!. viromen-alSc:a MRADI WA UMEME WA GESI YA .. Environmental & Social * Assessment & Management SONGO SONGO . 5: Plan Sum m ary - Sw ahili -- --- ------------ -- - ---- - ---- - ------- - - --- -------------- - - - - ------------------------------ ::Plan Summary - Swahili *: - - ------ O TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI 0 14 ~~~~Muhtasari wa Tafirti za Athari za Kimazingira na Mpango wa Kina wa Udhibiti Oktoba 2001 E65 v.2 October 2001 9. 9. .-. 0- ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ *. .. , _ ;d.-- - v-~ = - - l . . ,= D i (_ -t * . .,.,. . ( * 0 . . ,:;5! . i½. ' . ,' ' 'o P y ..~~ :. .... -i, ..:.E, ......... . . : .q :.;,-.. . . S.. " ':y,, .D ,,,,s, 0 N;~~~('~~igu 0* TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIIAMI NA MPANGOWA UDHIBITI Oongas Mradi wa Umeme wa Gesi ya Songo Songo TA-HMINI Z KIMAZINGIR NA KIJAMII NA HMANGO WA UDuIBITI Congas Mradi wa Umeme wa Gesi ya Songo Songo Tathmini za Kimazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti Muhtasari waTafiti zaAthari za Kimazingira na Mpango wa Kina wa Udhibiti Oktoba 2001 Kampuni ya Songas Nyumba ya Maarifa Mtaa wa Ohio Dar es Salaam Simu: +255-22-21 1-7313 Faksi: +255-22-21 1-3614 www.songas.com info@songas.com TATHmINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI Mombasa - , Tanga,. Pernba - ~i1. -ZANZI BAR I_____ 1' __ I - ~~~~~Unguia F____ Kh ha $Ka arLi - S Mtambowaurjmc rvU DAR ES SALAAM Mkuranga O'0 Mazomorao _ ~~~~BunguO , , -- ~NgulakulaVSW0 I. ! --4 -! - _ i,- ,0 ,AVYAMAFIA z Mbvera _ Sormanga Visima vya Gesi naMtarbowa a: Kitwa Kivinieo Kusafisha Gsi < Kitwa hlasoko Lindi Mitwara ' (Gesi iliyogunduliwa Mnazi Bay) Ramani 1: Eneo la Mradi wa Gesi ya Songosongo 2 TATHMINI ZA KIMAZING,RA NA KIJAmII NA MPANGO WA UDHIBITI SURAYA Ufupisho Gesi asilia iligunduliwa mwaka 1974 katika kisiwa cha Songo Songo kilicho nje kidogo ya pwani ya mashariki mwa Tanzania. Mradi wa gesi ya Songo Songo kuzalisha umeme umepangwa kuendeleza na kuuza raslimali ya gesi asilia nchini Tanzania. Wadhamini wa sekta binafsi wa mradi wa Songo Songo ni Shirika laAES na Kampuni ya Nishati ya PanAfrica. Kampuni ya utekelezaji inaitwa Songas Limited (Songas), ambayo ni kampuni binafsi kwa asilimia kubwa na imesajiliwa kwa mujibu wa sheria yaTanzania.Washiriki wa Mitaji wa CDC pamoja na Shirika la Maendeleo ya Fedha laTanzania (TDFL) ni wawekezaji wa hisa pia. Wakopeshaji wa mradi huu ni Benki ya Dunia na Benki yaWawekezaii ya Ulaya. Maelezo kuhusu Mradi Mradi utatoa gesi asilia kutoka kwenye visima vya gesi huko Songo Songo na kuipeleka kwenye mtambo wa kuzalisha umeme wa Ubungo unaoendeshwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).Vilevile gesi itapelekwa kwenye kiwanda cha Saruji chaWazo, jijini Dar-es-Salaam. Eneo lote la mradi limeonyeshwa kwenye ramani namba 1. Sehemu kuu za mradi ni pamoja na: (i) visima vya gesi katika kisiwa cha Songo Songo (tazama picha ukurasa 3); (ii) mfumo wa kukusanya gesi na kiwanda cha kuisafisha katika kisiwa cha Songo Songo; (iii)kilomita 25 za bomba litakalolazwa chini ya maji kutoka kisiwa cha Songo Songo hadi Somanga Funga na kilomita 207 za bomba litakalozikwa ardhini kutoka Somanga Funga hadi Dar-es-Salaam; (iv)kilomita 16 za bomba kuelekea kiwanda cha Saruji chaWazo; (v) mitambo ya kuzalisha umeme (tabaini) iliyoko kwenye kituo cha umeme cha Ubungo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 112 za umeme na yenye uwezo wa kutumia gesi asilia; (vi)udhibiti wa mfumo, kituo cha uendeshaji na miundombinu mingineyo pale Ubungo, na (vii)utawala na mafunzo kwa mradi. Ahadi za Songas za masuala ya mazingira na kijamii Songas, kwa kupitia wafadhili wake pamoia na Serikali yaTanzania, inakusudia kwa dhati kuendeleza mradi wa Songo Songo kwa utaratibu ambao utaweka mizania (wakati wote na kwa kuwajibika) kati ya uhifadhi wa mazingira na sura ya kijamii ya Tanzania na uondoaji wa umaskini na faida za kiuendeshaji za mradi. Kwa kutumia filosofia hii na mwelekeo huu, Songas itadumisha fursa bora na za muda mrefu za kibiashara kwa ajili ya wadhamini wa mradi huu na maslahi yanayoambatana nayo ya washikadau wa nchi, kanda, na mahali ambapo mradi unatekelezwa. AES, kampuni inayoongoza kwa hisa, ina sera ya kuchangia hadi asilima 5 (5%) ya mapato halisi kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Maamuzi yanayohusiana na kiwango na mahali ambapo msaada uta- tolewa umeachiwa mameneja wa zaidi ya mitambo ya umeme 125 inayoendeshwa na kampuni ya AES duniani kote. Kwa makubaliano na wanahisa wengine wa Songas, kampuni ya Songas itaanzisha TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KI.AMII NA MPANGOWA UDHIBITI Kisima cha Gesi cha Nchi Kavu i- - A - ;_____- - I__C __ _ __ S _ |~~S |~~~~~~ ~ _ - Kisima cha Gesi cha Baharini 3 TATHiM NI ZA KImAZINGIRA NA KrJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI sera kama hiyo nchini Tanzania. Mwezi Juni mwaka 2000, sheria ya kodi ya Tanzania ilibadilishwa, hivyo kuipa moyo zaidi Songas kuchangia maendeleo ya kijamii nchini Tanzania. Sera na Masharti ya Kiurekebishaji na ya Kisheria Mradi wa Songo Songo umeandaliwa na utaendeshwa kwa kulingana na matakwa ya kanuni na she- ria, ikiwa ni pamoja na zile za Serikali yaTanzania na Benki ya Dunia. Mashauriano na Uarifu wa Umma Sehemu muhimu tatu za mradi wa Songo Songo, tayari zimekamilika. Mafanikio ya sehemu hizi ndogo tatu za mradi yanaonyesha mawasiliano mazuri ya Songas na mashauriano yenye mafanikio kati yake na watu waliothirika na mradi. Mradi wa Songo Songo unafahamika sana na umma wa Tanzania na umeelezewa vizuri sana katika magazeti, redio na televisheni. Songas imepanga kuen- delea kuwasiliana vizuri na washikadau wote na watu walioathirika na mradi ili kuwe na taarifa sahihi zinazotolewa kwa washirika wote kuhusiana na mradi. Zaidi ya kuwepo kwa majadiliano mengi na umma pamoja na tathmini, Songas imekubaliana na masharti rasmi ya uarifu ya Benki ya Dunia kwa ajili ya tathmini za mazingira kwa kutoa taarifa zake kwa Kitengo chaTaarifa cha Benki ya Dunia na hapa nchini. Kwa kuzingatia hilo, ripoti yaThathmini za Mazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti, ilisambazwa kwa washikadau wote ndani na nje ya Tanzania. 1 - 1_ ; J _N~L , 4~~ _ F~~~~~71_ Mkutano wa wananchi walioathirika na Mradi TATHMINI zA KIMAZNGIRA NA KilAmii NA MPANGO WA UDHIlM Upembuaji waVibadala na Uteuzi wa Njia Songas imechunguza vibadala vingi, ikiwa ni pamoja na njia mbadala za kuzalisha umeme, umbo mbadala la mradi, na njia mbadala za bomba la majini na la nchi kavu ili kufikia mfumo unaokubali- ka na usio na gharama kubwa. Muhtasari waTafiti za Kimazingira na Kijamii Katika kuupa mwega mradi wa Songo Songo, Songas imegharamia utayarishaji wa ripoti maalum zipatazo 28 zinazohusu mazingira na mada nyingine za kijamii tangu 1993. Kama ilivyodokezwa, kazi hii ilifanywa i1i kutekeleza masharti ya tathmini ya Benki ya Dunia na Sekta mbalimbali zaTanzania zinazohusiana na mazingira na wajibu wa kijamii. Kwa ufupi, ripoti hizo zinapendekeza kuwa mradi hautakuwa na athari mbaya za kimazingira na kijamii kama Songas na makandarasi wake wakubwa na wadogo watatekeleza hatua za kupunguza makali zilizopendekezwa, kusimamia na kufuatilia hatua hizo. Athari za Kimazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti Songas inakusudia kutumia "mwenendo bora" wa kimataifa katika udhibiti wa athari za kimazingi- ra na kijamii za mradi wa gesi ya Songo Songo wa kuzalisha umeme. Songas itasanifu, kuunda na kuendesha mradi na kutekeleza mfumo wa usimamizi wa mazingira, afya na usalama ambao umeegemea kanuni za Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO), ISO 14001. Muundo wa Utawala wa Songas Songas itakuwa na wajibu kamili kwa mambo yote yanayohusu mradi wa Songo Songo kwa kutu- mia timu ya uongozi yenye uzoefu katika kuendesha majukumu yake.Wakati wa kipindi cha ujen- zi, majukumu ya kuchukua hatua mbalimbali za kimazingira na kijamii kwa ajili ya udhibiti na usi- mamizi yataachiwa makandarasi. Katika mazingira kama hayo, Songas itabaki na uwezo wa kusi- mamia i1i kuhakikisha kuwa makandarasi wanatekeleza wajibu wao. Wajibu wa Makandarasi Songas itahakikisha kuwa mikataba na makandarasi wakuu na wadogo wa ujenzi inazingatia vipen- gele maalum vya mfumo wa usimamizi wa mazingira, afya na usalama ambavyo vitakuwa ndani ya wigo na wajibu wa mkandarasi. Maelezo kuhusu Masuala Muhimu: Ridhaa Ukuzaii wa mpango wa udhibiti wa kimazingira na kijamii kwa aiili ya mradi wa Songo Songo umeridhia Sera za Utekelezaji na Maagizo ya Benki ya Dunia kama inavyoonyeshwa katika jedwali linalofuata: TATHMINI ZA KIMAZINGIRA MA KIJAMII NA MPANGO WA UCDI-ITI OP 4.01 :Tathmini ya Mazingira. Mradi unaridhia:Tathmini ya mazingira imetayarishwa kulingana na masharti ya mradi wa kategoria A. OP/BP 4.04: Makazi Asilia Mradi unaridhia: Mradi umetumia mwelekeo wa kitahadhari katika usi- mamizi wa rasilimali za asili katika jitihada za kuhifadhi na kulinda makazi asilia, kuyaepuka makazi muhimu na kudumisha shughuli za kiekolojia. Kila inapokuwa budi hatua za kupunguza na kuondoa tatizo zimebainishwa ili kupunguza kasi ya upoteaji wa makazi pale ambapo hali haizuiliki. Mdhamini wa mradi atatoa pia uhakika wa fursa za maendeleo endelevu ya muda mrefu katika nchi kwa kupitia mpango wake wa maendeleo ya jamii, michango na ushiriki katika Bodi ya Mfuko wa Kanda ya Mashariki (The Eastern Arc Endowment Trust Fund) na Chama cha Hifadhi ya Wanyamapori chaTanzania, OP 4.09: Udhibiti wa wanyama Mradi Unaridhia: Mdhamini wa mradi hatatekeleza shughuli yoyote ya au wadudu waharibifu kudhibiti wanyama au wadudu waharibifu. OPN 11.03: Mali ya Kijadi Mradi unaridhia: Usanifu kamambe wa njia utaepuka uharibifu mkub- wa kwenye mali za kitamaduni zinazofahamika na zisizoweza kurejeshwa upya. Zaidi ya hayc, mdhamini wa mradi atasanifu na kutekeleza programu ya uandani ya kushughulikia'mali ya Kijadi itakayobahatika kuonekana' yaani 'Chance finds' wakati wa ujenzi wa mradi. OD 4.20: Wenyeji Haihusiki: Hakuna mwenyeji, kama ilivyofafanuliwa na OP 4.20, ambaye ataathinika na mradi. OD 4.30: Kulazimika kuhamia Mradi unaridhia: Mdhamini wa mradi ametayarisha Programu ya tath- Makazi Mapya mini ya Kiuchumi-jamii ili kuhakikisha kuwa wale waathirika wa mradi wanasaidiwa ipasavyo kwa ajili ya mali walizopoteza na kwamba mapato yanarejeshwa au kuboreshwa kulingana na sera.Tafiti nyingine zinapen- dekezwa za kukagua uridhiaji wa sera na kuongezea kanzi ya data za kiuchumi-jamii kwa ajil. ya jambo hili. OP 4.36: Misitu Mradi unaridhia Mradi haujihusishi na biashara ya magogo au ununuzi wa vifaa vya magogo. Kwa kuwa uoto fulani utafyekwa katika maeneo yaliyopangwa, mfadhili wa mradi atatekeleza hatua za kupunguza uharibi- fu ili kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara katika uoto pamoja na hatua nyingine yoyote ziiakazopendeke7wa na Idara ya Misitu yaTanzania. Mfadhili wa mradi atafanyakazi pia na wenyeji, na MashirikaYasiyo ya Kiserikali (NGO's) kila inapobidi, ili kuendeleza hatua za uimarishaji na urejeshaji uoto juu ya ardhi. OP/BP 4.37: Usalama wa Haihusiki: Mradi haujishughulishi na ujenzi wa mabwawa. Mabwawa OP/BP/GP 7.50: Miradi iliyoko Haihusiki: Mradi utaendeshwa katika eneo la maji yaTanzania pekee. katika Njia za Maji za Kimataifa OP/BP/GP 7.60: Miradi katika Haihusiki: Mradi hauko wala hautaingia hadi kwenye maeneo yenye Maeneo yenye mgogoro mgogoro. Sera ya Utoaji wa Habari Mradi unaridhia:Taarifa kuhusiana na mradi zimekuwa zikitolewa na zitaendelea kutolewa nchini Tanzania na katika Kitengo cha habari cha Benki ya Dunia. Viwango vya Kazi Mradi unaridhia: Mdhamini wa mradi hatatumia ajira ya watoto au ya nguvu. 6 TAT-MINI ZA KiMAZINGIRA NA KIJAMIl NA MPANGO A UDHIRcI Masuala muhimu ya Kimazingira na Kijamii Sura ya 7 ya ripoti ya mazingira ambayo huu ni muhtasari wake inajumuisha muhtasari na masuala ya mazingira ya asili na pia tafiti za kijamii, matumizi ya ardhi na kiuchumi-jamii, ikiwa ni pamoja na masuala ya afya, makazi na fidia. Sehemu hizi zinajumuisha haii za msingi za mazingira kufuatana na aina na unyeti wa mazingira katika ukanda unaopita bomba. Sura ya 8 inaeleza kwa kina athari zinazoweza kutokea za kijamii (ikiwa ni pamoja na za kiuchu- mi-jamii) na athari za kimazingira pamoja na hatua zitakazochukuliwa na Songas ili kupunguza athari hizo na kuongeza faida zinazotokana na mradi kwa wenyeji na taifa zima. Masuala muhimu ya kimazingira na kijamii, yaliyo chanya na hasi, yaliyobainishwa wakati wa uchanganuzi wa tathmini ya athari za mradi huu na namna Songas itakavyoyadhibiti yameorod- heshwa hapa chini. 1. Bioanuwai - Spishi za kimamalia zinazohitajika kuhifadhiwa zinapatikana katika eneo la mradi. Shughuli za mradi zitafanywa kwa namna ambayo haitaziathiri spishi hizi wakati wa ujenzi na uendeshaji wa mradi. 2. Misitu - Haki ya njia inapitia katika maeneo yenye uoto wa asili. Songas itatumia njia zote zinazowezekana kupunguza ukataji wa miti na itasaidia shughuli za usimamizi mzuri wa misitu katika ukanda unaopita bomba. 3. Maji - Songas itawapatia wakazi wa kisiwa cha Songo Songo maji safi ya kunywa (pamoja na umeme) kutoka kwenye kiwanda cha gesi. 4. Mmomonyoko wa Udongo - Mkandarasi atahakikisha kwamba maeneo yanay- omomonyoka kirahisi yanaimarishwa baada ya kutibuliwa. 5. Taka - Songas itatekeleza mkakati wa kudhibiti taka ngumu kwa mradi wote ili kuhakikisha kwamba taka zinaondoshwa kwa namna isiyohatarisha mazingira. 6. Hewa - Utoaji wa hewa kutoka kwenye mradi utazingatia miongozo ya Benki ya Dunia. Gesi zitakazotolewa zitachangia kwenye utoaji wa gesi zenye kuongeza kiwango cha joto katika angahewa duniani, lakini kwa kiasi kidogo zaidi kuliko kama mitambo ya kuzalisha umeme (tabaini) zingeendelea kutumia fueli mafuta. 7. Bomba - (Majini na Nchi Kavu) - Ili kushughulikia uvujaji wa gesi utakaotokea kwa bahati mbaya, Songas itaunda na kutekeleza mpango wa dharura wa kudhibiti hali itakayotokana na uvujaji wa gesi. 7 TATHmI-NI ZA KIMAZ NGIRA NA KjAmII NA MPANGO WA UDHIBITI . j ' -fI;'., I . , _ Kikundi cha wahasibu wakilipa fidia kwa walioathirika na mradi 8. Masuala ya Kiuchumi-jamii - Ujenzi na uendeshaji wa bomba utatoa ajira za kutosha nchini Tanzania na katika eneo la mradi. Songas itamhitaji mkandarasi kutumia nguvukazi ya wenyeji na kununua bidhaa na huduma za wenyeji wa eneo la mradi. Songas itaziunganisha jumuiya zilizoathirika na mpango wa mikopo midogomidogo.Jumuia zitafaidika pia na ukuzaji wa biashara ndogondogo. 9. Masuala yanayohusiana na Afya - Kwenye kisiwa cha Songo Songo, Songas itainua viwan- go vya watumishi wa afya na kituo kinachotoa huduma ya afya ili kuhudumia vizuri zaidi wananchi na watumishi wa mradi. Songas itaandaa mkakati wa kuthibiti ueneaji wa VIRUSI/UKIMWI katika maeneo yote ya mradi. Makazi Mapya Shughuli za kuwapatia wananchi makazi mapya zilifanyika chini ya Mipango ya Utekelezaji ya Makazi Mapya iliyopangwa kutekeleza masharti ya Benki ya Dunia na yale ya Serikali ya Tanzania, hii ni pamoja naAgizo la Kiutendaji nambari 4.30 la Benki ya Dunia:Mpango wa Kulazimika kuhamia Makazi Mapya. Songas imekwishafanya uchunguzi unaohitaiika, ikaandaa mipango inayotakiwa, na katika baadhi ya maeneo ikaanza utekelezaji na ufuatiliaji wa programu zinazohitajika ili kuhakik- isha kuridhia kwa sera za Benki ya Dunia za usalama wa kijamii, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Kulazimika KuwapatiaWananchi Makazi Mapya. Programu za fidia za Songas ziliandaliwa mahsusi kuwarejeshea mapato watu walioathirika na mradi. Mradi umelipa fidia kwa viwango vya soko, ambavyo ni vikubwa kuliko viwango vilivyowek- wa na serikali yaTanzania.Viwango vya fidia ni vikubwa mara tatu zaidi ili kurejesha mapato ya watu 8 TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIUAMII NA MPANGO WA UDHIBITI waliofidiwa na huku yakiwepo makusudio ya kuboresha, au kukaribia hali ya maisha yao kabla ya kuathirika na mradi. Kwa ujumla, jambo lililozingatiwa sana katika kupanga njia litakamopita bomba lilikuwa ni kupunguza usumbufu na kuwapatia wananchi makazi mapya. Kutokea mahali bomba linapoibuka kutoka majini na kuingia nchi kavu hadi viungani mwa Dar es Salaam (umbali na takribani kilomita 200), ni kaya 33 tu ndizo zilizohitajika kupatiwa makazi mapya. Zaidi ya hayo, ingawa bomba linapi- tia katika eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam, ni kaya 155 tu zilihitaji kuhamishwa kutoka kwenye eneo la njia ya bomba katika maeneo ya mji. Maeneo mawili yalichaguliwa kwa ajili ya makazi mapya ya familia katika eneo la Dar es Salaam - Kinyerezi, kusini mwa Dar es Salaam, na Salasala, huko kaskazini (tazama ramani namba 2). Kaya nyingine 155 zilizoathiriwa na mradi, ni kaya ambazo zilikuwa katika maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma, zimefidiwa pia na kuhamishiwa humo humo ndani ya maeneo ya makazi mapya. Makazi haya mawili yaliyopangwa vizuri ni rasilimali kubwa kwa jiji la Dar es Salaam. Mpango wa Ufuatiliaji wa Mazingira na Jamii Songas inatekeleza Mpango wa Ufuatiliaji wa Mazingira naJamii ili kufuatilia athari za mradi. Mpango huu unajumuisha maeneo yanayohusika na bomba la Songas, mitambo ya kuzalisha gesi na uende- shaji wa mtambo wa kuzalisha umeme. TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI _A1TONGA A~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~A t:,,, ; Nt -:~~~~~~~~~~~~A . _ . - V BAHARI HINDI 1, ~ ~ s S. lani 0~~~~~~~~~~~~ >111~ 'h 'Ii /; I I' E, n e, Xi-.z; D1ar-es Salaam- : 7 _ >_;F_ 1 ,-^ s~~~~~~Kituo . 60~~~~~~~~~~~~ ~~~~~~~~~~~~~~ ,.--,S'-~ ~ ~~>-~. I;; ,I - . .... TA -- --- -- ----, . Maka, mapya Mkaz, Bambamin kgog Njla ya ges ya Songosongo ~~~~~~~~~~~~~~~~~~ -- Maneoy i'm a Yaal e. --u M starl ya kontua RamMani k2: . Maeneo-kMto yMkzap Ramani 2: Maeneo ya Makazi Mapya~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ TATHMINI ZA KiMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBIT SURAYA 2 Shughuli za Programu ya Maendeleo ya Jamii hadi Januari 2001 Fursa za kuboresha mapato Mapato ya watu walioathirika na mradi inawezekana hayakuwa hasi, hasa katika maeneo ya vijijini ambako watu waliofidiwa na mradi bado wanaendelea kutumia mashamba ambayo tayari wame- fidiwa. Hili lilifanyika i1i kujenga uhusiano mzuri kati ya mradi na jamii za wenyeji. Maji Kwenye kisiwa cha Songo Songo, mradi umejenga tangi la maii lenye mabomba kwa ajili ya kuwa- patia wananchi maji yaliyowekewa dawa (maji safi na salama) kutoka mapangoni wakati wakisubiri kupatiwa maii (yatakayofikishwa hadi kwenye mpaka wa mtambo wa gesi na mradi) kutoka kwenye mtambo wa gesi. Kuwepo kwa mfumo wa kuwekea maji dawa kumeongeza sana ubora wa maji. Usafi Utoaji wa maji kisiwani umeboresha afya na usalama, kwani ugumu wa kuchota maji toka kwenye mapango yenye kina kirefu umepungua. Upatikanaji wa maji umesababisha kuwepo na mazingira mazuri zaidi kwa wanakijiji. Nyumba Bora Kumekuwepo mabadiliko toka nyumba za kuezeka kwa makuti hadi nyumba za bati, hasa katika maeneo yaliyofidiwa na mradi, kwa mfano: Rungungu, Bungu na Jaribu Mpakani.Wananchi wame- boresha sana ubora wa nyumba zao na sasa wanapanga kuvuta umeme hadi vijijini mwao. Mipango Jiji Makazi mapya ya mradi huko Kinyerezi na Salasala yalikuwa maeneo yenye sifa za kijiji na ambayo hayakupimwa. mradi umeyabadilisha na kuwa makazi yaliyopangwa yenye idhini kamili ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kama yanavyoonekana katika ramani namba 3 na 4. Elimu Mradi wa Songo Songo umesaidia katika ukarabati wa Shule ya Msingi ya Songo Songo, ambapo mradi umechangia vifaa vya ujenzi kama vile mifuko ya saruji, mabati ya kuezekea na mbao za kuandikia madarasani. Zaidi ya hayo, mradi uliwahamasisha watoto kwenda shule kwa kutoa ufad- hili kidogo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ya sekondari na vyuo. Kalamu na madaftari vimetolewa kama msaada kwa shule kadhaa katika maeneo litakamopita bomba na katika kisiwa cha Songo Songo. TATHM[NI ZA KIMAZINGIAm NA KIIAMl NA MPANGO WA UDHIRM I., ~ ~ ~ * _ _ _ _ _ _ , _ _ _ _ _ _ _ _ _ ak_ Mk2i Nj. Y g. Y. S---- -w,,): *1.~~~~~~~~~~~~~1 q~~~~~~~~~~~ - -;{ - N N P-, ,. ~ ~ ~ ~ ~ ~ 6,, OAOg MAt'M Msnoaionmkz -- MN we Ramani 3: Eneo la Makazi Mapya Kinyerezi 12 Ramani 4: Eneo la Makazi Mapya Salasala Machirnba ' MTONGANI a i ' m~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ ya Mawe -~ ' Makazi m-pya 4 Makatl mapya Banabana n go _ __, Mlitatya bomba la gesl ya SongoM.sya Ma go i.4 p~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 3 .4 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~-~~~~~~~~~~~~~I~~~~0 MaEEE, mapyE Makazi m~~~~~~~~~ya Barabara WI NilE ~~~~~~~E bombs Ia YEsI ya Songosongo~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ BambOo 09090 ~ ~~~~~~~~ 040001150 komua~ ~~~'P0 1 Mel Nia YE mig~~~~~~~~~~~~~~~~~~~a ~ ~ ~ ~ Mto ~ ~ ~ ~ TATHMINI ZA KIMAZINGtRA NA KIJAMil NA MPANGO WA UDHIBITI Ushauri Watumishi wa mradi waliwatembelea MaafisaWatendaji wa Kata na kuzungumza nao juu ya mata- tizo kadhaa ya kijamii na kimazingira vijijini mwao. Maofisa wa mradi waliwapatia MaafisaWatendaii Kata, viongozi na wazee wa kijiji changamoto mbalimbali. Matokeo yake ni kwamba watoto wengi zaidi wameandikishwa shule na watu wengi zaidi wamehudhuria vituo vya afya. Wakati wa Programu ya Kufidia Haki ya Kupita Njia, watumishi wa mradi walishauriana mara kwa mara na wanavijiji katika jamii zilizoathirika juu ya masuala yanayohusu maisha yao na masu- ala mengine yanayohusiana na mradi kama vile elimu na afya. Hili lilifanyika katika mikutano kadhaa wakati wa kuzitembelea ofisi mbalimbali vijijini. Miundombinu Wakazi wa kisiwa cha Songo Songo hurusiwa kutumia viti vilivyo wazi kwenye ndege za kukodish- wa kutoka kisiwani hadi mikoa ya Dar es Salaam na Lindi. Zaidi ya hayo, wanatumia gati la saruji (ambalo linahitaji kukarabatiwa) kufunga vyombo vyao wakati wa kupakia na kupakua mizigo na abiria, kwani gati lao la zamani la mbao halitumiki tena. Mabadiliko ya Hali ya Maisha Kumekuwepo na mabadiliko ya hali ya maisha katika maeneo kadhaa kama vile Kinyerezi na kati- ka kisiwa cha Songo Songo kwani watu sasa wanaishi katika nyumba nzuri zaidi baada ya kulipwa fidia na baada ya programu ya uhamasishaii iliyofanyika kisiwani. Programu ya uhamasishaji ilifanyi- ka ili kuwaandaa wakazi wa kisiwa kwenda sambamba na mabadiliko yanayohusiana na mradi kati- ka vipengele vingi kwa mfano: kutayarisha nyumba zao kwa ajili ya kuingiza umeme. 14 TA:HMINI ZA KIMAZINGIPA NA KIrAMII NA MPANGO WA UDHIBITI SURAYA 3 Mpango wa Shughuli za Baadaye za Programu ya Maendeleo ya Jamii Elimu Kwenye kisiwa cha SongoSongo, Songas hutoa ada kwa wanafunzi watatu wa kwanza wanaochag- uliwa kuendelea na elimu ya sekondari baada ya kufaulu mtihani wa taifa wa darasa la saba. Programu hii ilianzishwa mwaka 2000 na itaendelea wakati wa utekelezaji wa mradi. Hadi sasa wanafunzi watatu (3) wanafaidika na programu hii. Programu nyingine za kielimu na misaada zitatolewa kwa kisiwa cha Songo Songo na jamii zilizomo katika maeneo linakamopita bomba la gesi. Hii itakuwa huduma moja miongoni mwa huduma nyin- gi zitakazotolewa kwa jamii zilizoko kwenye maeneo linakamopita bomba la gesi, kulingana na wajibu wa kimazingira na kijamii ambao Songas imeahidi kutekeleza. Maji na Umeme Songas itawapatia wakazi wa kisiwa cha Songo Songo maji na umeme bure hadi kwenye mpaka wa mtambo wa gesi. Usambazaji wa maji na umeme katika maeneo muhimu ya jamii utafanywa na Programu ya Usambazaji UmemeVijijini. Miundombinu Songas itapanua na kuboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na barabara na upatikanaji wa maji na umeme kwa jamii za makazi mapya ya Kinyerezi na Salasala jijini Dar es Salaam. Juhudi za kurejesha mapato Songas itaziunganisha jumuiya zilizoathirika kwenye mipango ya mikopo midogomidogo. Jumuiya zitafaidika pia na uendelezaji wa biashara ndogondogo. Mipango hii itaendelezwa kupitia mashauri- ano kati ya wanavijiji na watumishi wa mradi. Ushauri Songas ina mpango wa kuendelea kuwa na mashauriano na wanavijiji katika jamii zilizoathirika juu ya masuala ya Programu ya Maendeleo yajamii hasa yanayohusu mipango ya mikopo midogo mido- go, uendelezaji wa biashara ndogo ndogo na masuala mengine yanayohusiana na mradi. Mpango wa Usambazaji UmemeVijijini Mpango wa kusambaza umeme unaotokana na miale ya jua (umeme wa sola) unachunguzwa kwa ajili ya familia zilizo karibu na njia ya bomba. Uchunguzi huu umeonyesha pia kwamba watu waishia 15 TATH-MINI ZA KIMPZINGIrIA NA KIJAMI, NA MPANCO WA UDHIBITI 4:S L~~~~', #_'_ s p~~~~~~~~~~~ -- t.^ 2 B . j. :1 m .2' .- . - i r ______ &iX Ene Ia Mrd Kiiw cha Songosong- ;' pes' 11ri,,;9S,.,^,,q,...16 TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAM I NA MPANGC WA UDHIBITI ~~- r ~~ S S v : e M5 Lr - ,r - -- i:'' W.~~~~~~~~~N _i~~~ ~ J- -- _ 4:- _ ---#> ' -- 3i '. 4 S ,-11 _ A . . . . Ai_ Mitambo wa Umeme - Ubungo 17 TATHMIN ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGOWA UDHIBrTI karibu na njia ya bomba wanatoa kipaumbele cha juu kwa maji na elimu. Hivyo kuna uwezekano kwamba baadhi ya fedha zilizotengwa kupitia mradi huu zitatumika kwa aiili ya shughuli nyingine za jamii zilizopewa kipaumbele, licha ya umeme. Songas itashiriki na kusaidia dhana yoyote itakay- oonekana inafaa kwa aiili ya utoaii wa gesi na/au umeme na huduma nyinginezo. Ahadi ya Songas ya Kutimiza Majukumu ya Kijamii Songas itachangia kwenye miradi ya maendeleo ya kijamii na ya kitaifa, ikitilia mkazo maalum kati- ka miradi iliyomo kwenye maeneo ya mradi,yaani kisiwa cha Songo Songo,eneo linamopita bomba na Ubungo. Mahitaji ya haraka sana kwenye kisiwa cha Songo Songo na katika maeneo linamopita bomba yanahusu afya na elimu.Aidha Songas itachangia kulinda na kuboresha mazingira na pia kuwa kichocheo cha kuleta mawasiliano miongoni mwa serikali za mitaa, serikali kuu na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). Wakati ambapo miradi yote ya maendeleo ya namna hii huzua mambo na masuala mbalimbali, mradi wa Songo Songo utafuata:- * Sheria, Sera naViwango vya Tanzania; * Sera za Usalama za Benki ya Dunia; * Miongozo ya Benki ya Dunia ya Kupunguza Uchafu wa mazingira, na * Miongozo ya Afya na Usalama ya Shirika la Fedha la Kimataifa. Kwa ujumla, masuala yamkini hasi ya kimazingira na kijamii yanayoweza kuibuliwa na mradi wa gesi ya Songo Songo yanaweza kudhibitiwa ili kwamba athari zake zipungue. Songas inaamini kuwa athari zozote hasi zitafidiwa kwa kiwango kikubwa na mazuri mengi yatakayotokana moja kwa moja na mradi katika maeneo ya mradi na faida kubwa kwa nchi kutokana na kuendeleza rasilimali hii muhimu. 18 TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI USAMBAZAJIWA RIPOTIYA UHAKIKIWA MAZINGIRA Uhakiki wa athari za mazingira, kijamii- uchumi na namna ya kuzirekebisha umekwishafanyika kama ilivyoelezwa hapo awali. Uhakiki wa kwanza ulikamilika mwaka 1994 na tangu hapo ripoti 28 za utafiti wa mazingira na kijamii - uchumi zimekwishatengenezwa. Ripoti zote hizo zimeungan- ishwa pamoja na kupata ripoti moia kuu ambayo niTathmini za Kimazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti. Ripoti hiyo ambayo huu ni muhtasari wake imesambazwa kwa washikadau wote. Baadhi ya sehe- mu ambazo inaweza kupatikana ni kwa wakuu wa mikoa ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam; wakuu wa wilaya za Kilwa, Rufiji, Mkuranga,Temeke, llala na Kinondoni.Vile vile inapatikana katika sehemu zifuatazo:- Katibu Mkuu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Nishati na Madini TANESCO Barabara ya Sokoine na Mkwepu Mtaa wa Samora Dar es Salaam Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Mratibu wa Mazingira,Afya na Usalama Baraza la Usimamizi wa Mazingira Songas Barabara ya Sokoine Nyumba ya Maarifa Dar es Salaam Mtaa wa Ohio Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Ofisi ya Benki ya Dunia Barabara ya Ali H. Mwinyi Kitalu namba 50 Dar es Salaam Mtaa wa Mirambo Dar es Salaam 19