90434 v1 TUNAHITAJI AJIRA ZENYE TIJA TANZANIA TAARIFA YA UCHUMI WA NCHI BENKI YA DUNIA MUHTASARI RASMI www.worldbank.org/tanzania Chanda Atulinda Lwansa Mshindi wa Shindano la Kuchora kwa Watoto, 2014 Lililofadhiliwa na Benki ya Dunia Picha kwenye jalada imechorwa na Chanda Atulinda Lwansa katika Shindano la Watoto la Uchoraji lililoandaliwa na Benki ya Dunia, kati ya Machi 17, 2014 na Aprili 17, 2014. Chanda, msichana wa miaka 12, ni mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Wasichana, Feza jijini Dar-es-Salaam na hupenda kuchora kwa burudani. “Napenda kuchora na hufanya niwe bize muda wote,” anasema Chanda. “Huwa napata msukumo kutokana na hisia au kitu nilichokiona, au kupenda kuwa bize tu, kwa hiyo naanza kuchora. Nilipoona tangazo kwenye gazeti, mara moja nikaamua nitaingia kwenye shindano. Nafurahi nilifanya hivyo!” Mama yake, Akiza Kamuzora, anasema Chanda alionyesha kupenda kuchora tangu akiwa na miaka mitatu. “Kuchora ni kitu anachokipenda baba yake kama burudani, kwa hiyo wakati wote alikuwa anamhimiza.” Chanda anapenda kusoma vitabu vya hadithi na kuandika hadithi fupi. Masomo anayoyapenda ni baiolojia na kemia. Ijapokuwa anasema “hana uhakika” anataka kuwa nani atakapokuwa mkubwa, hata hivyo Chanda anakiri ana ndoto ya mambo makubwa. “Kama nitaruhusiwa kuchagua, basi nitachagua kuwa mtengenezaji katuni au mbunifu. Nataka kuwa na kazi muhimu ambayo itanifanya nijulikane ulimwengu mzima. Napenda kuleta mabadiliko duniani.” Katika mchoro wake anaonyesha wanaume na wanawake wakijihusisha na kazi mbalimbali, madaktari, marubani, wana kemia, wafanyabiashara, shamba boi na walimu, Chanda anaeleza: “Na kiri hakuna Mtanzania anayepaswa kuzuiwa katika ndoto zake za kupata kazi nzuri na kipato cha juu.” Chanda alizaliwa tarehe 16 Machi, 2001 kwa wazazi Akiza na Mulenga Lwansa. Namara, mdogo wake mwenye miaka 7, pia anapenda kuchora na kuandika hadithi kama dada yake. TUNAHITAJI AJIRA ZENYE TIJA TANZANIA TAARIFA YA UCHUMI WA NCHI MUHTASARI RASMI Agosti 2014 Kitengo cha Uchumi Jumuishi na Fedha Benki ya Dunia Benki ya Dunia Kanda ya Afrika www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 3 Shukrani Taarifa ya Uchumi wa Tanzania ilitayarishwa na Jacques Morisset na Mahjabeen Haji. Tunatoa shukrani kwa michango iliyotukuka kutoka kwa: Alan Roe, Andrea Mario Dall’Olio, Arun Joshi, Austin Kilroy, Célestin Monga, Cristian Ugarte, David Rohrbach, Elisa Gamberoni, Francis Ratsimbazafy, Isis Gaddis, Hinh T. Dinh, Josaphat Kweka, Julie Regolo, Louise Fox, Murat Eker, Olivier Cadot, Paul Brenton, Remy Pigeois, Robert Stone, Shwetlena Sabarwal, Victoria Cunnimgham, Waly Wane, Yiye Lu, naYutaka Yoshino. Ripoti hii iliboreshwa na michango ya mashauriano mbalimbali kutoka kwenye makundi tofauti ya wadau, iliyojumuisha maafisa wa serikali, wafanya biashara na wengineo. Mashauriano hayo yalifanyika kati ya Oktoba 2013 na Aprili 2014, na tunawashukuru Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kwa kuwezesha shughuli hiyo. Mnamo Oktoba, 2013, warsha iliandaliwa katika jiji la Washington D.C., Marekani kwa ushiriki wa Benki ya Dunia na wanazuoni, pia na watunga sera muhimu wa Kitanzania waliojumuisha Profesa Benno Ndulu, Servacius Likwelile, Philip Mpango, Longinus Rutasitara, Joseph Massawe; na Danny Leipziger, Jim Adams, Marcelo Giugale, Gaiv Tata, Deon P. Filmer, na Ejaz Ghani. Mwisho, ripoti iliboreshwa na majadiliano ya mada mbalimbali zilizolenga sekta mahususi, yaliyofanyika katika Maabara za Mazingira ya Biashara kati ya Februari na Aprili 2013, na katika mwezi Machi 2014 kama sehemu ya Mpango wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’. Wachambuzi mbalimbali pia walipata nafasi ya kuchangia mawazo yao katika ripoti hii, wakiwemo John Page, Celestin Monga, Bill Maloney, na Samuel Wangwe. Timu ilipata mwongozo kutoka kwa Albert Zeufack na Philippe Dongier. Jamie Yang na Loy Nabeta walihariri ripoti hii, wakati Justina Kajange alitoa msaada mkubwa wakati wa utayarishaji wake. 4 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, Benki ya Dunia imekuwa ikiandaa mpango unaojumuisha sekta tofauti utakaoshughulikia changamoto za upatikanaji wa kazi zenye tija nchini Tanzania, ambao umewasilishwa katika Waraka mpya wa Uchumi utakaoitwa “Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija”. Utafiti huu ni hatua kuelekea uelewa mzuri zaidi wa jinsi ya kuongeza ajira nchini Tanzania. Ni kweli kwamba ongezeko la ajira zenye tija ni muhimu katika kupunguza umasikini na kukuza ustawi wenye uwiano – shabaha mbili muhimu katika mkakati wa kiuchumi wa Tanzania. Kijitabu hiki kinaweka msisitizo katika mpango wenye nguzo tatu wa kujenga ajira uliotokana na Taarifa ya Uchumi wa Nchi ya Tanzania. Kwa kuweka msisitizo katika hatua madhubuti zinazojumuisha sekta anuwai, lengo ni kusisimua mjadala ili kuongeza umiliki na uwajibikaji miongoni mwa watunga sera na wadau wakuu nchini. Hizi ndizo hatua muhimu za kuharakisha matumizi ya mpango huo. Tanzania haina mbadala kwenye suala hili. Nguvu kazi yake itaongezeka maradufu ifikapo mwaka 2030, kwani wafanyakazi wapya karibu milioni moja huingia soko la ajira kila mwaka. Kazi – kwa maana ya ajira zenye tija – inabidi zitengenezwe kwa kasi na kupewa kipaumbele. Mpango wa nguzo tatu wa kujenga ajira nchiniTanzania ni matokeo ya mchakato uliokuwa na ushirikishwaji wa kina. Ni dhahiri mchakato huu umehusisha ushirikiano mpana kati ya Benki ya Dunia na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wadau wengine mbalimbali pia walihusishwa katika mashauriano katika majukwaa tofauti, ikijumuisha mikutano na wamiliki wa biashara wa Kitanzania katika sekta isiyo rasmi na iliyo rasmi, pia na wawekezaji wa kigeni. Rasimu ya mpango kazi pia ilijadiliwa na wawakilishi kutoka takribani Wizara zote, na kuwasilishwa kwa vikundi tofauti katika majukwaa yaliyoandaliwa na REPOA na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation). Aidha, majadiliano yaliyolenga mada mahususi yalifanyika katika Warsha za Mazingira ya Biashara kama sehemu ya programu ya “Matokeo Makubwa Sasa”, na warsha iliyoandaliwa katika jiji la Washington DC iliyowaleta pamoja watunga sera wa juu nchini na wataalamu kutoka Benki ya Dunia, pia na Vyuo Vikuu vinavyoongoza. www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 5 Tunahitaji Ajira Zenye Tija K ipato changu kutokana na kilimo hakikidhi mahitaji yangu siku hizi” analalamika Robert Umala, mkulima kijana kutoka Magharibi mwa Tanzania, “marafiki zangu wote wanakimbilia mijini kwenda kufanya biashara. Kuna maisha mazuri ya baadaye kule.” Kupata kazi yenye mshahara mzuri ndio matarajio ya takribani Watanzania 800,000 wanaoingia soko la ajira kila mwaka. Historia ya hivi karibuni inaonyesha kwamba kuendeleza ajira ndio jambo kuu kwa ustawi wa kiuchumi na utulivu wa kisiasa. Huu ndio uzoefu kutoka nchi za Asia ya Mashariki – China, Thailand na Vietnam zote zimeweza kujenga ajira nyingi zenye mishahara mizuri kwa kipindi cha muda mrefu. Ili kukabiliana na changamoto za kujenga ajira, itabidi Tanzania ifanye mageuzi. Leo hii, Watanzania wengi wameajiriwa, lakini ni katika shughuli zilizo na kiwango kidogo cha tija. Katika maeneo ya vijijini, shughuli zimejikita kwenye mashamba, ambayo uzalishaji wake ni wastani wa mara tano chini ya uzalishaji nchini China. Katika miji, wananchi huendesha biashara ndogo ndogo ambazo ni za kujikimu zaidi kuliko ujasiriamali wa ‘kweli’. Ili kutoa nafasi kwa nguvukazi inayokua kwa kasi kuingia katika ajira zenye tija, haitoshi kwa uchumi wa nchi kukua kwa haraka katika kipindi cha miaka 10 ijayo, bali pia inatakiwa kuhamisha nguvu kazi yake ambayo iko katika sekta zisizo na tija kwenda sekta zenye tija. 6 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Kwa nini tunaweka msisitizo katika ajira? Tanzania ina changamoto kuu 3 Viwango Ongezeko la Uhamiaji vya juu vya watu kutoka vijijini umasikini kuja mijini Umasikini Wengi ni vijana, zaidi ya Watu wakihama umekwama katika 700,000 huingia soko la kuelekea mijini - > 30% na watunga sera ajira kila mwaka mabadiliko katika wakitafuta njia za kazi na matarajio ya kuongeza ajira kazi Nguvukazi ya Tanzania inayokua kwa haraka ikilinganishwa na punguzo dogo katika umasikini 45 25 40 35 20 Nguvu kazi (mamilioni) 30 % Umasikini 15 25 Kutoka: Benki ya Dunia & Utafiti Bajeti ya Kaya 20 10 15 10 5 5 0 - 19 19 19 19 19 20 20 20 20 20 20 20 90 92 94 96 98 00 02 04 06 08 10 12 % Umasikini Idadi ya nguvu kazi www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 7 Tanzania itabidi ikue kwa haraka zaidi ili kuzifikia nchi ...na kubadili muundo wake wa ajira. zinazoibuka kiuchumi…. 5500 Kipato cha kila mfanyakazi, Dola 2005 9.8% kwa mwaka 4500 3500 7.6%kwa mwaka 2500 1500 4.5% kwa Kutoka: Benki ya Dunia & ILO mwaka 500 06 08 10 12 14 16 18 20 22 24 26 20 20 20 20 20 20 20 20 20 20 20 Makadirio ya ukuaji wa kihistoria, Dola 1943 mwaka 2016 Ukuaji unaohitajika ili kui kia Indonesia 2009, Dola 3374 Ukuaji unaohitajika ili kui kia Thailand 2009, Dola 5057 Leo hii, Watanzania wengi wameajiriwa kwenye makampuni ...ambayo hayana tija wala faida madogo Dola 31. 4 Kutoka: Taasisi ya Taifa ya Utafiti mara 4.9 Wastani wa faida kwa Tofauti ya uzalishaji katika biashara isiyo tokana na mashamba kati ya China na kilimo (Dola kwa mwezi) Tanzania 8 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Makampuni hujenga ajira Mpango wa nguzo tatu wa kukuza ajira Utafiti huu unawasilisha mpango wa nguzo tatu wa kujenga ajira Tanzania hususani katika makampuni na kwa misingi ya imani kwamba ajira hujengwa na sekta binafsi yenye nguvu. Nguzo ya kwanza inalenga kujenga ajira kwa mtazamo wa biashara ndogo zisizohusiana na kilimo, ambazo zimekuwa zikikua kwa haraka sana wakati wa kupanuka kwa haraka kwa miji yetu. Nguzo ya pili inaweka msisitizo kwenye mashamba kwa sababu hayo ndiyo yenye sehemu kubwa ya ajira nchini Tanzania, wakati nguzo ya tatu, inajadili uwezo wa kujenga ajira kunakohusiana na kupanuka kwa biashara na kuingia kwenye masoko mapya. Mkakati huu wa kujenga ajira unajenga hoja ya kuondolewa kwa vikwazo vikuu vinavyozuia kukua kwa biashara za Kitanzania. Hili si jambo dogo, kwani nchini Tanzania, vikwazo hivi ni vigumu sana. Vikwazo vinajumuisha muunganisho dhaifu kwenye masoko, upatikanaji finyu wa mikopo, ukosefu wa umeme wa uhakika, ujuzi mdogo wa watu walio wengi. Mpango unaelekeza kwamba vikwazo hivi – au njia zakuvishughulikia – zinaweza kutofautiana baina ya aina tofauti za biashara. Kwa mfano, ujuzi unaohitajika kwa biashara zenye tija ambazo www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 9 hazihusiani na kilimo, za kilimo na za wasafirishaji wa bidhaa nje sio sawa. Upatikanaji wa ujuzi unaohitajika pia unatofautiana kutegemea mahali, shughuli, na viwango vya elimu ya awali ya wamiliki wa biashara na wafanyakazi. Kanuni hii pia hutumika katika sekta nyingine kama vile miundombinu, ardhi na vifaa. Mapendekezo ya sera yanahitaji kiwango fulani cha taarifa mahususi ili mkakati uliopendekezwa uwe na ufanisi. Kwa kila moja ya nguzo hizi tatu, hatua mahususi zinapendekezwa kwa lengo la kuimarisha msingi wa kiuchumi na mazingira shindanishi ambayo ni muhimu kwa biashara kushamiri na kutengeneza kazi zenye tija. Uzoefu katika utendaji wa kimataifa utatumika pale inapowezekana. Ingawa hatua hizi zilizopendekezwa haziwezi kushughulikia vikwazo vyote vinavyoyakabili makampuni nchini Tanzania, zinatoa mwelekeo wa vipaumbele vinavyohitajika zaidi. Mpango huu pia unajaribu kuweka uwiano kati ya hatua mtambuka na zile ambazo zinalenga eneo mahususi. Kwa kila nguzo, sekta mahususi inayoonyesha uwezekano wa kukua ilitambuliwa kama ndiyo kipaumbele kwa Tanzania. Kulenga sekta mahususi kunaweza kuisaidia Tanzania kuanza haraka zaidi kukua kwake katika uzalishaji, ajira na kuuza bidhaa-nje na kuleta manufaa haraka zaidi.1 Kwa kutumia mchanganyiko wa mbinu mbalimbali za uchambuzi pia kuchunguza uwezo wa uhitaji wa nchi na nchi jirani na athari zake kwenye ajira, Mpango uliopendekezwa sekta ndogo tatu zimewekewa msisitizo kutokana na uwezo wake wa kukua: umeainisha mambo 12 muhimu yaliyopangwa kwenye (i) viwanda vya ngozi kwa ajili ya kupanuka kwa biashara ndogo; misingi 3 ili kuongeza kazi (ii) mboga zenye thamani ya juu kwa ajili ya mashamba; na zenye tija nchini Tanzania (iii) utalii kwa ajili ya huduma za mauzo ya bidhaa nje ya nchi. Haya yote yachukuliwe kama ni mifano elekezi tu na sio kuwa ni mifano toshelezi ya sekta zinazokua. Wakati sekta nyingine zenye uwezo wa juu zimetajwa katika ripoti hii, uchunguzi wa kina wa uwezo wa fani /sekta kukua na kuongeza ajira uko nje ya wajibu wa ripoti hii. Wakati kila nguzo ina umuhimu wake wa kipekee, ni matumizi ya nguzo zote kwa pamoja ndiyo ambayo hasa yatakayoleta matokeo makubwa zaidi. Kwa kiwango kikubwa, uwezo wa Tanzania wa kujenga ajira utategemea katika kuboresha mazingira ya kampuni ndogo zinazofanya shughuli katika maeneo ya mijini. Hata hivyo, uwezo huu pia utategemea mafanikio ya sekta ya kilimo, ambayo sio tu inapaswa kuzalisha chakula kingi zaidi kwa idadi ya watu mijini inayoongezeka, lakini pia ijenge fursa za kazi na kukuza maendeleo katika miji midogo na majiji yanayoambatana nayo. Ukuaji wa kazi za mijini katika viwanda vya usindikaji utatokana kwa sehemu kubwa na upatikanaji kwa gharama nafuu kwa pembejeo, ikijumuisha chakula, pamba, mbao na ngozi. Wasafirishaji wa bidhaa nje wanaweza kuongeza ajira kwa kuyafikia masoko mapya, na wakati huo huo, kusaidia kuharakisha kupevuka kwa makampuni madogo kwa kutoa motisha wa ziada kwa ajili ya kuwekeza na kushindana katika masoko ya ndani na nchi jirani. Kukuza aina hizi za mahusiano inapaswa kuwa kipaumbele cha watunga sera. 1. Angalia “Growth Diagnostics”, R. Hausmann, D. Rodrik, na A.Velasco, JFK Kennedy School of Government, Harvard University, Cambridge, 2005. 10 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 11 Nguzo 1 Kusukuma biashara ndogo ambazo hazitokani na kilimo kukua Leo hii kuna takribani biashara milioni tano ambazo hazihusiani na kilimo nchini Tanzania, nyingi kati ya hizi ni biashara za kaya. 2 Idadi hii inakua haraka kwa takribani asilimia 10 – 15 kwa mwaka, ikichochewa na kupanuka kwa miji na ukosefu wa njia nyingine za ajira kwa Watanzania walio wengi. Kutokana na hali hii, karibu nusu ya biashara ambazo hazihusiani na kilimo leo hii ziko mijini. Ni biashara ndogo sana (asilimia 95 zinaripoti kuwa na wafanyakazi chini ya wawili, ukijumuisha mmiliki) na hazina ustadi maalumu, na zina desturi ya kufanya kazi kwa masaa machache kwa siku au siku chache kwa wiki. Biashara nyingi za aina hii hupotea haraka na kuibuka tena chini ya jina tofauti, na wakati mwingine, hujihusisha katika shughuli za aina nyingine. Nyingi kati ya biashara hizi ndogo huwa hazilengi katika kukua. Hata hivyo, iwapo asilimia 18 tu ya idadi ya biashara hizi zitapanua maradufu misingi yao ya ajira katika mwaka mmoja, takribani ajira milioni moja zitatengenezwa nchini. Idadi hii sio ndogo. Inaonyesha umuhimu wa kauli kwamba makampuni madogo yanaweza kuwa njia kuu za kukuza ajira nchini Tanzania, kama inavyoshuhudiwa katika chumi nyingi za nchi zenye viwanda na nchi zinazoibukia. Ili kampuni ndogo zipate msukumo wa kukua, mchanganyiko wa hatua nne unahitajika. Kwanza, wamiliki wa biashara wanapaswa kuwa na uwezo wa kukuza rasilimali kuu mbili – ujuzi wao wenyewe na mtaji wa kudumu. Pili, wanapaswa kuwa na mawasiliano mazuri ya karibu na ya kimtandao na wasambazaji wa bidhaa na pembejeo na wateja wao. Tatu, wanapaswa kuweza kuepuka kutumia rasilimali zao adimu katika malipo yaliyopitiliza kwa watendaji wa serikali na katika mikakati ya kumudu kufanya shughuli katika mazingira yasiyo salama. Mwisho, wanapaswa kufanya kazi pamoja ili kufikia ukubwa bora wa biashara unaohitajika ili kuongeza uwezo wa ushindani wa pamoja. 2. ‘Biashara za Kaya’ kama zinavyofafanuliwa katika chapisho la Kweka, J. & L. Fox (2011) ni biashara ndogo ambazo si za shamba zisizo rasmi zinazomilikiwa na kaya. Biashara hizi zinajumuisha watu waliojiajiri wenyewe wanaoendesha biashara zisizo rasmi na wana familia wanaofanya kazi katika biashara hizo. 12 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Kulenga programu za mafunzo ili kuharakisha upatikanaji wa ujuzi kwa Hatua 1: kuunganisha programu za fedha na mafunzo kwa wajasiriamali vijana. Jenga uwezo wa wamiliki wa biasha- Toa huduma za nje za kifedha na kihasibu kwa wamiliki wa biashara ndogo ra ndogo kwa ambao hawawezi kulimbikiza ujuzi wote wa kitaalamu na usimamizi. kuendeleza ujuzi na mtaji wa kudumu Tayarisha mikataba rahisi na mamlaka za mitaa kusaidia wamiliki wa biashara ndogo kupata eneo la kazi na kuwahimiza kuwekeza katika mtaji wa kudumu. Hatua 2: Rahisisha usa ri katika Boresha matumizi ya maeneo kwa ajili ya kanda za viwanda na biashara, pia miji kwa kupunguza korido za usa rishaji mijini, ukiweka umuhimu maalumu kwa miji ya pembezoni. gharama za msongama- no katika majiji, ambao Fanya uwekezaji wa kimkakati na kutoa motisha ili kuvutia njia za usa rishaji wa unaweza kupunguza hadi pamoja (hii ni pamoja na treni na mabasi yaendayo kasi). theluthi ya kipato anachoingiza mfanyakazi Punguza umbali wa kusa ri kwa kuhimiza matumizi ya mtandao kupitia teknolojia wa kawaida jijini Dar es mpya za mawasiliano (kushirikishana habari, malipo, n.k.). Salaam Hatua 3: Ziba pengo kati ya wafanyabiashara wadogo na utawala wa mtaa kwa Punguza kiasi cha kuimarisha uwezo wao na kurahisisha taratibu zilizopo. rasilimali zinazotumiwa na kampuni ndogo Toa motisha za ustadi kwa wafanyabiashara wawekeze kuboresha usalama kwenye gharama za kupitia kushirikishana habari, kuchangia fedha kwa miundombinu ya pamoja, na utawala na ulinzi ili kuboresha udhibiti wa vikwazo kwa wakosaji. waelekeze rasilimali hizi katika shughuli za uzalishaji Tekeleza sheria, punguza uwezekano wa tabia za kudai kodi zinazofanywa na utawala na mawakala, na simamia utekelezaji wa adhabu. Hatua 4: Kukuza matumizi ya wafanyakazi wa mikataba mifupi kwenye kampuni ndogo kwa Ongeza kiwango cha kupunguza gharama za kuwatafuta na kuboresha kanuni za kazi. biashara ili kupunguza gharama za uendeshaji Kukuza vyanzo vya nje vya fedha ambavyo si rasmi kwa kupunguza gharama za kwa kutumia vyanzo vya kujiunga kwa watoa huduma na watumiaji. nje vya nguvu-kazi na fedha na kujenga fursa za Jenga vyama vya biashara ndogo ndogo/vinavyotarajiwa na kuimarisha vyama ushirikiano vilivyopo ili kupunguza gharama zisizobadilika zinazoambatana na programu za mafunzo, fedha, na huduma nyingine. www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 13 Kuelekeza nguvu katika sekta ya ngozi Uzalishaji wa viwanda vyepesi – ngozi: Wakati biashara ndogo kimsingi zinaweza kustawi katikashughuli nyingi, ni sekta chache tu ndizo zinazoonekana kuwa na uwezo wa kiushindani nchini Tanzania. Utafiti huu unachunguza sekta ya ngozi, ambayo tayari inaonekana kuwa na uwezo wa kiushindani kwa viwango vya kimataifa. Kwa mfano, gharama za kuzalisha jozi ya viatu vya ngozi leo hii ni pungufu kwa asilimia 20 nchini Tanzania ikilinganishwa na China. Hata hivyo, sekta ya ngozi imeshindwa kuendelea katika miaka ya hivi karibuni kutokana na vikwazo mbalimbali. Hatua zifuatazo zinazolenga kuondoa vikwazo hivyo zinaweza kuleta mabadiliko:  Kuinua ubora (ujuzi na viwango) wa ngozi kwa kutoa msaada wa kitaalamu kwa wafugaji kupitia vyama vyao  Kukuza uwekezaji mpya katika mkusanyiko wa viwanda vinavyoleta mabadiliko, ambavyo vitajengwa karibu na wagavi na/au masoko ya wateja. Hii itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na kuboresha upatikanaji wa nishati nafuu na ya uhakika, pia na kukuza nguvu kazi yenye ujuzi.  Kupunguza (na taratibu kuondoa) kodi ya mauzo ya nje kwenye ngozi ghafi kwa lengo la kukuza hatua kwa hatua ushindani katika bei na ubora wa pembejeo. 14 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Nguzo 2 Kukuza tija mashambani Kilimo ni shughuli kuu ya Watanzania wengi. Leo hii kuna mashamba takribani milioni sita, yanayotoa ajira kwa takribani 3/4 ya nguvu kazi. Kwa siku za mbeleni, ajira katika sekta hii inaweza kuongezewa nguvu kwa kupanuliwa kwa kilimo katika maeneo ambayo hayajalimwa. Hata hivyo, mkakati huu unaweza kukumbana na kikwazo kwamba sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba tayari iko katika maeneo yenye watu wengi na miradi mikubwa ya miundombinu itahitajika ili kuunganisha mashamba mapya na masoko. Ili Tanzania ifanikiwe, inahitaji kuboresha tija katika mashamba yake haraka. Mashamba mengi ya Watanzania yana tija ndogo (kwa mfano, mavuno ya mahindi kwa wastani ni mara tano chini ya yale ya nchini China) ilhali kuna nafasi kubwa ya kufanya maboresho. Iwapo katika kipindi cha muda mrefu ujao sekta ya kilimo yenye tija itatumia wafanyakazi wachache zaidi, basi uwiano kati ya nguvu kazi na teknolojia mpya unaweza kukuzwa wakati wa kipindi cha mpito. Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Vietnam na Thailand zimeonyesha kwamba kuongezeka kwa tija kunaweza kwenda sambamba na kujengwa kwa ajira mpya, hususani kazi zenye tija katika sekta ya kilimo. Uzalishaji bora wa chakula pia utasaidia kukuza maendeleo ya viwanda vya usindikaji na biashara za bidhaa za kilimo – sekta inayoweza kutoa ajira nyingi nchini Tanzania. Hatua nne shamirishi zinapendekezwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mashamba ya Tanzania. Hatua zote hizi zinalenga katika kuwaunganisha wakulima na masoko, kwa vile kilimo cha kibiashara ndio njia bora zaidi ya kuongeza kipato chao. Ni kweli, kwamba kilimo cha biashara kinaambatana na viwango vya juu vya Katika miongo miwili iliyopita, tija, na mashamba kwa ajili ya biashara yana uwezekano mkubwa Vietnam na Thailand wameonyesha zaidi wa kuzalisha bidhaa za thamani kubwa, ambazo hujenga ajira kwamba mafanikio katika tija zenye tija zaidi kuliko mazao ya asili. Ili kuongezea nguvu sekta hii, Tanzania inahitaji kupunguza gharama za usafirishaji, kuhimiza yanaweza yakaambatana na matumizi ya pembejeo za kisasa, na kuwaunganisha wakulima kutengeneza ajira hasa ajira zenye na mifumo yenye thamani na ufanisi, na kuhakikisha juhudi hizi tija katika sekta ya kilimo hazikwamishwi na sera zinazobadilika badilika. www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 15 Fanya uwekezaji wa kimkakati katika barabara za vijijini, kupunguza gharama za usa ri, na kuongeza muunganisho wa miundombinu kupitia Ubia baina ya Sekta Binafsi na za Umma. Hatua 5: Kuunganisha Kupunguza gharama za kudumu za usa rishaji kwa kukuza ushirikiano miongoni mwa wakulima wadogo, maghala ya kuhifadhi bidhaa ya pamoja, na taratibu za wakulima kushirikiana gharama. waliotengwa na masoko Kukuza ushindani miongoni mwa wafanyabiashara kupitia taarifa za masoko, kupunguza vikwazo vya kuingia sokoni, na usimamizi sahihi wa kanuni. Toa msukumo kwa skimu za kisasa za umwagiliaji kupitia ubia na jamii na Hatua 6: wasambazaji wa eneo husika. Kukuza matumizi ya pembejeo bora ili Saidia upatikanaji wa mbolea na mbegu bora kwa kuondosha matumizi ya kuongeza mavuno vocha na kuanzisha kilimo cha mkataba na matumizi ya zana za TEHAMA. kwa hekta kwenye mashamba Oanisha viwango vya ubora kitaifa na nchi jirani kwa pembejeo za kilimo na bidhaa za chakula. Ongeza uwezo wa kujadili bei kwa wakulima kwa kutoa habari kupitia simu za Hatua 7: mkononi na njia nyingine za TEHAMA. Kukuza usawa na ufanisi kupitia Himiza uwekezaji katika kilimo cha mkataba katika baadhi ya sekta ili kuwezesha taratibu zinazotokana upatikanaji wa kipato cha juu, mikopo, fedha, pembejeo na programu za ugani. na soko Kulegeza masharti ya kuuza soko la nje ili kusaidia wakulima kutegemea masoko Hatua 8: ya nje bei za chakula zinapopanda. Kuhakikisha uwazi na sera imara ili wakuli- Kupunguza kodi, pakiwa na msisitizo katika kupunguza "ushuru" unaowaumiza ma wasiadhibiwe sana wakulima na kukusanywa na mamlaka za mtaa ambayo huweza ku kia hadi asilimia tano ya uzalishaji wa kibiashara. Kushughulikia mapungufu katika haki za ardhi na mali kupitia kuanzishwa kwa masijala za ardhi za wilaya na kuleta ufanisi katika kumbukumbu za ardhi. 16 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Kuelekeza nguvu katika sekta ya kilimo Biashara ya kilimo – mboga zenye thamani ya juu: Maendeleo ya mashamba yenye tija sio tu yatainua uzalishaji wa kilimo na ajira, lakini pia yataleta pembejeo bora, ambazo hatimaye zitatumika kuzalisha bidhaa zilizoongezewa thamani. Uwezo wa kilimo na biashara ya kilimo ni mkubwa kwa Tanzania, lakini matarajio lazima yawekwe inavyostahili. Sehemu kubwa ya sekta hii kwa sasa haina uwezo wa kushindana kwa sababu ya gharama kubwa na ubora hafifu wa pembejeo. Uzalishaji wa mboga na matunda yenye thamani kubwa, hata hivyo, inaonekana kama ni fursa halisi, kwani iko juu katika orodha iliyoandaliwa na zana zote za uchambuzi zilizotumika katika utafiti huu ambao unatambua faida zilizopo na ambazo hazijatumika. Sekta ndogo hii imefanya vizuri katika miaka ya karibuni kwa kuzingatia mahitaji yanayokua katika masoko ya ndani, nchi jirani na kimataifa. Hatua zifuatazo zinapendekezwa ili kuinua shughuli hii:  Kuendeleza kilimo cha mkataba kati ya mashamba na kampuni za usindikaji. Mikataba hii itayarishwe ili kuwezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea) na mafunzo kwa wakulima, wakati wasindikaji waweze kupata bidhaa zenye ubora wa juu.  Kuharakisha uanzishwaji wa viwanda vilivyo karibu karibu kuzunguka eneo la kimkakati, ambalo litatumia faida ya kuweza kupata usafiri kwa urahisi na teknolojia, pia na kubadilishana ujuzi kupitia shughuli za ubia. Sehemu moja ambayo inaweza kuwekewa mkazo inapaswa kuwa mkoa wa Kilimanjaro/Arusha, ambao una faida ya kuwa karibu na Kenya.  Kukuza bidhaa zenye ubora kwa kuboresha muundo wa udhibiti na kuratibu programu za kujenga uwezo kwa wakulima kuhusu viwango vya ubora na usafi.  Kuhimiza sekta ya vifungashio vya bidhaa. www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 17 Nguzo 3 Kuelekea masoko ya nje Makampuni ya ndani yanayopanuka na kuingia katika masoko ya nje yana uwezekano wa kutengeneza ajira. Pia yanatarajiwa kunufaika kwa kuingiza teknolojia ambayo sio tu itaongeza uzalishaji wake, lakini pia hata ule wa makampuni mengine ya ndani yanayofanya nayo biashara. Mkakati huu umekuwa nyenzo muhimu katika kutengeneza kazi zenye tija katika chumi zinazoibukia, hasa za Asia Mashariki. Licha ya kukua kwa haraka kwa bidhaa zinazouzwa nje katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, wasafirishaji wa bidhaa nje wa Kitanzania bado wanahitaji kuongeza jitihada kuzifikia nchi nyingine. Ni kampuni moja tu kati ya makampuni 10,000 ndio huuza bidhaa zake katika masoko ya nje ukilinganisha, kwa mfano, kampuni moja kati ya makampuni 500 nchini Marekani. Wasafirishaji wa bidhaa nje kwa kawaida wanazalisha zaidi kuliko wasiosafirisha bidhaa nje. Hata hivyo, wakati baadhi ya makampuni yaliundwa yakiwa makubwa ili kuuza bidhaa nje, hasa katika madini, kampuni nyingine zilikua hatua kwa hatua. Zilianza kwa kuuza katika soko la ndani, taratibu yakaingia masoko ya nchi jirani na kimataifa. Wasafirishaji wengi wa bidhaa nje wa Kitanzania wamepitia mchakato huu wa kukomaa katika miaka ya hivi karibuni. Hatua nne za kuongeza nguvu zinapendekezwa kuhimiza makampuni ya ndani kuharakisha mabadiliko kuelekea masoko ya nje. Mchakato huu utahitaji makampuni haya kujionyesha zaidi na kuwa rasmi zaidi, kuinua ubora katika uzalishaji, kujiunga kwa ufanisi na masoko ya nje, kufikiria soko la nchi jirani angalau katika awamu ya kwanza ya kupanuka kwao. 18 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania Kuwezesha upatikanaji wa fedha kupitia vyanzo rasmi ili kupunguza gharama za Hatua 9: habari (Masijala ya Vitambulisho, taasisi za mikopo), kutayarisha zana za Kuyatoa makampuni kutoka kwenye sekta kujikinga na hasara (kulinganisha ruzuku, karadha), na kuimarisha uwezo wa isiyo rasmi kwa kuyapa wafanya biashara ya nje kuomba mikopo. vivutio yaweze kuuza nje, yarasimishe shughuli zake Kuboresha upatikanaji wa habari kuhusu masoko yanayotarajiwa kupitia kushirikishana mitandaoni. Kukuza viwango kupitia mafunzo na programu za kushirikishana habari, kwa ubia wa karibu na makampuni binafsi. Hatua 10: Kuongeza ujuzi kupitia mafunzo kazini na programu za ufundi pia za kitaalamu. Kukuza ubora katika uzalishaji wa bidhaa Kuhimiza upatikanaji wa teknolojia kwa ubia na wawekezaji wa nje. Kuingiza teknolojia na vifaa kutoka nje, na miundombinu ya pamoja. Hatua 11: Kufanya bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa na, baada ya muda mrefu Kuboresha muunganisho kujenga miundombinu mpya kuwiana na msongamano wa Dar-es-Salaam (kama na upatikanaji wa soko kupitia maboresho katika vile bandari kavu) na kutanuka kwenda bandari mpya (k.m. Bagamoyo). miundombinu ya kawaida na mtandao, pia kupitia matumizi ya Kujenga kanda maalumu za kiuchumi ili kunufaika na upatikanaji wa usa ri na kanda maalumu za miundombinu na masoko ya umeme. kiuchumi Kujenga korido za majimbo, pakiwa na ukarabati maalumu wa reli katika korido ya kati. Hatua 12: Kutilia maanani soko la nchi jirani ili kukuza Kupunguza vikwazo ambavyo si vya ushuru kwa kuendeleza matumizi ya bidhaa nje ukichukulia TEKNOHAMA mipakani, miundo bora ya rufaa za kodi, kurasimisha taratibu katika mchango wake katika mifumo ya bidhaa za kielektroniki na bidhaa za kilimo. ajira katika miaka michache iliyopita Kukuza biashara ya nje na nchi jirani kwa kutoa msukumo zaidi kwa vile ambavyo tayari vinauzika,’ ikiwemo mabomba, simenti, vioo, mchele na utalii. www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 19 Kuelekeza nguvu katika sekta ya utalii Huduma – utalii: Jumla ya mauzo ya huduma za utalii nje yamekuwa kwa haraka (zaidi ya asilimia 15 kwa mwaka katika miaka ya 2000) na matarajio ni mazuri katika bidhaa na huduma. Pia kuna fursa nyingi katika uzalishaji wa viwanda vyepesi na kilimo, kama inavyosisitizwa na mchanganyiko wa mbinu zilizotumika katika utafiti wa ripoti hii, pia fursa zinazotokana na maendeleo ya akiba ya gesi asilia baharini kusini mwa nchi. Ijapokuwa kuvunwa kwa akiba ya gesi asilia hakutarajiwi kujenga kazi nyingi za moja kwa moja, kuna fursa za kutengeneza ajira wakati wa awamu ya ujenzi, na kwa namna ambayo si ya moja kwa moja zaidi, kupitia kuibuka kwa mahusiano ya mbele na nyuma na makampuni ya nchini. Katika hatua hii, hata hivyo, jambo la kuzingatia mara moja inapaswa kuwa kwenye huduma kama vile utalii, ambapo Tanzania tayari inamiliki sifa ambazo hazijatumika katika huduma za kupitisha watalii (kwani Tanzania ni kitovu cha nchi jirani), na kuna uwezo mkubwa wa kujenga ajira kupitia matokeo ya kuongezeka kwa utalii (moja kwa moja au kwa njia nyinginezo) kunakoambatana na maendeleo yake. Kukuza uwezo wa utalii kuongeza ajira, hatua zifuatazo zinapendekezwa:  Kuboresha sera na mazingira ya kitaasisi kwa kupitia upya Sera ya Utalii (1999) na Sheria ya Utalii (2008) kwa ushirikiano wa karibu na sekta binafsi.  Kukuza mazingira wezeshi kwa ukuaji wa sekta binafsi katika biashara ya utalii kwa kupanga upya taratibu za leseni na udhibiti.  Kujenga mahusiano kati ya sekta ya utalii na uchumi wa ndani kwa kuimarisha uwezo wa wenyeji, ikijumuisha ngazi ya jamii, kwa kutoa huduma ya chakula, malazi na huduma nyingine kwa watalii.  Kujenga bidhaa na vivutio tofauti vya watalii, zaidi ya maeneo yaliyozoeleka sana ya Kaskazini na Zanzibar, kwa kukuza maendeleo ya miundombinu na kuongeza ubunifu katika kutangaza masoko pamoja na nembo ya kipekee, msisitizo ukiwa maeneo ya Kusini. 20 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 21 Hatua za Baadaye M pango kazi uliopendekezwa unatambua hatua kuu 12 zilizoandaliwa zikizingatia nguzo kuu tatu ili kukuza utengenezaji wa kazi zenye tija nchini Tanzania. Kwa wengi, idadi hii inaweza kuonekana kuwa kubwa sana (hasa ukichukulia kwamba hatua hizi zimegawanywa tena katika hatua nyingine zaidi, kipengele kwa kipengele). Hata hivyo, changamoto ya ajira zenye tija haiwezi kukidhiwa kiuhalisia kwa hatua chache za juu juu. Ni suala ambalo kiasili ni mtambuka na ukubwa wa mageuzi yanayohitajika kuhimiza kujenga kazi zenye tija kunahitaji matumizi na utekelezaji wa mpango kazi jumuishi. Shabaha ya utafiti huu ni kuchangia katika mjadala kuhusu kujenga ajira nchini Tanzania kwa kupendekeza mwelekeo katika kutunga sera. Ni pale tu muafaka unapofikiwa miongoni mwa wadau ndipo utekelezaji wa hatua zilizochukuliwa utakapojadiliwa kwa kina, ikiwemo muda, fedha, na kugawana majukumu miongoni mwa wakala, wizara zinazotekeleza, wabia wa maendeleo, na sekta binafsi. Hatua hii inayofuatia itakuwa muhimu kwani vitendo vinakuwa havina maana kama havitekelezeki. 22 Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija www.worldbank.org/tanzania www.worldbank.org/tanzania Tanzania: Tunahitaji Ajira Zenye Tija 23 BENKI YA DUNIA