo, kutozingatia kwa serikali katika 16 Kuongeza kasi ya Maendeleo kuimarisha na kuboresha vyuo vya ufundi katika inatia mashaka hasa ikizingatiwa kuwa vyuo hivi vitoa mchango mkubwa katika utatuzi wa matatizo yanayohusiana na uchumi wa taifa. Kwa muktadha huu, kugharamia elimu ya juu kumekuwa na matatizo makubwa na changamoto – na ni chanzo cha ubishani katika majukwaa ya kisiasa. Gharama za umma katika nchi nyingi bado hazipelekwi katika maeneo yanayohitaji fedha sana, gharama hizo hazisaidii kutoa nyenzo kwa ajili ya usimamizi mzuri na wenye ubora unaotakiwa, na haina ufanisi katika kusaidia tafiti. Kadiri taasisi za elimu ya juu zinavyoongezeka na uingizaji wa idadi ya wanafunzi unavyozidi kupanda, ugharamiaji bado unaendelea kuwa kikwazo kinachokabiliana na maendeleo ya elimu ya juu ya nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara hapo baadaye. Katika miaka ya hivi karibuni, kuongezeka kwa uchangiaji gharama kwa wanafunzi na wazazi umeongeza chanzo kingine muhimu cha fedha katika mfumo wa elimu ya juu. Katika bara la Afrika, hali hii imetumia utaratibu wa programu zinazoenda pamoja, wanafunzi “wanaojigharamia�, wanaochangia kiasi fulani cha ada, au baadhi ya vitendea kazi “kwa kutumia ada�. Lakini maendeleo ya uchangiaji wa gharama na uzalishaji wa mapato bado ni mdogo sana ili kuziwezesha taasisi hizi kujiwezesha kifedha, kupunguza utegemezi wa kifedha toka serikalini, na kupata rasilimali mara moja moja kwa ajili ya utafiti na uvumbuzi. Ili kutoka hapa kunahitajika mjadala wa kitaifa juu mabadiliko ya kifedha ambao unapaswa kwenda zaidi ya elimu ya juu. Kwa hivi sasa, nchi zilizo kusini mwa jangwa na Sahara zinawekeza wastani wa asilimia 4.5 ya pato la nchi katika elimu kiwango cha juu kulingana na viwango vya kimataifa. Matokeo yake, mataifa haya yanakaribia mwisho wa uwezo wao katika kugharamia maendeleo ya sekta ya elimu. Hali kadhalika, nchi nyingi zinakaribia kufikia kikomo katika kutenga kiasi cha asilimia 20 toka katika bajeti zao za taifa kwa ajili ya elimu ya juu kiasi kinachodaiwa kuwa ni sahihi katika nchi zenye kipato kidogo. Katika ngazi ya taasisi, zimekaribia kufikia kikomo katika uzalishaji wa kipato. Aidha, mapitio ya tafiti za matumizi ya fedha za umma na za jamii katika sekta ya elimu zinadhihirisha kuwa katika nchi nyingi, mgawanyo wa rasilimali za umma kwa misingi ya kiwango cha mapato na michango inayoombwa ya wazazi una upendeleo kwa kiasi fulani. Ili kuyashughulikia masuala haya, kuna haja ya kuzingatia zaidi matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo na kubuni vyanzo vingine ya Kuongeza kasi ya Maendeleo 17 mapato. Kuongezeka kwa viwango vya ufanisi katika utumiaji wa rasilimali utahitaji utashi wa kisiasa, ukubalifu wa kisera, na busara. Kuongeza ufanisi pia kunamaanisha kushughulikia taratibu zilizozoeleka ambazo bado zipo katika nchi nyingi zinazozungumza Kifaransa zinazo na kawaida ya kupewa misaada, na kupinga fursa mbalimbali zinazotolewa kwa wasomi ambazo mara nyingi zinatolewa kwa uficho zinazohusisha fedha nyingi sana zinazotolewa kama msaada. Mkabala sahihi ni ule ambao ungeweka kipaumbele kutoa udhamini wa serikali kwa wanafunzi kusoma taaluma zile zenye umuhimu tu kwa taifa katika siku za usoni. Jitihada nyingi za kufanya mabadiliko ya elimu ya juu zimefanywa katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara katika miaka ya hivi karibuni, lakini matokeo yake bado yameonekana kuwa hafifu. Ili kuokoa umuhimu wa taasisi za kanda kuchangia vilivyo katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi zao na katika kanda kwa ujumla, taasisi za elimu ya juu zitapaswa kujibadilisha kwa umakini mkubwa zenyewe ili ziwe taasisi tofauti za kielimu: zilizounganishwa, zilizotofautishwa, na taasisi zinazokidhi haja zinazolenga katika kuzalisha watu wenye ujuzi unaohitajika na matumizi ya tafiti zinazolenga katika kutatua matatizo. Kama haya yatafanikiwa, hii itaonyesha namna “maendeleo ya vyuo vikuu� vya Kiafrika yanavyopaswa kufikiwa. Baadhi ya utendaji mzuri umeanishwa katika kipengele kinachofuata umewasilishwa katika kusaidia utendajikazi wa serikali. V. Kuifanya Elimu ya Juu kuwa Chachu ya Maendeleo Kadiri nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zinavyojitahidi kupata mafanikio linganishi ya kiuchumi yanayotokana na mikakati ya maendeleo ya rasilimali watu, kila nchi itapaswa kutumia njia yake, mkakati wake wa maendeleo na kujifunza utendaji mzuri toka katika nchi zingine kama mfano. Taasisi za elimu ya juu ni zaidi ya kuwa rasilimali za kimkakati za taifa ambazo zinaweza kuongozwa na kuwezeshwa na sera ya serikali ili kuongeza maslahi ya nchi katika mifumo ya ushindani katika utandawazi. Kwa ufupi, uchumi wa ushindani hivi sasa unategemea kwa kiasi fulani mfumo wa elimu ya juu wenye ushindani. Leo hii, kipindi cha ubinafsi katika taasisi za elimu ya juu kinaanza kupitwa na wakati, kwani serikali na wadau mbalimbali wanazishauri taasisi hizi kufanya kazi kama timu moja ambapo watachangia katika mfumo wa 18 Kuongeza kasi ya Maendeleo uvumbuzi wa taifa ambao utainufaisha nchi kiuchumi. Ili kuweza kufanya hili, taasisi hizi zinapaswa kuzitekeleza sheria zao za kujitegemea, ili ziwe za kijasiriamali, kuzama katika tafiti na kubadilika, zijione kama ni wabia na washiriki, zielewe mahitaji ya mienendo ya soko la ajira, na kuongeza bidii ili ziwe na uwezo wa hali ya juu katika kufundisha na kufanya tafiti. Kwa pamoja, mifumo ya elimu ya juu katika bara la Afrika imekomaa vya kutosha katika miongo miwili iliyopita. Hata hivyo, kwa taasisi mojamoja, mifumo hii bado imetofautiana kwa kiasi kikubwa. Taasisi binafsi zinatoa mchango mkubwa sana katika baadhi ya nchi lakini katika nchi zingine mchango wao ni mdogo mno. Mifumo mingine inasaidia mpango wa utoaji wa masomo baada ya shahada ya kwanza lakini mifumo mingine haifanyi hivyo. Sifa za wafanyakazi, vifaa vya kufundishia, uwezo wa kifedha, na uangalizi wa sera za serikali pia umetofautiana sana. Kutokana na athari za mambo mbalimbali (na kutofautiana katika hali siasa juu ari ya mabadiliko) mtazamo wa jumla juu ya mikakati ya pamoja ya elimu ya juu katika kanda inapoteza thamani katika tondoti za matumizi yake. Ni jambo la msingi kwa serikali, wadau, na wabia katika maendeleo kutafuta kwa pamoja suluhisho pekee la changamoto zinazohusiana na mikakati ya maendeleo ya rasilimali watu pamoja na mikakati ya ukuaji uchumi. Ili kusaidia mambo hayo, utendaji mzuri ufuatao unaweza kusaidia kuharakisha safari ya kuelekea katika mfumo wa elimu ya juu unaofaa. • Kuweka mkakati wa maendeleo ya rasilimali watu ya taifa Elimu ya juu inapokuwa nyenzo muhimu ya ukuaji wa uchumi, serikali pamoja na ukata wa fedha haina njia nyingine zaidi ya kuchagua vipaumbele vichache na kuzitumia fedha chache zilizopo katika kuvishughulikia hivyo vipaumbele vichache vilivyo muhimu. Kwa mfano, ikiwa serikali zinagharamia vyuo vya umma katika mkataba wa makubaliano unaozingatia kiwango cha kufaulu, zinaweza kusaidia kuvielekeza upya kwa kuongeza vichocheo vya uwekezaji, kugharamia tafiti, uhandisi, na teknolojia. Uwezekano mwingine ni kusamehe ada katika baadhi ya taaluma ambazo zina wataalamu wachache sana katika serikali kama vile kufundisha somo la hisabati. Vichocheo kama Kuongeza kasi ya Maendeleo 19 hivyo vinaweza kutumika katika kuhamasisha utoaji elimu katika taasisi zinazomilikiwa na watu binafsi. Mchakato wa kuendeleza mkakati huu sharti uende zaidi ya sekta ya elimu ya juu ili kuiwezesha serikali kuwa na malengo makubwa ya kiuchumi, wawakilishi wa sekta binafsi kuchangia uwezo na viwango vya ujuzi vinavyohitajika katika kuboresha uzalishaji. Mchakato huu ni lazima uhusishe pia tathmini za viongozi wa elimu ya juu zenye uwezo linganishi ndani ya mfumo wa elimu ya juu. Ingawaje zinafanana katika tamaduni za kitaasisi na mfumo wa ndani, taasisi za elimu ya juu zinaisaidia nchi yao kwa usahihi zaidi ikiwa kila taasisi inafanya vizuri katika maeneo yake machache ya kimkakati, kama washiriki wa mfumo wa uvumbuzi wa taifa. Taasisi za elimu ya juu zina uwezo wa kuwa wachangiaji wakuu wa kutoa maarifa kwa taifa kwa kutumia uwezo wao wa kufanya tafiti. Ili kupata uwezo huu, serikali duniani kote zimekuwa zikiweka vipaumbele vya tafiti vya kitaifa, kutengeneza sera saidizi, kuunda taasisi mpya zinazogharamia na kusaidia kuimarisha juhudi za kupanua uwezo wa kufanya tafiti, na kuziunganisha katika mfumo wa uvumbuzi wa kitaifa. Nchi nyingi za Kiafrika zinasaidia taasisi zinazofanya tafiti zinazogharimiwa na umma ambazo zinaweza kuwa nyenzo muhimu katika mfumo wa uvumbuzi wa kitaifa, lakini taasisi nyingi sio imara, hazipewi fedha za kutosha, ziko katika hatari ya kuyumbishwa na matukio ya kisiasa, zinazoyumbishwa sana na mabadiliko katika majukumu ya wizara zinazoshughulikia sayansi na teknolojia. Kunahitajika mikakati madhubuti katika katika kuunganisha sekta mbalimbali na ushirikiano ambao utasaidia kuongeza utumiaji wa maarifa na kuimarisha ushirika kati ya taasisi za elimu ya juu na sekta za uzalishaji. • Mipango ya kugharamia mabadiliko ili kusaidia vichocheo kwa ajili ya kuyafikia malengo ya sera wakati huohuo kujenga uwezo ili taasisi zipange shughuli zao kimkakati. Wajibu wa kugharamia elimu ya juu utaendelea kuwa mgumu katika miaka ijayo kadiri mahitaji ya kijamii yanavyoongezeka. Kila nchi itapaswa kujiwekea utaratibu wa kugharimia ambao utazingatia uwezo wa kiuchumi, uwezo wa kitaasisi, na uwezekano wa kisiasa. Kwa kuwa matumizi ya fedha ya serikali katika elimu na elimu ya juu katika baadhi ya nchi yanaweza kuwa magumu kuongeza viwango vya vilivyopo hivi sasa kama vilivyoelezwa hapo juu, hatuna budi kuongeza viwango vya ada 20 Kuongeza kasi ya Maendeleo katika taasisi za elimu ya juu za umma, na kutoongeza idadi ya wanafunzi ili ibaki idadi iliyopo hivi sasa. Njia zingine ni pamoja na kuandaa kodi maalumu kwa ajili ya kuchangia elimu ya juu na mapato yanayotokana na mikopo ya wanafunzi (utaratibu ambao umeshaanza kutumika katika baadhi ya nchi za Kiafrika); ubia wa umma na watu binafsi ambapo wabia toka katika nchi husika wanadhamini baadhi ya kozi au eneo fulani la utafiti ambalo linaweza kuwanufaisha wao, au kuchangia katika mfuko wa maendeleo; ari kubwa ya ufuatiliaji wa ufanisi, hasa kwa kubadili uelekeo wa misaada ya masomo inayotolewa na nchi za nje isiyo faida ili kuinua ubora wa kiwango cha ufundishaji cha taifa, kujifunza, na kufanya tafiti; kuzidisha hamasa kwa watu au taasisi katika utoaji wa elimu ya juu, na kufanya uchunguzi wa utoaji wa elimu ya juu wenye manufaa unaolingana na gharama kwa kutumia mipango inayoendeshwa kwa TEHAMA, yenye ubunifu, na inayoweza kubadilika. Kabla ya kutekeleza mapendekezo haya, serikali zinashauriwa kushughulikia mabadiliko ya kimfumo na kitaasisi. Jambo hili ni muhimu katika kuhakikisha kwamba rasilimali zilizopo na zijazo zinatumiwa kwa ufanisi mkubwa na zinaelekea kutoa matokeo yanayotegemewa ikiwa ni kigezo cha kupanua wigo wa kuchangia gharama za elimu. Sehemu ya wajibu wa serikali katika kufuatilia mabadiliko ya kimfumo ni kuvutia wawekezaji wa ndani na wa nje kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji. • Kutoa uhuru wa kitaasisi, unaotegemea mifumo ya kiuwajibikaji, ili kuongeza fursa kwa ajili ya utofauti wa kimfumo na uvumbuzi wa kitaasisi. Muunganiko wa uhuru, uwajibikaji, na ushindani katika mifumo ya elimu ya juu ni muhimu ili kuongeza uwezo wa kujifunza wa wanafunzi: Uhuru katika kutoa maamuzi unaweza kuwahakikishia wasimamizi wa taasisi na bodi za watawala wanaweza kuamua kufanya chochote ili kukuza mafanikio ya taasisi; mfumo wa uwajibikaji unaweza kuonyesha na kuzituza taasisi zinazofanya vizuri; na ushindani na uchaguzi katika taasisi na programu za elimu zinaweza kuchochea nia ya mwanafunzi katika kujitengenezea vichocheo vya utendaji kazi. Katika mataifa mengi ya Kiafrika, moja au zaidi ya vipengele hivi muhimu vinaweza kutofikiwa au kutokuwepo kabisa. Kuongeza kasi ya Maendeleo 21 Uelekeo katika uhuru na uwajibikaji unaathiri sio tu utawala wa elimu ya juu, bali pia inaathiri usimamizi wake. Katika kiwango cha mfumo wa elimu ya juu, kuibuka kwa “bodi zinazosaidia mifumo� katika nchi nyingi za Kiafrika ni mafanikio ya ujengaji uwezo. Hii inahusisha vyombo kuongoza au kusimamia, bodi zinazosimamia ubora, na programu zinazosaidia fedha kwa wanafunzi. Katika kiwango cha taasisi, vyuo vikuu vingi vya umma vya Kiafrika hivi sasa vimekua na kuwa taasisi kubwa. Hali hii imesababisha ongezeko la “kitu kama biashara� kama njia ya usimamizi katika taasisi, ikijumuisha kupanga mikakati, na usimamizi wa utendaji. Uelekeo huu unatoa thamani ya juu inayoongezeka kwa uwezo wa uongozi na usimamizi katika taasisi za elimu ya juu. • Kuhamasisha utofauti katika ufundishaji, na mikabala ya kufundishia ambayo inawezesha ubobezi wa kitaasisi. Huenda kazi ngumu inayozikabili taasisi za elimu ya juu zinapobadilika kuelekea katika utamaduni unaopendelea zaidi katika uvumbuzi ni kubadilisha taratibu za ufundishaji. Mabadiliko yanayohitajika yanafahamika barabara: mitazamo inayohusisha taaluma mbalimbali badala ya ile inayohusisha taaluma moja; uwezo wa kubadilika katika kujifunza; kufanya kazi katika vikundi badala ya mihadhara; kutatua matatizo badala ya kukariri dhana mbalimbali, kujifunza kwa vitendo (safari za uwandani, kufanya kazi, mafunzo katika uangalizi) kama kijalizo cha nadharia; tathmini za mafunzo kupitia kazi za mradi zinazodhihirisha uwezo badala ya mitihani ya maswali ya kuchagua; stadi za mawasiliano; na ujuzi wa kompyuta. Inapotokea kwamba taasisi mbalimbali za elimu ya juu zinafahamika kwa umma kwa juhudi zao katika kufundisha na katika mikabala yao mbalimbali ya kufundishia, zinapunguza hali ya kuwa na vitu vya namna moja, badala yake vinajipanua zaidi, vinakuwa na uwezo zaidi wa kubadilika, na kupanua wigo wa uchaguzi wa masomo kwa wanafunzi na pia kwa waajiriwa wao watarajiwa. Mchakato huu wa kuongeza utoaji wa maarifa maalum ya kitaasisi unaboresha mfumo mzima wa ufanisi katika kukidhi haja tofauti za wanafunzi na mahitaji ya kitaifa. Hii hutokea katika njia mbalimbali. Kwanza kabisa, inakidhi mahitaji ya kazi katika soko kwa kutoa mlolongo wa utoaji wa maarifa maalumu yanaohitajika kwa ajili ya 22 Kuongeza kasi ya Maendeleo maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Pili, inaongeza ufanisi wa kila taasisi kwa kuihamasisha ibobee katika maarifa yale inayoweza kukifanyia kazi barabara. Tatu, mfumo wenye utofauti unarahisisha namna ya kuwafikia wanafunzi wenye historia tofauti kielimu na uwezo kwa kupanua wigo wa uchaguzi na maelekezo ya mbinu ya ufundishaji. Mwisho, inasaidia mabadiliko ya kijamii kwa kutoa vigezo mbalimbali vya kumuwezesha mwanafunzi kuingia katika taasisi za elimu ya juu na chaguzi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanikiwa kuendelea katika viwango vingine vya elimu ya juu. • Kukuza maendeleo ya programu za masomo ya shahada ya juu kitaifa na kikanda; kama njia bora ya kuongeza idadi ya wanataaluma na kujenga uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali. Jitihada za R&D za Kitaifa zinaonekana kuwa endelevu zaidi ikiwa zinajengwa katika programu za masomo ya shahada ya juu kitaifa na mitandao ya kitaalamu inayowazunguka. Utaratibu wa kugharamia kwa ushindani ni njia bora ya kuendeleza misingi imara ya programu za ufundishaji na utafiti zinazotakiwa katika masomo baada ya shahada ya juu. Kama mwongozo wa jumla, wanafunzi wa shahada ya juu wanapaswa kufundishwa ndani ya nchi pale inapowezekana. Baada ya kujiimarisha katika hili, kuna uwezekano sasa wa kuanza kuchukua mafunzo toka katika nchi zingine zenye mifumo bora ya elimu ya juu, hasa zile zenye zilizobobea na zenye ujuzi wa hali ya juu, kutumia njia inayoweza kupunguza gharama kadiri iwezekanavyo. Mitandano ya kikanda na kanda ndogo mara nyingi inafanya kazi kama ‘daraja’ kati ya mifumo ya elimu ya juu na taasisi na uzoefu, utendaji bora, na uvumbuzi uliopo katika kiwango cha kimataifa. Mitandao hiyo inatumia rasilimali chache kwa ufanisi zaidi. Njia ya ushirika katika utafiti kikanda, ikiunganishwa na ubia imara wa kimataifa, inaweza kuwa njia bora katika kushughulikia changamoto za maendeleo ya Afrika, kama ilivyojitokeza katika baadhi ya nchi. Mara nyingi njia bora ya kuanzisha kituo cha kikanda chenye uwezo wa hali ya juu inaweza kufikiwa kwa kupitia maendeleo ya taasisi imara za kitaifa ambazo zinajenga hatua kwa hatua mazingira yanayovutia kikanda kadiri sifa zake zinavyokua. Imethibitika kuwa ni vigumu kuanzisha na kuendeleza programu za shahada ya juu za kikanda zinazojitegemea Kuongeza kasi ya Maendeleo 23 kama njia mbadala. Zinaweza kuwa hatari kisiasa, kuligawa taifa, na zilizo na gharama kubwa. Hata ikiwa wafadhili wamedhamini programu za mafunzo za kanda kwa muongo mmoja au zaidi, viongozi wa siasa wa kitaifa hawajawa na ari ya kuendeleza programu pale misaada ya kimaendeleo inapokwisha. Hali hii inaonesha kwamba umiliki wa ndani unapaswa kufanyiwa kazi toka katika hatua za kupanga na kuendelea. • Kutafuta njia mbadala ya utoaji elimu ya juu wenye gharama ndogo Taratibu za kutoa elimu za vyuo ana kwa ana zina gharama kubwa na zinazuia uwezo wa nchi zinazoendelea kupanua wigo wa kuingiza idadi kubwa ya wanafunzi vyuoni. Serikali na jamii kwa pamoja zinakaribia kufikia kikomo cha uwezo wa kuchangia katika kugharimia elimu ya juu. Mbadala wake, njia za utoaji elimu zenye gharama ndogo zinahitajika kama upatikanaji wa elimu unaongezeka katika mfumo wa elimu isiyo na mwisho, matumizi ya TEHAMA katika elimu, elimu kwa njia ya mtandao, kozi zenye vyanzo bayana, mafunzo binafsi yanayofanyika hatua kwa hatua, na elimu yenye misingi imara. Utafiti huu umelenga kudhihirisha sababu zinazoifanya mifumo ya elimu ya juu katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zilingane barabara na maendeleo ya kiuchumi ya kitaifa na mikakati ya kupunguza umasikini, na umeonyesha manufaa ambayo yanaelekea kuhusishwa na mabadiliko hayo ya kimtazamo. Utafiti huu unapendekeza kwamba muda wa kuyatekeleza haya ni sasa, na fursa ya kupata mafanikio ya mikakati hiyo imo ndani ya kipindi cha takribani miaka kumi ijayo. Kwa kufanya hivyo, utafiti huu utakuwa umetambua kwamba serikali na taasisi binafsi za elimu ya juu zimefanya mabadiliko makubwa katika mazingira magumu katika muongo uliopita, na kwamba suala la maboresho ya aina zote katika elimu ya juu katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ni lenye kuendelea. Hata hivyo, umuhimu wa hali ya juu na jitihada kubwa zinapaswa kushughulikiwa katika suala hili mara moja. Athari za kutochukua hatua kikamilifu zinaweza kuwa: kuongezeka kwa wanafunzi katika taasisi dhaifu, wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wasio na ujuzi wa kazi wa kutosha; kutomalizika kwa haja ya kugharamia bajeti za umma katika mambo mengi yasiyoleta tija; kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, kutumia siasa kwa hali ya juu katika kushughulikia masuala yanayohusu elimu na sera za ajira; na 24 Kuongeza kasi ya Maendeleo uwezekano wa machafuko ya kisiasa. Kutafakari kwa kina mambo haya kunazipa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na raia wake muda wa kutosha wa kuchukua hatua zinazofaa. VI. Mkabala wa Benki ya Dunia: Kuoanisha Mikakati na Mahitaji ya Nchi. Elimu ya juu ni kipengele muhimu katika mkakati wa maendeleo ya Benki. Ijapokuwa katika miaka iliyopita Benki ilisaidia sekta ya elimu kwa ari kubwa kwa madhumuni ya kuweza kufikia malengo ya milenia ifikapo mwaka 2015, elimu ya juu wakati wote imekuwa ni sehemu ya agenda yake. Elimu ya Juu katika nchi zinazoendelea: Matatizo na mafanikio (2000) na Kujenga Uchumi wa maarifa (2002) vinatoa kipimo bora cha elimu ya juu kama nyenzo ya kuondoa umasikini, maendeleo na ushiriki katika uchumi wa maarifa ya dunia. Kwa hakika, mambo hayo yanatupatia kiungo muhimu katika jitihada za Benki kuunga mkono hatua zilizowekwa kwa lengo la kuboresha nafasi ya elimu ya juu katika nchi wanachama wake. Kuanzia mwaka 1990, miradi ya Benki ya Dunia katika elimu ya juu inakadiriwa kufikia asilimia 20 ya fedha zilizo elekezwa kwenye elimu ulimwenguni. Kwa pamoja mjadala wa sera, kazi za uchanganuzi na msaada wa kifedha vimesaidia utekelezaji wa mabadiliko ya kina katika sekta ya elimu ya juu katika nchi mbalimbali kama Argentina, Chile, China, Vietnam, Misri, Tunisia, Ghana na Msumbiji. Kuanzia mwaka 1990 karibu asilimia 19 ya fedha za mkopo toka Benki ya Dunia katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zilielekezwa kwenye elimu ya juu na miradi sita inayofadhiliwa na Benki ya Dunia iliyoelekezwa kwenye elimu ya juu ipo katika utekelezaji katika nchi ya Ethiopia, Mauritania, Uganda, Msumbiji, Bukina-Faso na Tanzania. Zaidi ya hayo, katika nchi 13 Benki inasaidia mabadiliko ya sekta ya elimu ambayo inajumuisha pia elimu ya juu1 muhtasari kuhusu msaada wa Benki ya Dunia kwenye elimu kwa sekta ndogondogo kwa kipindi cha mwaka 1990-2008 unaoneshwa katika kielelezo cha 1 (data kama hizi zipo katika Kiambatisho) 1 Katika nchi za Burkina Faso, Cameroon, Chad, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Namibia, Rwanda, Nigeria, Msumbiji na Mali Kuongeza kasi ya Maendeleo 25 Michango mingine muhimu ni mjadala wa kisera na kazi ya uchanganuzi iliyofanywa na Benki ya dunia kama taasisi inayoshiriki utoaji wa maarifa. Hizi huzisaidia serikali kutafakari machaguo ya mageuzi katika elimu ya juu na kupanga utekelezaji wake. Maeneo makuu yaliyofanyiwa kazi hivi karibuni ni kudhibiti ubora, elimu na mafunzo ya kilimo, teknolojia ya habari na mawasiliano, utoaji wa fedha na utofauti na ufundishaji katika mifumo ya elimu ya juu. Aidha, taarifa ya sifa za nchi (CSRs) inatoa uchanganuzi wa elimu ya juu katika mawanda mapana ya sekta ya elimu, kipaumbele kikiwa katika ongezeko la wanafunzi na ushirikishwaji, ugharamiaji na uwezeshaji, gharama ndogondogo na ufanisi na usawa. Katika miaka miwili iliyopita CSRs imekamilika katika nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Benin, Mali, Mauritania, Sierra Leone na Togo. Kielelezo 1: Mikakati mipya ya elimu katika nchi za Afrika Kusini mwa Jjangwa la Sahara kwa Sekta Ndogondogo MF 90 – 08 (mamilioni ya fedha katika dola za kimarekani) 200 Wastani wa Kimaendeleo Wenye Pande Mbili za Miaka Mitatu (MA) 180 160 (milioni za dola za kimarekani) 140 120 100 80 60 40 20 0 FY90 FY92 FY94 FY96 FY98 FY00 FY02 FY04 FY06 FY08 Elimu ya msingi Elimu ya sekondari Elimu ya juu Chanzo: Hesabu kulinagana na Benki ya Dunia Angalia Table 2 katika Annex 26 Kuongeza kasi ya Maendeleo Wakati gharama za utoaji wa elimu ya msingi na sekondari zikiwa zinategemea sana mifumo ya gharama katika sarafu za nchi husika, mifumo ya gharama za elimu ya juu na hasa elimu ya chuo kikuu inajumuisha mifumo ya manunuzi ya kimataifa katika sarafu za kigeni. Faida ya wafadhili kugharamia elimu ya juu inaonekana kuegemea kwenye uwezo wa kutoa elimu na ujuzi wa kimataifa ili kuibua na kuendeleza mageuzi katika mifumo ya elimu ya juu au kusaidia utambulishaji wa taaluma zinazohitajika zaidi. Wakati wa makongamano matatu yaliyolenga elimu ya juu yaliyodhaminiwa na Benki ya dunia, bara la Afrika lilianzisha programu katika elimu ya juu yenye jina linalofahamika, sayansi na teknolojia ambayo inalenga kubainisha mahitaji ya nchi husika.2 Lengo ni kuangalia msaada wa benki ya dunia, msaada wa kiufundi, na shughuli za ujifunzaji kwa kuzingatia mikakati ya nchi husika na bara zima inayoweza kuzisaidia nchi zinazofadhiliwa kutoa elimu bora ya juu na elimu ya juu yenye uhusiano na nchi husika kwa asilimia kubwa ya watu wao wanaongezeka sana kwa vigezo endelevu. Maeneo yafuatayo yanaweza kupewa kipaumbele: (i) kuboresha sera endelevu za ugharimiaji katika kuongeza wanafunzi (ii) kuifanya elimu ya juu itoe pia elimu ya ufundi, kuongeza ushirikiano wa vyuo vikuu binafsi na vya umma, na kuhimiza uanzishwaji wa vyuo vikuu binafsi; (iii) kuimarisha mazingira ya kisera na utawala wa kisekta na uwezo wa uendeshaji wa kitaasisi.; (iii) kuboresha ubora wa elimu kwa kuongeza walimu wenye sifa na kuboresha mbinu za kuhakiki ubora na uwezo wa kuiga teknolojia mpya, pamoja na TEHAMA; (v) kuimarisha miunganiko ya soko la ujira kwa kuhimiza miunganiko na viwanda, mitaala iliyoboreshwa, na uwezo wa kibara kupitia vituo vya ubora vya kibara na mitandao ya kufundishia. Ni wazi kwamba maeneo ya kipaumbele yaliyobainishwa siyo ya nchi zote na kwa wakati wote. Kiwango cha kipato cha nchi, ukubwa wa nchi na utulivu wa kisiasa, pia na kama nchi imetoka katika vita, vyote lazima zingatiwe. Mifumo ya elimu ya juu inatambuliwa kuwa ya kizamani na imeegemea matakwa fulani yanayozuiwa kuingiliwa na mataifa ya nje. Kwa hiyo mchakato mpana wa mashauriano utakaowahusisha washika dau wote 2 Makongamano mawili ya kanda ya Benki ya Dunia Afrika kuhusu elimu ya juu (Accra, 2003; Ouagadougou,2006) na Mjadala wa kidunia kuhusu Sayansi na Teknolojia na Uvumbuzi uliodhaminiwa na Benki ya Dunia, huko Washington, DC, Februari 2007. Kuongeza kasi ya Maendeleo 27 ndiyo njia bora ya kutekeleza mageuzi haya. Ili kutoa msaada unaohitajika kwa wateja wake wanapotafuta masuluhisho endelevu kwa changamoto za elimu zao za juu, Benki ya dunia hutumia mtazamo unaoegemea mahitaji na hali ilivyo katika kila nchi. Hasa, benki ya dunia inarekebisha uingiliaji kati wake (kukopesha au kutokopesha) kwa kiwango cha ulazima kwa mageuzi katika mfumo husika wa elimu ya juu pia na kwa kiwango cha utayari wa kisiasa wa nchi katika kufikia mageuzi hayo. Uingiliaji kati unafanywa kwa kutumia muunganiko wa: (i) msaada wa kiteknolojia katika kuandaa mikakati itakayowezesha taasisi za elimu ya juu kupata vyanzo vya nje na kupata vyanzo toka katika mashirika ya kimataifa na wafadhili; (ii) kukopesha ili kusaidia miradi ya serikali iliyojumuishwa katika mikakati ya usaidizi kwa nchi; na (iv) mikopo ya mashirika ya kimataifa kwa taasisi binafsi. katika uingiliaji kati wowote benki ya dunia hutegemea ushirikiano na washirika wengine wa maendeleo na jumuiya za kikanda. 28 VIAMBATISHO Jedwali 1: Kanda ya Afrika – Mikakati Mipya ya Elimu kwa Sekta Ndogondogo MF 1990 – 2008 IBRD + IDA mikakati mipya (mamilioni ya fedha katika dola za kimarekani) MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF Visekta 90 91 92 93 94 95 96 97 98 99 00 01 02 03 04 05 06 07 08 Elimu ya Kuongeza kasi ya Maendeleo msingi 92 153 83 184 99 104 95 15 226 126 57 60 214 238 92 106 91 258 45 Elimu ya sekondari 39 19 40 32 26 12 19 98 11 14 14 54 124 11 18 141 4 Elimu ya juu 120 31 164 131 70 30 42 12 46 25 14 17 69 46 61 29 106 105 Jumla 251 203 287 347 195 146 137 46 370 162 85 91 283 292 262 178 138 505 154 Chanzo: data za Benki ya Dunia Jedwali 2: Kanda ya Afrika – mikakati mipya ya elimu kwa sekta ndogondogo MF 90 – 08 Maendeleo ya wastani kwa pande mbili wa miaka mitatu IBRD + IDA mikakati mipya (mamilioni ya fedha katika dola za kimarekani) MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF MF Visekta 90 91 92 93 94 95 96 97 98 99 00 01 02 03 04 05 06 07 08 Elimu ya msingi 122 108 140 122 129 100 72 112 123 137 81 111 171 181 145 96 152 131 151 Elimu ya sekondari 29 33 30 33 23 19 16 59 43 41 13 14 34 89 63 51 43 43 55 Elimu ya juu 75 105 109 122 77 47 28 33 27 28 19 33 43 58 54 45 77 92 123 Jumla 226 246 279 277 229 166 116 204 193 206 113 158 248 328 262 192 272 266 329 Chanzo: ukokotozi ulioelemea data za Benki ya Dunia Ufunguo MF=Mwaka wa fedha Kuongeza kasi ya Maendeleo 29 30 Kuongeza kasi ya Maendeleo